Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Ok
 
Haya ushauri wa bure huo...watu wasikae kulialia tu kama watoto yatima
 
Nadhan mleta uzi hujielewi..suala la balozi ni suala muungano..na mule katika ubalozi wapp wazanzibari pia..kwann hawakufanya kama unavyotaka..halafu unasingizia ungekua ubalozi wa mzanzibari..wakati wazanzibari wamo kwenye balozi zetu pia.umevurugwa.. ungekuja kusaidia kukusanya Kodi ili huduma za kijamii zipanuliwe kama hizo ningekuona wa maana sana..lakini maadam hujitambui..basi tena
Bangosha..
 
Nadhan mleta uzi hujielewi..suala la balozi ni suala muungano..na mule katika ubalozi wapp wazanzibari pia..kwann hawakufanya kama unavyotaka..halafu unasingizia ungekua ubalozi wa mzanzibari..wakati wazanzibari wamo kwenye balozi zetu pia.umevurugwa.. ungekuja kusaidia kukusanya Kodi ili huduma za kijamii zipanuliwe kama hizo ningekuona wa maana sana..lakini maadam hujitambui..basi tena
Bangosha..
 
Kumbe wengi humu hatujui haki zetu za kiraia.
Ndo. maana Raisi Kenyata(The Senior) aliwahi kumwambia Mwlm Nyerere ''Wewe unatawala maiti,'' Mimi natawala watu walio hai''
Usiyejua ni wewe.

Haki zako za uraia hazijumuishi kusafirishiwa maiti ya ndugu yako popote duniani. Haikupi haki kuwasemea ovyo na kuwasingizia watumishi wa umma ambao wanatekeleza majukumu yao kama taratibu zinavyowataka wafanye. Haki zako za uraia hazisemi kuwa upendelewe kwa sababu unatoka Zanzibar au Bara.

Siku nyingine ukitaka huduma katika taasisi ya umma fanya kwa staha na taadhima, kumbuka wale pia ni binadamu. Ubabe haukufikishi mbali hasa unapotafuta upendeleo na sio haki.

Amandla...
 

I misquoted you.
 
Pole sana wafiwa
 
Angekuwa ndugu wa kiongozi angeshughulikiwa fasta kwa kuwa ni kajambanani wamempotezea mbaya sana hii
 
Kiranga usiongee sana hao wahuni wananunua gari moja million mia nne kwa nini wasiweze kusaidia watu wengine pia hiyo kila kukicha ujambazi wa kutosha tunasikia kupitia CAG na pia kwa Nchi wanazojali raia wao hawagawawi fungu kila ubarozi zinakuwepo baadhi tuu hayo mambo wanafanya Botswana, Namibia na SA
 
Asikwambie mtu wazanzibar wana hutu sana ,ukiona mzanzibar ana roho mbaya basi huyo mzanzibar wa magomeni au ilala.

Wabara wana umimi sana ,sasa serikali inashindwa vipi kugharamikia tukio kama hilo? JMT hawana funds za dharura?

Kwanini hujauliza kwanini dada asingekata bima ya dharula kabla ya safari.
 
Mkuu unashangaza sana umelalamika kisha umeonyesha jinsi ubalozi wa Tanzania usivyowajibika kwa wote sio tu wazenji hata wa bara mfano wako hapo kwa wanafunzi. Sasa si mngeenda ofisi husika huko zenji mlalamike labda wangewasaidia badala ya kusema mnaonewa.
 
Tunaweza kuwawajibisha viongozi watumie fedha za umma kwa umakini zaidi ili kuimarisha uchumi na wakati huo huo wananchi wakaacha tabia ya kupenda kusaidiwa na serikali kila kitu.

These two things are not mutually exclusive.

Tujenge utamaduni wa kujitegemea wenyewe, tuache kutegemea serikali kila kitu.

Hilo ni jambo la aibu.

Nitamuunga mkono mtu atakayeishutumu serikali kwa kufanya uchumi udorore mpaka watu wanashindwa kurudisha miili ya ndugu zao.

Hapo ilitakiwa kikao cha familia cha watu wachache tu kikae, kichange rambirambi, kifanye kazi ya kurudisha mwili. Ubalozi sanasana ungesaidia coordinatio na kufuatilia mambo huko nje tu.

Lakini kuubebesha ubalozi gharama ni ubinafsi wa hali ya juu, kuna watu wengi wanakufa nje, balozi zetu hazina bajeti za kurudisha hizi maiti.
 
Mimi nisamehewe bure.

Ila sionagi umuhimu wa kusafirisha maiti sehemu moja kwenda nyingine, haina mantiki (kwangu mimi) ni kuongeza gharama kwa jambo lisilo na tija.

Unakuta mtu wakati anaumwa huoni michango au juhudi za kuchangia pesa nyingi huyu ili mtu apate matibabu bora apone, ila akifa sasa mapesa mengi huchangwa sijui kusafirisha sijui kuweka mashughuli, baada ya mazishi familia inaendelea na msoto.

Ukifia england zikwa hukohuko
Ukifia masasi kwenu upareni zikwa hukohuko

Hata ukizikwa kwenu hamna faida yoyote itapatikana kwa kuzikwa kwako nyumbani kwako.
 
General wa jeshi ni Mtumishi wa Umma Serikali inapaswa kugharamia mazishi yake, Mke wake na Watoto wa 4.
Mwanzoni walisema hakutoa taarifa ubalozini hata angekua nani baadae wakaja kuomba msamaha na iliwaletea sana shida na hata uhusiano na Wananchi ulipotea kiasi fulani...
 

Mkuu King Kong III kwanini unadhani serikali ina wajibu wa kusafirisha watu wa nje na kuacha raia wa ndani wapambane na hali zao?

Unadhani mtu wa Kigoma akifia Iringa serikali inabidi imsafirishe? Basically it's the same thing. Vinginevyo unaunda mazingira ya kufanya raia waliopo nje ya nchi waonekane ni tabaka la juu kuliko walio ndani.

Aidha kuna life insurance zinacover haya mambo, kuna bima za dharulu wakati mtu unakata ticket unaweza ongeza tena kwa gharama ndogo tu kwanini tusimlaumu marehemu kwa kutokata hizo bima. As cold as it sounds, ni kwaajili ya kueleweshana.
 
Matumizi ya fedha serikalini yanaendana na mafungu ( votes) ambayo ndio yanaongoza matumizi yake. Kama serikali haina Vote inayohusu kusafirisha marehemu nyumbani, Accounting Officer hawezi kuamuru fedha zilizopo kwenye fungu la kulipia mafuta zitumike kumsafirisha marehemu. Hiyo itakuwa ni kujitafutia audit querry na maswali kwa nini huyu na sio yule. Njia sahihi ni kuwasukumiza wabunge wetu wailazimishe serikali waone umuhimu wa hili ili fedha ziwe zinatengwa kwa ajili yake kwenye budget ya serikali na liundwe fungu mahsusi kwa ajili yake.

Ukweli ni kuwa watanzania ni wabishi. Kuna mifuko ya jamii inatoa huduma hii kwa wale wanaochangia lakini huwa hatuoni umuhimu mpaka yanapo tukuta. Njia nyingine ni tukubali kuzikwa pale ambapo umauti unapotukuta.

Amandla...
 
Sijazungumzia watu wote warudishwe kama unavyozungumza wewe Nchi inayojali raia wao naona kabisa hata wanapozungumzia maendeleo yanaonekana kama hujali raia wako utaendelea kuwa hapo hapo tuu wapo wengine wenye uwezo wanajigharamia wenyewe ni vile tupo katika Nchi ambazo ufisadi umechukua nafasi kubwa sana nakumbuka huko ubalozini kuna dili za kifisadi sana sijui ile kesi ya ukarabati na ununuzi wa ubalozi wa Tanzania huko iliishaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…