Wakuu Bwana Yesu asifiwe!
Ebana kuna issue inanitatiza halafu nimeshindwa kuizungumza kwa mhusika ambae ni wife nikaona nitafute kwanza mawazo humu.
Issue nzima iko hivi, ninavyojua kwa mila na ustaarabu wa kiafrika endapo itatokea familia ikachinja kuku basi baba ndiye mwenye kustahili kula mapaja ya kuku.
Sasa hapa kwangu sielewi wife ananichukuliaje,yani kila kuku akichinjwa basi mimi father house ntalichwa vipapatio na vitoto vyangu viwili vya kiume vyenyewe ndio vinawekewa mapaja.hii kitu wakuu inanishangaza kidogo as iko kinyume na mila na desturi za kiafrica.
Wife yeye kwao walikua ni mambo safi hivyo nadhani hawakua watu wa kujali vitu hivyo vidogo vidogo ndio maana anaona ni sawa tu mimi Baba kula vipapatio.
Wakuu,nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe kuwa siridhishwi na kulishwa vipapatio?