Tukio la Rais Kikwete, Dr. Shein kukabidhiwa Rasimu ya pili na tume ya Katiba - Karimjee Hall

Wakuu mwenye hiyo rasimu atuwekee humu tuipitie na kuijadili kwa kina
 
Jk amejitahid kufikisha ujumbe,maana nae watu wake huwa wanaropoka kama wamepakwa -----
 

Huyu JK akitulia huwa kichwa yake inachaji sana..
 
Kwa jinsi nilivyomsikia kikwete hawezi kuruhusu chama chake kuingiza ushabiki kwani ameshasoma kuwa kwa serikali 2 hakuna namna ya kupata theluthi 2 za kuipitisha kwa zanzibar.aibu itamkuta kama ataruhusu mabilioni ya kodi yatumike na katiba isipatikane.
 


Uhuni watakaofanya magamba ni kuondoa baadhi ya vipengele kwenye rasimu likiwemo hili suala la Serikali Tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ili zibaki Serikali Mbili wanazotaka wao. Usione kila namna ilifanywa ili Bunge la Katiba liwe na magamba wengi. Hiyo ndio karata yao ya mwisho na wataitumia vilivyo. Naona kama jinamizi la Serikali Mbili litaendlea kuwepo.

Kwa hiyo la msingi ni sisi wananchi kujiandaa kisaikolojia kukubaliana na pinduapindua ya magamba.
 

Kodi yako sh ngapi kwa mwaka weyee...acha kutuzingua hapa eti mlipa kodi wewe...!!
 

Hata na mimi siliamini hilo Bunge la katiba maana CCM walikuwa wanalipigania kwa mbinde sana na kuhakikisha haliwashirikishi Wanzanzibar kwa wingi. Imagine kwenye rasimu ZNZ wametoa wajumbe sawa na bara lanini kwenye bunge wanakuwa wachache. Nashangaa kwa nini ZNZ hawakulikomalia hili!! Au wana mtego wao wanasubria Khanga ijiingize mwenyewe!!
 
Kodi yako sh ngapi kwa mwaka weyee...acha kutuzingua hapa eti mlipa kodi wewe...!!

Mie nalipa kodi milioni 3 kila mwezi jumla nawapa serikali milioni 36 kwa mwaka wewe unalipa bei gani kwa mwezi nina uchungu na kodi yangu.
 
Mkuu, usishangilie sana. Hii ni sawa na kupewa mahindi mabichi utafune wakati hauna meno. Serikali tatu, uraia mmoja, rais mmoja, jeshi moja, polisi moja na usalama wa taifa mmoja. Umeona changamoto iliyo mbeleni?

= taifa moja

inatosha!
 
Hivi kutakuwa na wimbo wa Taifa la Tanganyika....Inabidi tuanze mchakoto wa kutunga wimbo wa taifa la Tanganyika. .
Upo labda ni kuukarabati kidogo tu uendane na wakati. Una maneno ya "Tanganyika Tanganyika nakupenda kwa moyo wote nchi yangu Tanganyika nina lako ni tamu sana. Nilalapo nakuwaza wewe niamkapo ni heri mama weee....... Tanganyika Tanganyika ..........."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…