Hapa Tanzania matibabu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 6 ni bure katika hospitali za serikali. Vivyo hivyo kwa matibabu ya wazee wa kuanzia umri wa miaka 60. Lakini sio wazazi wote wanaowapeleka watoto wao kupata matibabu ya bure hospitali za umma, huwapeleka hospitali za binafsi na kulipa gharama za matibabu kwa sababu wazijuazo wao, vivyo hivyo kwa matibabu ya wazee, sio wote hutumia hospitali za serikali.
Alichomaanisha
Isanga family ni kuwa kuwepo na bajeti ya mambo kama haya kwa balozi zetu, uwepo wake haumaanishi kuwa wote wataokufa wataitumia. Ni kama ulivyosema wewe, wengine wataamua kuzikwa hukohuko na wengine watajisafirisha wenyewe nk ipo hivyo kiuhalisia, watu wote hatufanani maamuzi. Sasa bajeti iwepo halafu kutosha au kutotosha itakuwa jambo lingine baadae. Zamani kabla ya uwepo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Serikali ilikuwa inatoa fedha kusafirisha wagonjwa wa moyo India, ni mambo yanayowezekana kama nchi tukiamua kuyafanya.