Tuko tayari kuacha kazi na kujiajiri. Tupatieni fao la kujitoa

Tuko tayari kuacha kazi na kujiajiri. Tupatieni fao la kujitoa

Kumekua na kauli za kubeza watumishi pindi tunapo lalakikia maslahi duni. Wanasiasa wengi na watu binafsi wanekua wakitamka kuwa asiyetaka au anaye ona mshahara haitoshi aache kazi.

Ifahamike kuwa wapo watumishi ambao tuko tayari kuachia nafasi ili na wengine wapate Ajira ili sisi tukajiajiri.

Tatizo ni vile serikali imepokonya Hali ya malipo ya FAO la kujitoa.
Haina haja jambo la kubadili kazi iwe ni kejeli na dhihaka Kwa watumishi. Kazi iwe ni Moja ya haki na uhuru binafsi wa mtumishi. Mtu awe huru kupanga namna ya kutumia muda wake hapa duniania. Mtu apenge ni lini afanye mambo yake kulingana na malengo yake.

Kama Nina wito wa kuzeekea kwenye utumishi niamua mwenyewe. Kama nataka kuwa mkulima baada ya utumishi wa miaka mitano au zaidi niamue.

Sasa tuko tayari kuacha hiyo kazi ili tubadili namna ya kulitumikia taifa Kwa njia mbadala.

Tunaomba pesa zetu huko NSSF ambazo mmezishikilia kama fao la kujitoa.

Huo mshahara wenu tunashukuru Kwa hapa tulipo fika, Sasa tupishe wengine.
Tunaomba hilo fao
Viongozi wetu wengi hawana MAONO na wana uwezo mdogo mno kiakili.

Hawajui wewe ukijiajiri baadae unaweza kuajiri vijana wenzako kama kumi na kiwachangia michango yao NSSF..

Yaani wana UONI HAFIFU mno na akili za KIMASKINI MNOOOO eti mtu akichukua pesa zake atasumbua mtaani baadae akizeeka halafu hana kitu. They're shortsighted wanaangalia upande mmoja tu.
 
We na nani?? Hao wanajiita wapinzani wanakula Asali huko ndio wanitetee mimi...Kila mtu apiganie tumbo lake nw.
Huu ndio usaliti kwa taifa... Ubinafsi utalifanya taifa liendelee kuingizwa na wasiofaa !!
 
Ukijiari tu hii nchi unaanza kupata tabu. Mfano; Utashangaa mkuu wa Wilaya anakuja kuomba hela za vikao, Mbio za mwenge, Diwani nae vivo hivyo, Katibu mwenezi nae hivyo hivyo, hapo TRA hawajaja.. ili mradi tu wakutaabishe.
Hapana. Sio kweli kabisa, labda kama umejiajiri na kuendesha mambo yako kwa janja janja, ukifuata taratibu zote na kulipa kodi kwa wakati, hakuna Raha kama kujiajiri.... Wasi wasi uko kwenye wateja kama wataendelea kukuunga mkono.
Kuna wimbi kubwa la watumishi kuacha kazi na kujiajiri huko Marekani hivi sasa, hata kujiunga na jeshi kumedorora kuliko kawaida. Sababu kubwa, watu wengi wamegundua utumwa unaofanywa na waajiri hasa Serikali.... Yaliyotokea Sri Lanka ni mfano maridhawa. Karibuni private sector!!.
 
Hilo fao la kujitoa mimi naona liliwalenga zaidi Walimu maana ndio waajiriwa wanyonge zaidi wa Serikali.
 
Hapana. Sio kweli kabisa, labda kama umejiajiri na kuendesha mambo yako kwa janja janja, ukifuata taratibu zote na kulipa kodi kwa wakati, hakuna Raha kama kujiajiri.... Wasi wasi uko kwenye wateja kama wataendelea kukuunga mkono.
Kuna wimbi kubwa la watumishi kuacha kazi na kujiajiri huko Marekani hivi sasa, hata kujiunga na jeshi kumedorora kuliko kawaida. Sababu kubwa, watu wengi wamegundua utumwa unaofanywa na waajiri hasa Serikali.... Yaliyotokea Sri Lanka ni mfano maridhawa. Karibuni private sector!!.
Ndugu yangu . Unaongelea Mambo ya Marekani? Basi ndio maana hujui ninaloandika Mimi hapa.

Jishughulishe , kujiajili ni kizuri ila bongo ni shida. Ukiona mtu mweusi amefanikiwa kwenye kujiajili ujue anapambana mno. Wengi ni wahindi, waalab , wasomali na wazungu. Mtanzania anasota sana kwenye nchi yake.
 
CHADEMA ipi hiyo? Ishakukufa mda tu. Wanalamba Asali.

Ukijiunga huko unakosa tenda tena. Ilimradi tu upate tabu.
Muulize chifu Hangaya atakueleza kwa mapana.Hayo maneno ya ..."CHADEMA imekufa"...mpelekee Steven Wassira aya-clarify!
 
Natamani serikali iwape kweli mafao yao hawa mambumbumbu wakaonje mziki wa kujiajiri..
 
Ndugu yangu . Unaongelea Mambo ya Marekani? Basi ndio maana hujui ninaloandika Mimi hapa.

Jishughulishe , kujiajili ni kizuri ila bongo ni shida. Ukiona mtu mweusi amefanikiwa kwenye kujiajili ujue anapambana mno. Wengi ni wahindi, waalab , wasomali na wazungu. Mtanzania anasota sana kwenye nchi yake.
Niko kwenye ajira binafsi kwa miaka zaidi ya ishirini sasa tena hapa hapa Tanzania.Hao unaowataja kwa ujumla wao ndio wadau wangu katika biashara.
Mtazamo wako hautofautiani sana na waajiriwa wengi ambao hawaamini katika kujiajiri kwa kutiana hofu tu.

Mimi niliachana na Serikali baada ya kufanya miaka mitano, sijawahi kujutia uamuzi wangu huo, hata michango yangu ya uzeeni niliwaachia baada ya kuleta longo longo.....

Siko Marekani mkuu, Niko bongo hii hii na mambo yanaenda, nafuatilia kinachoendelea kwenye uchumi wetu na hata nje ya nchi kwa umakini mkubwa. Ila nikiri hapa kuwa watumishi wasioamini katika kujiajiri huwa ni wasumbufu kwa wale walliojiajiri, pale wanapotembelea ofisi za Serikali...

Ila kama ni mjasiriamali makini unayefuata sheria zote na taratibu, huwa wanalielewa somo tu.
 
Viongozi wetu wengi hawana MAONO na wana uwezo mdogo mno kiakili.

Hawajui wewe ukijiajiri baadae unaweza kuajiri vijana wenzako kama kumi na kiwachangia michango yao NSSF..

Yaani wana UONI HAFIFU mno na akili za KIMASKINI MNOOOO eti mtu akichukua pesa zake atasumbua mtaani baadae akizeeka halafu hana kitu. They're shortsighted wanaangalia upande mmoja tu.
myopic leaders indeed
 
Back
Top Bottom