Tukubabali au tusikubali, Hayati Magufuli alikuwa mkombozi wetu

Tukubabali au tusikubali, Hayati Magufuli alikuwa mkombozi wetu

Ndugu zanguni, hapo nyuma kidogo na sasa kwa uchache baadhi ya watu wamekuwa wakitoa kauli za kubeza kazi nzuri zilizofanywa na JPM kwa kejeli na dhihaka.

Nadhani lengo lao kubwa ni kutaka kufuta Legacy yake. Ukweli ni kwamba, hakuna mtu awaye yote anayeweza kufuta Legacy ya JPM.

Mbaya zaidi ni kwamba,wanapozidi kumbeza JPM na kazi zake ndipo wanapozidi kuumbuka zaidi.
Hapo ni lazima tukubabali kuwa, Mungu yupo upande wa JPM.

Ikumbukwe kwamba:-
1. JPM aliingiza Nchi katika uchumi wa kati katikati ya kipindi cha CORONA, lakini sasa tunaambiwa uchumi umeshuka.

2.Wakati wa JPM, vibaka walitoweka kabisa, lakini sasa wamerudi kwa kasi ya ajabu.

3. Wakati wa JPM, watumishi wa serikali walikuwa na nidhamu na walitekeleza wajibu wao ipasavyo lakini sasa ni balaa tupu. Hata kama ilikuwa nidhamu ya woga kama wanavyosema wengine lakini ilisaidia.

4. Wakati wa JPM, bei za vitu hazijawahi kupanda kiholela holela hivi, lakini sasa kila Mtanzania anajua hali ilivyo huku mtaani. Hali ni mbaya kweli kweli.

5. Wakati wa JPM, Ajali nyingi za kijinga kijinga zilikwisha kabisa lakini sasa zimerudi kwa kasi ya ajabu na kila mtu ni shahidi.

6. Wakati wa JPM, umeme haujawahi kukatikakatika kihuni huni namna hii, lakini sasa kila Mtanzania ni shahidi.

Hayo ni machache tu, yapo mengi mazuri yaliyofanywa na JPM yaliyokuwa msaada kwa Watanzania.

Rai yangu kwa viongozi ni kwamba, fanyeni tathmini ya kina muone mmekosea wapi na mjirekebishe.

Kamwe msihalalishe UDHAIFU wenu kwa kumdhihaki JPM, haitawasaidia isipokuwa mtaharibikiwa zaidi.

Acheni visingizio vya ajabu ajabu, maana sasa kila mnapofeli jambo fulani mnasingizia CORONA kana kwamba CORONA imeanza baada ya JPM kututoka.

Hivi karibuni mmeanza kusingizia vita vya Urusi na Ukraine. Visingizio vingi ni dalili za wazi kabisa za udhaifu wa kiongozi/viongozi.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Hitler nae alikuwa na wapenzi wake hata Idd Amin Dada Kuna watu wanamkumbuka.

Lakini baba wa mbinguni hatuna budi kumshukuru Kwa alilo tenda kwa taifa letu 17/3/2021.

Hakika Leo magereza yangekuwa yamefurika Kwa kujaa kesi za walikuwa wanatuhumiwa kumtukana huyo mtu.
 
Kwa hiyo mmekata tamaa baada ya mkombozi wenu kufariki?
Poleni sana.

Pia mkumbuke kuwa, Magufuli huyo huyo kwa watu wengine wengi alikuwa ni muuaji, mkatili, Dikteta, mfilisi na shetani.
Watu wengine alikuwa dikteta,wezi, wazembe ataachaje kuchukiwa,kafa tunaona walioko serikalini wanahangaika na marehemu huku mambo yakidorora kwa Kasi ya 4g.
 
Alikuwa mkombozi wako ww na family yako na watu wako, kwangu mimi alikuwa mnyang'anyi! Alikuwa katili, alikuwa dhulumati! Kwangu mimi na family yangu na ukoo wangu na ndugu na jamaa zangu wote walikuwa waathirika wa magufuli, nili furahi alipolala yooo na ninasema am happy now Mimi na family na ukoo wangu na ndugu zangu na jamaa zangu wote we are so happy now.
Sasa endeleeni kuiba.
 
Alikataza watu wasiseme vyuma vimekaza. Itachukuwa miaka kumi na tano kurekebisha uchumi alioharibu na Kisha kupika takwimu kutengemaa.

Pole sana Mama Samia...
 
Alikua aibu kwa taifa. Hakufuata misingi ya utawala bora, hakuwaheshimu wenzake aliwafokea na kuwafukuza kazi hadharani bila kujali utu. Aliumiza watu wengi. Elimu yake aliyoisomea kwa kiingereza ilitia mashaka sana kwani hakuweza kuzungumza kiingereza ata sentence mbili kwa usahihi. Kifupi alikua ni aibu kwa taifa
 
Alikua aibu kwa taifa. Hakufuata misingi ya utawala bora, hakuwaheshimu wenzake aliwafokea na kuwafukuza kazi hadharani bila kujali utu. Aliumiza watu wengi. Elimu yake aliyoisomea kwa kiingereza ilitia mashaka sana kwani hakuweza kuzungumza kiingereza ata sentence mbili kwa usahihi. Kifupi alikua ni aibu kwa taifa
Kiingereza ndio kipimo cha elimu sikuhizi? Mbona wachina ni ma Tycoon na wanaongelea kingereza cha “Noti Byutifuley”
 
Kwa hiyo mmekata tamaa baada ya mkombozi wenu kufariki?
Poleni sana.

Pia mkumbuke kuwa, Magufuli huyo huyo kwa watu wengine wengi alikuwa ni muuaji, mkatili, Dikteta, mfilisi na shetani.
Kaua mtu mmoja halafu Kazuia mfumuko wa Bei Kwa watu million 60...unahisi Sisi tutajali huyo mmoja aliyekufa au maslahi yetu watu million 60?
 
Sampling ya kumuita Magu katili ati inakamilishwa na tuhuma za ben saa8, kupigwa shaba kwa Tundu lissu 😅 out of 60million people! Hakuna mwenye ushahidi ila ndio utetezi wenu ulipo
Yani hata kama Ni Kweli aliwaua....Yani watu million 60 tusahau mazuri yote aliyotufanyia kwasababu ya Hao watu wawili?
 
Kwa hiyo mmekata tamaa baada ya mkombozi wenu kufariki?
Poleni sana.

Pia mkumbuke kuwa, Magufuli huyo huyo kwa watu wengine wengi alikuwa ni muuaji, mkatili, Dikteta, mfilisi na shetani.
Nchi hii ina kirusii kibayaa sana..ni ngumu kuendelea. Sababu kubwaa ni moja! Ideology za nchi hii ziko mbili kubwaa..ambazo zinaathir maendeleo. Mfano rais hachaguliwi kwa kuangalia ubora wake katika utendaji bali anachaguliwa kwa kuangalia mrengo wake! Kwamba kama ametawala wa mrengo huu baas ajae anatakiwa awe wa mrengo huu ili kuridhisha pande mbili kwa kila awamu! Hilo limeenda hadi kwenye kusupport na kupinga..rais akiwa wa mrengo fulani baas wale watu wote wa mrengo huo humpa support hata kama anafanya upuuzi...provided ni wa mrengo wao baas watampa support tuu..hili liko hasaa kwenye mrengo mmoja zaid..mana huo mrengo hawana habari na maendeleo ya nchi wao wameshazoea kula kulala suala la kupiga hatua kimaendeleo halipo kwao..mrengo mwingine kidogo wameachana na huo utumwaaa..asilimia kubwa wanataman kuona nchi ikisonga mbele..na wengi wao humpinga hata akiwa akiwa ni kiongoz wa mrengo wao ikiwa atafanya tofauti na matakwa ya nchi kwa ajili ya maendeleo.
Suluhisho ni lipi? Suluhisho ni moja tu
Ili hii nchi iendelee baas ni lazima igawanywee kwenye pande mbli..kuwe na nchi mbili..kila eneo litawaliwe na mrengo ambao ni pupular..baas..hapo ndipo tutaona maendeleo ya mrengo fulan huku mrengo mwingine ukiendelea kula urojo..kucheza ngoma na singeli kusoma lugha za ajab ajab na kuitupilia mbali elimu dunia.
Maendeleo hayana chama.
 
Wakati wa JPM, bei za vitu hazijawahi kupanda kiholela holela hivi, lakini sasa kila Mtanzania anajua hali ilivyo huku mtaani. Hali ni mbaya kweli kweli.
Hivi sukari ilipanda bei wakati Gani? mbona mnapenda sana kumkuza JPM?

Uchumi ulipanda sababu tu ya Miradi mingi kujengwa say SGR, JNHEP, Bombardiers, Kibaha highway etc so kwenye GDP unaonekana component ya investment inapanda juu even though faida za moja kwa moja hazijaonekana maana Miradi haijakamilika.

Kingine TRA ilikua inakamua wafanyabiashara so walikua hawachukui faida ila mpaka mtaji so obvious mwanzoni Hazina lazima ijae pesa ila long run ndio wafanyabiashara wanapungua na ajira kuisha, mwisho wa siku ndio uchumi unaanza kuona effects za kupungua wawekezaji!!

Kingine JPM alicheza na media sana, mfano ajali za vivuko,matetemeko, sijui lucky Vincent zilitokea awamu Gani? Wanajeshi wetu huko DRC zaidi ya 20 waliuawa awamu Gani? Ila kwa sababu media ziliminywa zikawa haziripoti mara kwa mara hizi ajali labda social media tu so ikajengwa perception kuwa ajali ziliisha.

Kuhusu umeme performance audit ya CAG ilionyesha mashine zilikua overrun zaidi ya scheduled maintenance Ili tu kufurahisha JPM madhara yake imebidi zifanyiwe maintenance sahivi hadi kusababisha umeme ukatike katike sana. Sasa hapo Nako mnamsifia JPM? au mnashauri na Makamba asingefanya maintenance ilimradi tu umeme usikatike mfurahi?

Hayo yaliyobaki ni media propaganda tu kuliko uhalisia..... Mfano uchumi wa kati tulioingia ulikua Low-Middle Income yaani uchumi wa kati wa CHINI So haikua sustainable lakini tungefika uchumi wa kati wa JUU hapo tungesema tumeporomoka sana.

Msikuze mambo sana JPM was average but branding ilikua kubwa kuliko uhalisia.
 
Nina wasi wasi, PhD siyo level ndogo, kuna kitu hakipo sawa
Acheni ushamba, i can do more in writing than speaking! Haimaanishi kwakuwa sipendelei sana kuongea kiingereza i aint smart!

Nina hakika vyeti vya ndalichako ni visafi kuliko vyako japo hawezi ongea kingereza kilichonyooka vizuri.
 
Alikomesha mambo yote ya blaaa blaaa, sasa yamerudi kwa kasi. Ninapenda hii "tajiri kufanyiwa lolote bila woga" sasa mguse tajiri unuke.
Furaha ya masikini kuona Tajiri anateseka kama yeye...umasikini ni mbaya na umasikini unaleta roho mbaya na uchawi
 
Back
Top Bottom