Tukio limejirudia tena katika mazingira yaleyale, nikiwa na watu walewale huku tukizungumza maneno yaleyale

Tukio limejirudia tena katika mazingira yaleyale, nikiwa na watu walewale huku tukizungumza maneno yaleyale

Matukio yanayofanana na hili ni Kuota ama kujirudia kwa ndoto ile ile kwa nyakati kama ile ile !!
 
Msaada wakuu, hii hali imeanza kuwa serious sana. Kwa sasa inanikuta kila mwezi tofauti na awali ilipokuwa inanitokea mara moja kwa mwaka

Inaanza uko maeneo fulani ukiwa na mtu fulani, wakati unamalizia mazungumzo, ndipo unakumbuka kuwa hayo maneno umewahi yatamka kabla. Hata eneo ulilopo ndilo lile lile, pia mtu unayezungumza naye ni yule yule au mtu anayeendana hobies na uliyozungumza naye mwanzoni

Au unapita mahali unakutana na tukio amabalo umewahi kukutana nalo kabla. Hata majibizano ya watu yanayoendelea ni yaleyale ya kipindi hicho. Unapojaribu kufungua mdomo kuzungumza, unajikuta unazungumza yale yale uliyowahi kuzungumza. Unabaki unashangaa tu

Hii hali husababishwa na nini wakuu?
Je, tukio la kwanza kabla, lilikuwa ni ndoto? Au liliwahi tokea kweli? Au ni mawenge tu? Au naumwa malaria? Maake sielewi hata limekuja vipi, yaani from nowhere

Nikijaribu kumuuliza huyo ninayezungumza naye kwamba haoni kama tunafanya marudio?, anaishia kusema nipunguze wenge au kucheka tu

Naombeni ufafanuzi wakuu
N.B: Situmii mihadarati
Dejavu hyo ,mimi ni kawaida nshazoea
 
Ujitunze sasa mmebaki wachache mm nilikua hivyo dhambi zimeniondolea huo upako...
 
ULEVI. Ni sawa na ukiota unakojoa halafu uwe unakojoa kitandani kila siku. Ulevi ni chanzo kikuu. Punguza pombe.
Mi sio mlevi na sijawahi husa pombe maishani , lakini hali hii pia hunitokea
Huyo jama aliyeleza dejavu kidogo nimemuelewa .
 
Sasa mkuu wakati Yohana alipouliwa ulikufa mwili tu na sio roho right?

That’s means roho ilirudi kwa Elia?
Umesoma hiyo mistari ? Pia kitabu cha Samuel kimezungumzia Samwel alipo amshwa na sauli wakati alishakufa ,kuna mambo mengi yapo ki code kwenye biblia mpaka uamke ndio utapa ufahamu nayo.
 
Back
Top Bottom