Tukio la Lissu: Dhana 3 za msingi ambazo zinatokana na ‘mchujo’ wa dhana mbalimbali

Tukio la Lissu: Dhana 3 za msingi ambazo zinatokana na ‘mchujo’ wa dhana mbalimbali

matokeo yanapo kuwa tofauti na matarajio nq hakuna namna ya kubadili mchungaji lazima apakwe damu ya kondoo kuuziwa kesi ya kondoo aliyeraruriwa ukizingatia kondoo hakuwa kipenzi cha mchungaji!! DEEP STATE aka wenye nchi yao
 
Viongozi wa Chadema walitoa tahadhari mapema wakidai kuna mtu aliomba kumuua Tundu Lissu kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook. Hili ombi kwenye mtandao wa facebook lilitokana na tuhuma nzito toka serikalini kupitia viongozi mbalimbali kuwaaminisha wananchi kuwa Mh. Tundu Lissu ni ''adui wa taifa'', siyo mzalendo, kikaragosi wa mabepari, anahujumu juhudi za viongozi n.k


Source: BongoStars
 
Published on 8 Sep 2017
IGP Sirro kaongelea ishu ya Tundu Lissu kupigwa risasi
Kamanda wa Polisi Tanzania IGP Simon Sirro amekutana na wanahabari kuzungumzia ishu za usalama likiwepo tukio la kushambuliwa Mbunge Tundu Lissu.

 
Those who kill for partisan ends cannot be patriots
Patriotism and nationalism are two different concepts. We must not confuse the two. It is not unpatriotic to oppose the government when it is behaving dishonestly, foolishly or viciously.

The State and Institutions including courts should not test patriotism. Our patriotism is tested on a daily basis by our activities in the way we live and the way we deal with each other. A soldier’s patriotism is tested when he is confronted with the enemy and is willing to risk his life to save the identity of which he is an integral part.

The patriotism of a lawyer is tested when he is, despite opposition, prepared to protect the victims of injustice. A doctor will emotively demonstrate his patriotism when he goes out of the way to save lives though in the process he might endanger his own. A patriotic businessman will not participate in transactions that are dishonest and adversely impact the economic interests of his country. Smugglers, terrorists and perpetrators of violence who kill for partisan ends cannot be patriots.
By Kapil Sibal is a former human resource development minister

Source: Those who kill for partisan ends cannot be patriots
 
*Evarist Chahali* anaandika:

Jana, Septemba 07, 2017, majira ya mchana, zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Singida Mashariki, Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma, wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D, inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana.

Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu, na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema, chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa.

Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100, kwa kimombo wanasema “intelligence is not an exact science.”

Okey, sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana na‘mchujo’ wa dhana mbalimbali.

Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa ‘akiisumbua mno’ serikali, ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli, ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi.

Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa ‘mwiba mchungu’ kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu.

Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu, Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa.

Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.”


Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta ‘kulaumiwa bure.’ Kwa sababu, Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space).

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo ‘anawachukia wapinzani’ hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela.

Katika hotuba zake mbalimbali, Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu, Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo

“Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni, waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote, sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni, ukishamfukuza hata mwezi mzima… atakuja aropokee huku, na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao, wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele…. ni nafuu unyamaze ukalale.”

Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani, hususan wa Chadema, dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ‘ready-made.’

Hata hivyo, pamoja na ‘dalili zote’ kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu, dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa, sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri, lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu.

Na hata kama ingekuwa lazima ‘aondoke,’ basi kuna ‘njia mwafaka zaidi’ za mauaji ya watu maarufu (assassination), huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi.

Halafu kinachotatiza katika tukio la jana, na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba ‘kuna mkono wa serikali,’ ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu.

Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla, unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema.

Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu, hususan ndani ya chama chake.

Udhaifu wa dhana hii ni kwamba, kama ambavyo kwenye dhana ya kwanza, hakuna tija katika kumdhuru Lissu hadharani. Kwamba hata kama kungekuwa na lundo la wapinzani wa kisiasa wa Lissu huko kwenye chama chake, kwanini wafanye ‘operesheni’ hiyo waziwazi badala ya kuandaa mkakati wa siri?

Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza, hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika, kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya ‘kusaka publicity kwa nguvu’?

Hiyo inatuacha na dhana moja, ya tatu, na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita ‘rogue elements.’ Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine.

Kuna kitu kinachofahamika kama ‘Deep state.’ Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu ‘deep state’ lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii – mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola, wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule, lakini zaidi chama kilichopo madarakani.

Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli, ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti ‘chuki zake’ dhidi ya wapinzani, anawapa nafasi nzuri ‘wabaya wake’ kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake.

Ndio maana dhana ya kwanza – kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu – inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made.”

Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi, wenye nguvu, na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli, hawatosita kufanya hivyo.

Lakini kwa vile ni ‘vigumu mno’ (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo, njia nyepesi inaweza kuwa katika ‘kuua character yake,’ ambayo bahati nzuri kwa ‘wabaya wake,’ sio nzuri sana.

Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu, sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo, ni rahisi kwa ‘wabaya wa Magufuli’ kutumia mwanya huo kujenga picha ya “serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa.”

Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa ‘Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao, na ikibidi hata kuwaua.’

Kwahiyo, kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumng’oa, na kwa vile ‘njia za kawaida’ sio rahisi, basi inakuwa ‘anything goes,’ liwalo na liwe.

Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu, tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity, yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba “mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa ‘wabaya’ wake.”

Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza, lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu, ikiwa ni pamoja na “yanayojiri nyuma ya pazia.”

Pili, lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu “nani ana/wanahusika.”

Mwisho, kama nilivyotanabaisha awali, tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo, japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi, sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100.

Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika, sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki.
You are so smart, kwani wengine wanaandika tu kwa hisia.

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Nilileta mada yenye msingi huu ikatiwa kapuni ....I wish ningekuwa ni maarufu kule twitter ili mada yangu iletwe JF.

By the way nimeshangazwa na ukimya wa EL kuhusiana na tukio hili.
Kuna namna ya kutoa habari na kuongea kwenye matukio kama haya na sio kila mmoja kuropoka! Unapoona pilau tamu mezani kwenye sherehe kuna waliovuja jasho ambao hawatajwi
Kitakuwa kituko cha karne na naweza kusema kitakachoingia kwenye Guinness book of records kutaka kuinasua mamlaka kubwa na hii death plot kisha kuwasingizia watu kana EL au wazungu (kama mlivyokwisha fanya) au mawakili na wanasheria wenzake walio kwenye tofauti za kutengenezwa

Jr[emoji769]
 
Kuna namna ya kutoa habari na kuongea kwenye matukio kama haya na sio kila mmoja kuropoka! Unapoona pilau tamu mezani kwenye sherehe kuna waliovuja jasho ambao hawatajwi
Kitakuwa kituko cha karne na naweza kusema kitakachoingia kwenye Guinness book of records kutaka kuinasua mamlaka kubwa na hii death plot kisha kuwasingizia watu kana EL au wazungu (kama mlivyokwisha fanya) au mawakili na wanasheria wenzake walio kwenye tofauti za kutengenezwa

Jr[emoji769]
Ubaya ni kumpoteza muhusika kwa kuhisia vibaya
 
Nilileta mada yenye msingi huu ikatiwa kapuni ....I wish ningekuwa ni maarufu kule twitter ili mada yangu iletwe JF.

By the way nimeshangazwa na ukimya wa EL kuhusiana na tukio hili.
Sidhani kama inaweza kufikia hata robo ya kiwango cha huu uchambuzi!
 
Katika mazingira ambayo rais wa nchi ameonyesha chuki za wazi na kutoa kauli za kutisha hadharani linapotokea tukio kama la Lisu serikali inabeba <90% ya uhusika
Namshangaa tena sana mtu anyedai kwamba serikali si mtuhumiwa kwa kigezo kuwa Ripoti, ambayo ina faida zote kwao, wasingeweza kuichanganya na tukio hili la Lissu!!!
Ni rahisi tu, ikiwa matukio yafanyika pamoja kwa kutumia wa pande mbili kinzani, ni rahisi upande mmoja kuonekana hauhusiki so far events occurred simultaneously!!! Japo upande mmoja unaweza ukawa ulijigawa kufanikisha mishe!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi mlio wengi hamuwezi kuelewa kilichotokea na kinachoendelea kutokea......ila wenye nchi wanajua kila kitu! Ila Mimi nawahakikishia kwa 100% kuwa tukio la lissu lina uhusiano mkubwa sana na 2020 iwe ndani ya chama chake au nje ya chama chake..Mwenye kuelewa ataelewa na ambae hataelewa pole yake, Mwanga wa screen unaniumiza macho hivyo sitopendelea kuandika sana hapa!
 
Nimesema humu sana,si rahisi serikali ifanye shambulio la kuvuta attention namna hii 'shambulio la kelele 'na wakati Lissu ameshakuwa mikononi mwa polisi mara kibao si wangeweza hata kumpa sumu ya kummaliza taratibu kama walitaka kumuua.
mkuu je kma hizo mbinu zimeshindakana huoni all out attack ndio ilikuwa option iliobaki???

mleta hoja keshasema serkali imejenga hayo mazingira kwa mfano lisu aliwahi kuongelea hilo gari kuwa linamfuatilia je hatua gani ilixhukuliwa?? nape,bashe na zito pia walidai kitu hicho hicho je kma serkali haikuchukua hatua kwanni tusiamini hivo kuwa inahusika??
 
Wananchi mlio wengi hamuwezi kuelewa kilichotokea na kinachoendelea kutokea......ila wenye nchi wanajua kila kitu! Ila Mimi nawahakikishia kwa 100% kuwa tukio la lissu lina uhusiano mkubwa sana na 2020 iwe ndani ya chama chake au nje ya chama chake..Mwenye kuelewa ataelewa na ambae hataelewa pole yake, Mwanga wa screen unaniumiza macho hivyo sitopendelea kuandika sana hapa!
hakuna kitu kma hicho lowasa hagombei 2020 whether lisu akiwa hai au amekufa afterall lisu na mnyika wote ni watiifu kwa mbowe hivyo anayeweza kumzuia lowasa ni mbowe kuliko lisu ama mtu mwingine yeyote ndani ya chadema!!

suspect anayebaki ni yule wa magogoni ingawa naye haihitaji kumuua lisu ili ashinde maana kwa namna yoyote atashinda hta kwa goli la mkono maana kma 2015 CCM ilikuwa ICU ila bado waliiba sembuse sahivi???

hapa hakuna cha 2020 ila ni kujaribu tu kupunguza wakosoaji ili aonekane yupo perfect
 
Siku ya kwanza niliposikia Lisu kashambuliwa sikuwa na shaka na uhai wake,
nadharia ya 1, na ya 2 zilikuja moja kwa moja, Hongera kwa nadharia ya 3 ina mantiki sana
 
Dhana ya kwanza ina mashiko sana, udhaifu uko kwenye utekelezaji tu ikumbukwe huyu bwana ana ugonjwa wa akili hivyo kwake si rahisi kupanga na kutekeleza kwa uweledi na ikumbukwe pia tabia zake za kukurupuka pia, na msisahau ana haiba ya ukatili hajali public itamchukuliaje, kwa hiyo haitoshi dhana hii kuipinga kwa hicho ulichosema ni publicity ya tukio pekee.
 
Toka jana nimesoma maoni ya wengi ...Chahali ndiye aliyechambua hili tukio akiwa na nafsi huru ....[HASHTAG]#prayingforLissu[/HASHTAG]
nonspurious presentation
 
Back
Top Bottom