Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa kuwa mambo ya kuchochea chuki za ukabila, ama udini, yakianza na tukayapa nafasi, hayana simile.
Si hoja yangu leo kumtetea Rais Samia kwa mambo anayolaumiwa, Hoja yangu ni propaganda za ubaguzi wa kidini, kikabila na kikaburu zinazoambatanishwa na ukosowaji wake.
Tafakari, kama swala ni kumkosoa Rais, mathalani kwa mambo fulani fulani ambayo kundi fulani haliridhishwi nayo, kuna sababu gani ya kumbadika rebo kuwa huyu mzanzibar, huyu wa kizimkazi au huyu muislam?
Wakati mwingine unaweza kuwa na hoja nzuri, lakini ukishaiwasilisha katika kifungashio cha kibaguzi, itakabiliwa badala ya kujibiwa.
Nchi yetu ni Tanzania, sisi wote ni watanzania na sote tuna haki sawa, angalau katika misahafu yetu ya sheria tuliyo nayo. Kwanini tusiishi kwa upendo na kuheshimiana?
Mwalimu aliwahi kutukumbusha kuwa tutakapomaliza kuchoma maduka ya wapemba kariakoo, wazaramu watagundua hata waha, wamanyema, wachaga na wakinga maduka yao hayatakiwi kuwepo kariakoo maana nao pale sio kwao. Hapo ndipo tutakapoelewa kuwa mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.
Leo hii kinachotufanya tujione sisi ni watanganyika na sio watanzania ni kwasababu tunataka kuwabagua Wazanzibari. Champions wa agenda hii wanatumia madhaifu ya Rais wetu mzanzibari, kueneza chuki kana kwamba uzanzibari ni janga kubwa mno kwa watu wa bara, kwani ukitaka kuua mbwa sharti umpe jina baya.
Nchi yetu sio "finished project", bali ni "work on progress". Katika safari yetu ya matumaini kuelekea nchi ya ahadi, ni wazi tutakutana na kero, changamoto, maudhi, vikwazo, n.k. Vitu hivi havipaswi kututoa kwenye reli ya kujenga nchi yetu katika misingi ya umoja, amani na utulivu.