Tuko tayari kuacha kazi na kujiajiri. Tupatieni fao la kujitoa

...Na wakati Mwingine wanaelewa kabisa ila ROHO MBAYA TU.
 
Upo sahihi Mkuu,
Ila ukitaka kutoka nowadays fursa za kuchukua mkopo hlf unatembea ni msaada mkubwa.
 
At Least You Have Come Up With Something !! Not Like Others Who With Complaints Every Now And Then !!!
 
Mmeshaanza chokochoko, mntaka mifuko ife ?
 
Katika nchi zetu hizi utumishi ni utumwa mkatae mkubali.
Na viongozi wengi kwenye hivi vyama hasa wa wafanyakazi hawapo kwa maslahi ya wafanyakazi ni vibaraka wa wanasiasa ni mabogaz sijawahi ona ...na kwakweli tusipo badilika tutakuwa watumwa mpaka tutakapo ingia kaburini ...
 
Hakuna sababu za kuweka fao la kujitoa bali kupunguza Umri wa kustaafu kuwa miaka 50 au 45 .
 
Wala hiyo sio sababu bali Mwendazake alipora pesa zote kwenye mifuko Ili kuzuia wanaota kuacha Kazi na obligation ya serikali kuwalipa Chao ndio alikuja na huu ujinga Kwa vile mifuko haina pesa..

Baadae iki stabilise watarudisha tena.
 
Uko sahihi, niliwahi kufanya kazi Serikalini kwa miezi 8 tu ila nilijilaumu sana, kwanza unadumaza akili tu.
Hongera kwa kujikomboa ndugu. Watu wengi ndoto zao zimezimika kisa ajira. Na unadumaa kwelikweli. Mimi nilimwandikia mwajiri wangu resignation letter nilipoenda kwa boss wangu ili aipitishe akaanza kutetemeka nikashangaa. Watumishi wengi akili si zao,we wazia mtu mzima uzabwe makofi na mtu mzima mwenzio na utulie kisa ni bosi wakati zipo code of conduct kama umekosea zinazoelezea ufanywe nini.
 
Duniani kote ipo hivyo,ila huku kwetu ni tatizo kubwa sana.
Wenyewe mlimsikia Profesa akikiri kwa kinywa chake baada ya kuteuliwa kuwa waziri kuwa miaka yote aliyokuwa kwenye utumishi alikuwa jalalani. Ni hatari sana. Nakubaliana nawewe hapa kwetu tatizo ni kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…