Tukiweka pembeni ufia Dini kwanini makanisani kuna walinzi na viongozi wa dini wana walinzi lakini sisi waumini tunaambiwa malaika watatulinda?

Niliona clip ya geodav nikajiuliza maswali sana na yule wa EFATHA jina limenitoka kuna msafara fulani alikuwa na walinzi kibao
 
Je, kuna kiongozi wa dini anayekuzuia wewe kama Mkristo kufanya hayo mambo? I.e
  1. Kujenga ukuta kwa ajili ya uzio (fence)
  2. Kuweka walinzi nyumbani kwako
  3. Kuwa na walinzi binafasi wa kutembea nao
  4. Kuweka CCTV cameras nyumbani kwako
  5. Kuweka nyara za umeme kwenye fence n.k?
Hata hivyo, baadhi ya hao unaowaita viongozi wa dini sio viongozi wa dini za kweli, ni viongozi wa dini za uongo (maandiko yanasema hivyo)

Lakini pia, kwa upande mwingine, hata kwa dini za kweli ulinzi wa rasilimali za kanisa ni jukumu la kanisa. Ndio maana utakuta maeneo kama majengo ambayo yanatunza rasilimali yanawekewa walinzi. (Kumbuka kwenye maandiko tunaona hata sanduku la agano liliibwa). Ndio maana hata huko maca umesema kuna walinzi, makanisa yenye uwezo wa kifedha yanaweka walinzi kulinda vifaa vyao n.k
 
KWANZA KABISA NATAKA KUWAKUMBUSHA WAKRISTO WOTE KUWA KANISA SIYO NYUMBA YA IBADA .... WOTE WANAO ENDA KANISANI KWA KISINGIZIO KUWA NI NYUMBA YA IBADA NI WAPUMBAVU ...TOKA ZAMANI KANISA ALIKUWA NYUMBA YA IBADA BALI LILIKUWA NYUMBA ZA KUKUTANIA KUFUNDISHANA INJILI YA KRISTO ...KWA KUWA AZIKUWA NYUMBA ZA IBADA BALI MAJENGO TU YANAYOTUMIKA KUFUNDISHANA INJILI WATU WALIINGIA NA VIATU NA KUKAA VITINI SASA UPUMBAVU ULIKUJA BAADA YA HIZO NYUMBA KUGEUZWA NYUMBA ZA IBADA NDIYO CHIMBUKO LA NYUMBA ZA IBADA ZA KANISA NA MITINDO YAKE YA KUINGIA NA VIATU NA KUKAA VITINI ILIVYO TOKEA.
 
Unataka kila kitu kiandikwe? Mbona haijaandikwa Kama walikua wanaenda chooni lakini wewe unaenda? Kuna vitu inabidi utumie akili tu ya kawaida
Yesu kipindi anakamatwa walinzi wake walikuwa wapi? vipi kuhusu stefano,sila napaulo walinzi wao walikuwa wapi?
 
kiongozi wa dini anapambana na maadui wengi sana, hasa wa kiroho. hata mlokole wa kawaida tu aliyesimama vizuri ana maadui wengi sana. mfano hata mimi binafsi, kuna watu wameenda kwa waganga, wameloga hadi wamemaliza pesa, ila wamedunda. kuna mitaa mingine ukienda, hati nguvu za giza zinashindwa kufanya kazi vizuri. mtumishi wa Mungu Bonke kama unamkumbuka, alikua akija nchini kwako, hadi baadhi ya viwanda vinastop, hasa vile vinavyotumia mauchawi, wachawi wanashindwa kuruka vizuri, hivyo tegemea wachawi ambao uchawi wao wameutolea garama kubwa sana, wanaweza kukujia kimwili wakikushindwa kiroho. kuna mitaa hata hapa bongo unapoishi, jua kile mtaa kuna mkuu wa anga, wameenda kwenye hyerachy hadi juu, wana shughuli zao za kishetani, uwepo wako unawafanya washindwe mambo mengi sana au wapite njia nyingine. wakikushindwa kiroho wanaweza kuja kimwili kwa bunduki au kisu kabisa. ilishatokea maeneo mengi tu watumishi kushambuliwa individually kabisa. vilevile inasaidia kutengeneza distance na watu unajua ukizoeleka saba inapunguza hata heshima. hata Yesu wale thenashara wake 12 pamoja na wanafunzi kibao karibia 70 walikuwa wanamzunguka kumtumikia na kumlinda pia. unakumbuka hata petro alichofanya pale getsemane, kata sikio la mmoja. kina Paulo na wengine mara nyingi sana walivamiwa na kupigwa kwa sababu ya imani yao tu. yaani kuna mtu tu mwengine sio mchawi wala lolote ila tu ni katili asiyependa ulokole, nimeshakutana na watu wanauchukia ulokole na walokole kuliko chochote na wanaweza kufanya lolote dhidi yao. mtu anaongea toka moyoni kabisa kwa chuki ya hali ya juu dhidi ya walokole.

sio wote wanaolindwa ni mambo yasiyopasa, though kuna wengine sio watumishi wa Mungu ni wapiga pesa tu wauza mafuta na maji na manabii wa uongo, wanakuwa hivyo hadi wanachukua utukufu wa Mungu, wanatukuzwa mno. kwenye kundi jua kiongozi ndiye anawindwa kuliko wengine.
 
Kwanza usinilishe maneno kwa kuniambia kuwa kiongozi wa dini kanizuia kufanya hayo yote.La jasha mimi sijasema hivyo Bali nimeuliza unapoweka walinzi maana yake malaika ni dhaifu sana na hawana uwezo wa kulinda ndio maana imetulazimu tulinde binadamu wenyewe.

Umewahi kusoma kuhusu elisha? je kisa cha Danieli kwenye tundu la simba bado hakikufundishi kuwa Mungu hawezi shindwa na kitu chochote.Mbona maandiko yako wazi kabisa Yohana aliambiwa na malaika "mimi ni mjori (mlinzi/mfanyakazi )wako msujudie Mungu"

SOMA======

2Wafalme6:15Mtumishi wa Elisha alipoamka mapema kesho yake na kutoka nje, akaona jeshi pamoja na farasi na magari ya kukokotwa limeuzingira mji. Akarudi ndani akasema, “Ole wetu, ee, Bwana wangu! Sasa tutafanya nini?”
16Elisha akamjibu, “Usiogope kwa sababu walio pamoja nasi ni wengi kuliko walio pamoja nao.” 17Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
Kisa hiki cha Elisha ni wazi kinaonyesha namna gani watumishi wa MUNGU wanavyolindwa na sivingine.
SOMA PIA======
Zaburi 127:1BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
 
hili suala hua najiuliza sana, unakuta fence kubwa unajiuliza ina maana huyo mungu wao hana uwezo wa kulinda?
kuna ulinzi wa kimwili na kiroho. Hivyo uvionavyo ni ulinzi wa kimwili na usivyoona ndio ulinzi wa kiroho.
Sasa malaika wapo huko usipoona ndio wanalinda sio kazi yao kuja kusimamia upande wa kimwili. Yaani waje wakae gatini. Japo mambo yote huanzia huko. Ukitaka kufika upande ule usiouona ukapime kama kuna ulinzi njia rahisi kamloge Mutumishi wa kweli wa Mungu ndio moto wa maraika wanaomlinda utauona. Ila ukidhurika usinilaumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…