Baada ya kumsikia Mheshiwa Rais Kikwete akirusha dongo kwa Tundu, ikanibidi nipige simu za hapa na pale kuutafuta ukweli.
Licha ya mimi binafsi kushuhudia kupitia TV siku moja bungeni Tundu baada ya kuhororoja sana akinyamazishwa kwa maneno mawili matatu na Mzee wa Vijisenti, na Tundu kuuona ukweli ikabidi atulizane huku akiona aibu. Simu nilizopiga nazo zimezaa mengine.
Kuna mtu aliyekuwepo kwenye kikao cha Ikulu cha Wanasiasa waliokwenda kumuona Rais, na Tundu katika kuongea yake, akimuiga mchungaji gani sjui, akaparanganya mambo na kutoa vifungu ambavyo havihusiki. Akawachwa abwabwaje walipoona anaendelea kuongea utumbo akaambiwa samahani kidogo, naam, magwiji wa sheria wakaanza kamuweka sawa na baada ya kujionea ukweli ulivyo, ikabidi aombe msamaha na baada ya hapo hakuongea tena mpaka kikao kinakwisha.
Ndio maana dongo alilorushiwa na Kikwete ilibidi ajichekesha tu, kuna cha kuchekelea pale? uumbuliwe mbele ya Watanzania wote na wasio Watanzania waliokuwa wanashuhudua live halafu ujikeshe na usipinge lolote mpaka leo hii? halafu ni mpinzani?
Madongo aliyorushiwa hayapingiki na mpaka kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, hamtamsikia Tundu akilalamika wala akikumbushia hilo kwani kikaoni Ikulu ilikuwa ni aibu sana kwake na kwa chama chake yaliyomkuta. Sijui kama ana hamu tena ya kurudi Ikulu hivi karibuni.
Waandishi wa habari nendeni mkamuulize Tundu alilikoroga vipi Ikulu.
Tundu, upoo? Njoo ukatae.