Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ukituhumiwa kuua mtu, (au kumnyang'anya mtu haki yake ya kuishi) tunategemea utafikishwa mahakamani na kujibu mashataka ya kosa la kuua. Inawezekana kabisa, hukumu ya kesi yako ikawa ni kuachiwa huru kwa kuwa katika ushahidi uliotolewa ulionyesha labda ulisingiziwa, au uliua kwa kujitetea maisha yako, au uliua katika mazingira tunayoita "upotevu wa akili wa ghafla" au temporary insanity. Hivyo unaachiwa huru kwa kuwa mahakama haijakutia hatiani.
Ukituhumiwa kuchana Biblia au Quran - pia tutategemea ufikishwe mahakamani na kujibu mashitaka ya kuchana Biblia au Quran. Sasa hapa suala la kujiuliza ni kwamba, je inawezekana katika ushahidi kutolewa mahakamani, ikaonekana kuwa hiyo Biblia au Quran hukuchana wewe ila ulisingiziwa, au uliichana katika mazingira tunayoita "upotevu wa akili wa ghafla" au temporary insanity, na ukaachiwa huru kwa kuwa mahakama haijakutia hatiani?
Lakini kwetu sisi kama jamii ya karne ya 21, ni lipi lapaswa kuwa kosa kubwa na jambo zito zaidi - kuua mtu au kuchana Biblia au Quran? Binafsi, naona kwamba kuchana Biblia au Quran ni jambo la kukosa heshima na ustaarabu, lakini hata siku moja siwezi kusema kuua mtu ni jambo la kukosa heshima na ustaarabu.
Kama ni hivyo, kwa nini basi mtu atakaetuhumiwa kukosa heshima na ustaarabu kwa kuchana Biblia au Quran tumchukulie kama ni mbaya zaidi sana kuliko hata yule ambae atakuwa ametuhumiwa kuua (au kumnyang'anya mtu haki yake ya kuishi)?
Je, ni kweli tuna mapenzi sana na Biblia au Quran, vitabu tunavyoona ni vya Mungu, na tunaumizwa sana tukiona vinachanwa kuliko hata kuuawa kwa wanadamu walioumbwa na Mungu? Tuangalie tusije tukaonekana wanafiki mbele za Mungu kwa ajili tu ya umaarufu wa mitaani au kiki za kisiasa!