Ndugu zanguni, hapo nyuma kidogo na sasa kwa uchache baadhi ya watu wamekuwa wakitoa kauli za kubeza kazi nzuri zilizofanywa na JPM kwa kejeli na dhihaka.
Nadhani lengo lao kubwa ni kutaka kufuta Legacy yake. Ukweli ni kwamba, hakuna mtu awaye yote anayeweza kufuta Legacy ya JPM.
Mbaya zaidi ni kwamba,wanapozidi kumbeza JPM na kazi zake ndipo wanapozidi kuumbuka zaidi.
Hapo ni lazima tukubabali kuwa, Mungu yupo upande wa JPM.
Ikumbukwe kwamba:-
1. JPM aliingiza Nchi katika uchumi wa kati katikati ya kipindi cha CORONA, lakini sasa tunaambiwa uchumi umeshuka.
2.Wakati wa JPM, vibaka walitoweka kabisa, lakini sasa wamerudi kwa kasi ya ajabu.
3. Wakati wa JPM, watumishi wa serikali walikuwa na nidhamu na walitekeleza wajibu wao ipasavyo lakini sasa ni balaa tupu. Hata kama ilikuwa nidhamu ya woga kama wanavyosema wengine lakini ilisaidia.
4. Wakati wa JPM, bei za vitu hazijawahi kupanda kiholela holela hivi, lakini sasa kila Mtanzania anajua hali ilivyo huku mtaani. Hali ni mbaya kweli kweli.
5. Wakati wa JPM, Ajali nyingi za kijinga kijinga zilikwisha kabisa lakini sasa zimerudi kwa kasi ya ajabu na kila mtu ni shahidi.
6. Wakati wa JPM, umeme haujawahi kukatikakatika kihuni huni namna hii, lakini sasa kila Mtanzania ni shahidi.
Hayo ni machache tu, yapo mengi mazuri yaliyofanywa na JPM yaliyokuwa msaada kwa Watanzania.
Rai yangu kwa viongozi ni kwamba, fanyeni tathmini ya kina muone mmekosea wapi na mjirekebishe.
Kamwe msihalalishe UDHAIFU wenu kwa kumdhihaki JPM, haitawasaidia isipokuwa mtaharibikiwa zaidi.
Acheni visingizio vya ajabu ajabu, maana sasa kila mnapofeli jambo fulani mnasingizia CORONA kana kwamba CORONA imeanza baada ya JPM kututoka.
Hivi karibuni mmeanza kusingizia vita vya Urusi na Ukraine. Visingizio vingi ni dalili za wazi kabisa za udhaifu wa kiongozi/viongozi.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.