Tuko tayari kulipa tozo na kodi aina zote lakini Serikali iwe tayari kusema imeshindwa kutumia rasilimali za nchi hii tulizojaaliwa na Mungu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Sasa ni wakati muafaka wa kuachana na misaada kutoka nje, maana nao huko kwao hali ya uchumi imekaza.
Misaada inashusha heshima, mtu anayekusaidia hata akiongea upuuzi lazima ucheke ili umridhishe.
Options ni 2 tu kwasasa.

1. Kutumia rasilimali zetu kama gas, makaa ya mawe, dhahabu, na madini mengine ya vito kujijenga.
Bila kusahau fukwe za bahari na bahari yenyewe, maziwa na mito, ardhi yenye rutuba , milima, hifadhi na wanyama pori wetu.

Rasilimali za nchi hii ni nyingi, haya matrilioni ya kodi tuyatumie kama mtaji wa ku utilize rasilimali zetu.
2. Tuendelee kulipa tozo zilizopo na ziongezwe zingine ili tupate pesa za kuendesha nchi na kuleta ustawi katika jamii.

Ila katika option namba 2 tunaomba Serikali ikiri kuwa imeshindwa kutumia rasilimali tulizojaaliwa na Mungu kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo imependekeza tozo ndizo ziwe mbadala wake.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa rasilimali za ardhini kama rasilimali watu ni empty set.
Unaijua DRC? ...Nigeria?
Hawa bongoflava na simba na yanga na ngono zembe unatarajia maendeleo gani..
Tozo ni kwamba hakuna namna nyingine
 
tunaomba serikali ikiri kuwa imeshindwa kutumia rasilimali tulizojaaliwa na Mungu kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo imependekeza tozo ndizo ziwe mbadala wake.
Msisitizo.

Wakiri

DOMOTOZO analipa tozo gani? anyway nje ya mada.
Wakiri
 
Kama lengo la kuwa na serikali ni kusimamia utumiwaji wa rasilimali zetu kutunufaisha na serikali imeshindwa kwa miaka 50 madarakani badala yake imetugeukia sisi wenyewe tulioipa hiyo kazi na kuanza kutukamua sisi... Kwanini TUSIITOE HII SERIKALI YA CHAMA HIKI TUWEKE CHAMA KINGINE?
 
Naunga mkono hoja ccm hawana jipya tena kwenye nchi hii
 
Wamekula 10% kwenye mikataba ya wazungu [nadhani bado wanaendelea kuzitafuna] matokeo yake mikataba wanayoingia na wazungu imeshindwa kuwa na manufaa kwa mtanzania.

Sasa wanaona bora waanze kumkamua mtanzania mwenyewe, halafu watu wakilalamika wanaambiwa wahamie Burundi.

Hata kama watanzania tunaonekana makondoo, lakini pia kwa hayo majibu ya viongozi wetu nayo yanawafanya waonekane mazuzu.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa rasilimali za ardhini kama rasilimali watu ni empty set...
Unaijua DRC? ...Nigeria?
Hawa bongoflava na simba na yanga na ngono zembe unatarajia maendeleo gani...
Tozo ni kwamba hakuna namna nyingine
Nini kifanyike tena kwa dharura?
 
Kama lengo la kuwa na serikali ni kusimamia utumiwaji wa rasilimali zetu kutunufaisha na serikali imeshindwa kwa miaka 50 madarakani badala yake imetugeukia sisi wenyewe tulioipa hiyo kazi na kuanza kutukamua sisi... Kwanini TUSIITOE HII SERIKALI YA CHAMA HIKI TUWEKE CHAMA KINGINE?
Panga kura yako. Mwambie na jirani wako.
 
Hakuna nchi iliyoendelea kwa rasilimali za ardhini kama rasilimali watu ni empty set...
Unaijua DRC? ...Nigeria?
Hawa bongoflava na simba na yanga na ngono zembe unatarajia maendeleo gani...
Tozo ni kwamba hakuna namna nyingine
Ngono inalaumiwa bure tuu....wenzetu marekani wanatumia ngono kugenerate billions of dollars sie tunabaki kuikandia bure. Sie ukweli mchungu ni kwamba tupo mkundunii mwa dunia i.e tupo gizani full time
 
ewe mtanzania mwenzangu usitegemee muujiza mpya under CCM. Cha kufanya sasa hivi ni kuanza upya kwa Kudai Katiba mpya kama starting point kwa vizazi vijavyo - sisi tunaoishi leo tumeshachemka. - hatuna direction tunatoka wapi na tunataka kufika wapi kama Taifa.

Yaani ni hivi kifikikia hatua unategema TOZO kujenga nchi ujue ushakwisha kifikra.
 
CCM haina kabisa na mpango wa kutoka madarakani
 
Habari!

Sasa ni wakati muafaka wa kuachana na misaada kutoka nje, maana nao huko kwao hali ya uchumi imekaza.
Misaada inashusha heshima, mtu anayekusaidia hata akiongea upuuzi lazima ucheke ili umridhishe.
Options ni 2 tu kwasasa.

1. Kutumia rasilimali zetu kama gas, makaa ya mawe, dhahabu, na madini mengine ya vito kujijenga.
Bila kusahau fukwe za bahari na bahari yenyewe, maziwa na mito, ardhi yenye rutuba , milima, hifadhi na wanyama pori wetu.

Rasilimali za nchi hii ni nyingi, haya matrilioni ya kodi tuyatumie kama mtaji wa ku utilize rasilimali zetu.
2. Tuendelee kulipa tozo zilizopo na ziongezwe zingine ili tupate pesa za kuendesha nchi na kuleta ustawi katika jamii.

Ila katika option namba 2 tunaomba Serikali ikiri kuwa imeshindwa kutumia rasilimali tulizojaaliwa na Mungu kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo imependekeza tozo ndizo ziwe mbadala wake.
Nakubaliana na ww kwa kiasi kuhusu tozo ,
Lakini hebu tuone je nikwa kiasi gani serikali inapunguza matumizi yasiyo ya lazima .
Juzi Kati Rais alikuwa ziara Mikoani lakini ukitizama msururu mkubwa wa magari ktk msafara wake hakika haikubaliki haya Ni matumizi mabaya ya fedha zetu.
 
Ogopa sana mtu mpumbavu na mjinga anapotoa maoni. Mara nyingi hutumia maneno Kama "tume...", Tuna....", "Tupo..." nk .

Ulipaswa kusema haya ni maoni yangu, na sio kujumuisha wengine kwenye kile unachofikiria
 
Back
Top Bottom