DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wagombea wa nafasi ya Urais na Makamu wa Rais kupitia Chama cha Demokrasia Makini, leo wamewasili katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu ambapo ametaja vipaomEKARI tano ikiwa ni pamoja na kuwapatia vijana mashamba ya umwagiliaji yenye ukubwa wa ekari tano.
Baada ya kukabidhiwa fomu hizo na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacob's Mwambegele,Kibonde alieleza kuwa chama chake kimeweka vipaumbele katika sekta tatu kuu ambazo ni elimu, afya na kilimo.
Amesema serikali yao itahakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu bora popote duniani, kujenga vituo vya afya kila kata na kuanzisha Bima ya Afya ya Taifa itakayojulikana kama Makini Care.
Aidha, kwa upande wa kilimo, Kibonde ameahidi kila kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 21 kupatiwa ekari tano za mashamba, kuanzishwa mashamba ya umwagiliaji na kuongeza uzalishaji wa chakula kwa lengo la kuuza nje na kuondoa umasikini
Mgombea huyo pia ameipongeza Tume kwa maandalizi na ushirikiano walioupata tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.