Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Umesema ukweli nilipata shida nchi flani nikaenda ubalozi wa hiyo nchi kuomba msaaada lakini nilichojibiwa acha tu, mpaka sasa sioni umuhimu wa ubalozi wa Wanyonge sehemu yoyote
 
Sasa watu kama hao wakikutana na mtu kama mimi niliyejiapiza kamwe sitafanya kazi serikali ya Tanzania, naweza kuelewa kwa nini inakuwa shida kuelewana.


Nafikiri moja ya sababu ni kukosekana Kwa 'big private corporations 'zenye maslahi makubwa Sana Kwa waajiriwa kuliko serikalini....

Unaona mtu anaacha kazi Vodacom anaenda Tanesco...


Mtu anaacha kazi NMB anaenda ajiriwa manispaa...

Mambo ya ajabu sana ..

Huko Kwa wenzetu mtu aache kazi Microsoft au Google au JP Morgan aende ajiriwa Manispaa lazima itakuwa sababu ingine na sio masilahi..labda ana ndoto za kutumikia watu..

Huku kwetu hizo Corporations zina vichefuchefu sana..
Huoni kijana ana ndoto ya kuajiriwa Mohamed enterprise au Azam ...achilia mbali kujiajiri...wote wanawaza kuajiriwa na serikali
 
Serikalini kuzuri, hakuna accountability wala responsibility wala scorecard wala goals wala sijui assessments.
Mtu anajua akiwa mtu wa Yes boss, ndiyo boss wangu ataishi kwa furaha.

Mtu anaishi BORA liende asubirie mwisho wa mwezi na kustaafu.

Mwendazake alijaribu kubadili lakini akagubikwa na siasa na kuleweshwa na hotuba za TUNAISHUKURU SERIKALI YA MAGUFULI as if he owned everything.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Unapopanga hizo bajeti hujui kwamba kuna matukio kama hayo hutokea?

Dhima kuu ya serikali ni kusaidia jamii,it may sound higher opportunity cost in terms of money but when you weigh the returns in terms of prerving the reputation of the country inakuwa bora ku help hao raia wako maana uko kwa ofisi kwa ajili yao.
 
Ya sad ....hawawezi hata kuandika wala kuwaza kitu chochote...

Mtu akiomba mtaji muombe business plan iliyoandikwa uisome.

Wa chochote Mungu alichonijalia mimi kwanza siamini kuwepo kwa Mungu hivyo Mungu hajanijalia kitu.
 
Wengi hamjamuelewa,tujadili hoja yake sio kumshambulia yeye binafsi,ndugu yake alishushwa kwa kuwa alikua anaumwa.
Asingekua mgonjwa asingeshushwa Ethiopia,tuanzie hapo,
Aliposhushwa ndo umauti ukamfika.
Kwa maana hiyo shirika la ndege,ilibidi warudishe chenji ,kibongo bongo,wakate nauli Hadi Ethiopia tu,
Hapo tuendelee Sasa.
 
Tumemwelewa sana. Asingekuwa mgonjwa wala ndege isingetua Addis. Yeye alichokitaka ni ubalozi ubebe gharama za hospitali na kumrudisha marehemu nyumbani. Ana imani kuwa ubalozi ulikataa kumsaidia kwa sababu tu wao ni wazanzibari ( ndio maana kasema pangekuwa na ubalozi wao wangesaidiwa). Hakuna mahali amezungumzia shirika la ndege. Ugomvi wake ni ubalozi na machogo waliomnyima anachoona kuwa ni haki yake

Amandla...
 
Ndugu tumemuelewa ana aamini Balozi umembagua angekuwa m-bara angelipiwa, siyo kweli, tumefiwa wabara na ndugu walio ughaibuni na tumewachangia, tumekopa maiti kuwarejesha kuzikwa huku kwao.

Balozi hazisafirishi labda awe mtumishi wa umma.
Tusilaumu tu serikali, tuulize je wengine inakuwaje?? Tena wa-bara wanaokufa ughaibuni ni wengi, kuwazika huko ni gharama, kasafirisha maiti vile vile pia gharama. Tunajichanga, ndiyo ilivyo, SERIKALI HAINA UWEZO mie ni mhanga wa hilo na natokea bara.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ndugu yangu tupoe sana na tumshukuru Allah S.W.T angalau kwa hao fly dubai kwa kutusogezea ndugu yetu maiti yetu na Battawi mwenzetu kwa hapo Ethiopia, japo imechukua muda kumzika ndugu yetu lakini hatimae tumeweza kumzika ardhi ya nyumbani, muhimu sasa tumtakie dua Allah amfanyie wepesi safari yake, Allah amjalie makazi mema na amjalie malipo yake yawe ni pepo na sisi tumuombe Allah atupe subira na msiba huu na husnul khatima njema.

Kuhusu hila za ubalozini ni kwamba nchi yetu huko bado haijawa nchi yenye kutenda haki, ingawa haya malalamiko kwa hapa jf hayatasaidia sana kama ni kwa ajili ya kuona hatujatendewa haki na kutoa madai nashauri tumuandikie rais moja kwa moja kuhusu hili naamini mama yetu Samia atajali sana.

Tupoeni sana nimeona clip ya huyu dada akiwa kwenye ndege akipunga mkono ya kuaga kwa heri kumbe ndio anaaga kwa kundoka hapa Ulimwenguni. Allah amsamehe madhambi yake na sisi sote. Amin.
 
Upo sahihi eti Mtanzania anapoteza passport kupata travelling document ili arudi nyumbani anaambiwa alipie vikaratasi tuu hawa watu kama Kiranga ndio watoa maamuzi wetu na wapo wengi mno huko...
 

Hivyo ndivyo tunavyoaminishwa. Kuna wakati nilikutana na dada mmoja pale Dubai Airport.. Yeye ni mhasibu wa ofisi fulani ya ubalozi wa TZ nchi moja ya Ulaya ( Naihifadhi) . Alikuwepo hapo, pamoja na kijana fulani akisoma huko ulaya , na wamekuja hapo kwa shopping . Ndivyo alivyoniambia huyo dada.

Hivyo ndivyo hizo pesa za ubalozi zinavyoliwa
 
Naomba kueleweshwa..Kinachopelekea gharama za kusafirisha maiti kuwa kubwa hivyo ni nn??..Naomba mchanganuo kama unafahamu..
 


Mwaka 1996 au 1997 Kuna kijana alifariki Ulaya kwa Ukimwi . Baba yake alikuwa ni mmoja wa wafanyakazi wa Ikulu. Maiti ilirejeshwa bongo kwa msaada wa Ubalozi. Kila kitu ubalozi uligharamia.
 
Hivi kwanini maiti inasafirishwa kwa gharama kubwa sana kuzidi mtu hai?

Msaada kwa anayejua anijuze
 
Mwaka 1996 au 1997 Kuna kijana alifariki Ulaya kwa Ukimwi . Baba yake alikuwa ni mmoja wa wafanyakazi wa Ikulu. Maiti ilirejeshwa bongo kwa msaada wa Ubalozi. Kila kitu ubalozi uligharamia.
HILI NDILO KHASA NILILOTAKA LIWEKWE HADHARANI KWA UMMA HUU
Kwa hiyo balozi zetu zinatowa msaada kwa Watumishi wa Serikali tuu?
Sisi makabwela na wajasiliamali hatuna haki?

HII NDIYO 'TZ' TUITAKAYO? WATANZANIA AMKENI!

Mimi naamini kwa mwaka watanzania wnaokufa nje ya Nchi kwa dharura hawafiki 100.

Pia naamini ,wenye shida za kibalozi kama kuharibikiwa au kuibiwa nakupoteza documents za na pesa pia hawafiki 100.

kwa Serikali kuweka fungu kwenye balozi zetu rasmi kwa dharura za RAIA zake halihusianina umasikini wa Taifa letu ,bali ama fungu lipo linaliwa au Serikali inapuuza RAIA WAKE.

Nimeona Ubalozi wa TZ nchini Malaysia umeonesha katika Web site yake kuna kifungu cha dhima ya balozi ikiwa moja wapo ni kuwasaidia watanzania wanapopatwa na dharura nje ya nchi.

Je hii ni kwa Ubalozi ule tuu?
Fuatilia hapa chini
 
Ndugu yangu pole sana kwa msiba uliokufikeni, nilisoma taarifa ya kifo cha dada yenu katika groups za whatsapp na nilisikitishwa sana sana.

Ndugu yangu kuhusu suali la balozi za Tanzania nchi yeyote ile, usiombe ufikwe na lolote lile ukafikiri utapata msaada au muongozo wa kutatua tatizo linalokukabili. Balozi zetu ziko tafauti kabisa na balozi zote duniani inapohusiana na masuali ya wananchi wao.

Nianze na mabalozi wenyewe, hawa wanajiona na miungu watu na fedha ziliopo ubalozini ni za kwao tu na kwa manufaa yao. Ingelikuwa aliefariki ana connection na serikali basi maiti na wale walioshuka nae ethiopia wote wangelipiwa tiketi za kurudi nyumbani na kwa haraka mno.

Tuje kwa maofisa wa ubalozini, hawa nao ndio hata la kusema hakuna, ukienda ubalozi wowote ule duniani, utaona behaviour zao ni sawa kabisa, yaani wanahisi kuwa sie wengine hatustahili kuwepo nje ya nchi ila wao tu. Na unapofikwa na tatizo huwa hawataki kujua lolote yaani atitude yao ni kwani alokwambia uje huku nani?

Hivi ndivyo ilivyo katika balozi zetu, wakati watu wote duniani wanapofikwa na matatizo nje ya nchi zao hukikmbilia kwenye balozi zao kwa muongozo na misaada balozi zetu wao wanatabia ya kujiona na kudharau wananchi wenzao unless uwe unatoka katika familia zinazojulikana.
 
Mkuu ikiwq nchi haina utamaduni wa kuwapenda raia wake wakiwa hai unataraji nini baada ya kuaga kwao dunia? Tazama hata kwenye fursa za ajira na masomo nje ya nchi hali ikoje...
 
Inna lillah wa inna ilayhi rajiun. Allah amghufirie marehemu na akupeni subra.
 
Sasa mnazidisha upuuzi.
Hao wanaofanya kazi ubalozini wanafanya kwa kujitolea au nao wanalipwa mshahara? Kama wanalipwa mishahara, unaona shida gani wao kwenda kufanya shopping Dubai? Wivu wa kijinga kabisa.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…