Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Tuliosoma vyuo vikuu tuliona. Vijana waliokuwa UVCCM ndo wengi wao walikuja kuajiriwa Serikalini na kuingizwa kwenye vyombo vya dola ikiwemo usalama wa Taifa.
Mimi niliosoma nao waliokuwa mstari wa mbele huko UVCCM wengi saivi ndo Watendaji Wakuu katika taasisi mbalimbali za Serikali na wana vyeo vikubwa ikiwemo DAS, DED, KM, NKM, CEOs katika mashirika ya Umma.
Kati ya sehemu ambapo nchi hii ilifeli ni kuendelea na mfumo wa chama kimoja katika kuendesha nchi baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi.
Leo hii CCM na Jumuiya zao ikiwemo UVCCM wanajiona kuwa wao ni sehemu ya Serikali na vyombo vya dola. Wanajiona wanaweza fanya chochote kama Serikali na vyombo vya dola wakati kiuhalisia baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi chama chao kilipaswa kuwa chama tu kinachofanya shughuli za kichama tu!
Madhila tuyapota leo tutaweza kuyakomesha pale tu tutakapoweza kukitenganisha Chama cha Mapinduzi na Serikali na hili litawezekana tu kupitia KATIBA MPYA.
Wenye akili watanielewa
Lord Denning!