Salamu kwenu ndugu zangu katika falsafa za JPM
Kutokana na kile kinachoendelea hivi sasa,nami nimeona ni vyema nikasema haya kwenu...
Ndugu zangu katika falsafa/itikadi za MWAMBA /MZALENDO/MPAMBANAJI ...JPM nyote ni mashahidi wa mashambulizi ,matusi na dhihaka za kila aina vinavyoelekezwa kwake (ingawaje yeye hayupo tena milele ) na baadhi ya wanasiasa katika siku za hivi karibuni
Nanyi ndugu zangu hampaswi KUUMIA wala KUHUZINIKA kutokana na haya bali kufahamu kwamba hizi ni dalili za USHINDI kwetu sisi wafuasi wa falsafa zake
Kinachosababisha yote haya ni ukweli kwamba,MAMLUKI wamegundua Hayati JPM anaelekea kuwashinda pasipo yeye kuwepo na aliwashinda alipokuwepo....hivyo basi ROHO ZINAWAUMA
Kwanini roho zinawauma?
Lazima mjue kwamba 'WAKUBWA'wengi ndani ya chama hawakumpenda JPM kutokana na misimamo yake juu ya MASLAHI ya Taifa hili,na jinsi alivyokubalika kwa kiasi kikubwa miongoni mwa raia ikizingatiwa kwamba JPM kwao ni 'MSHAMBA TU WAKUJA' na wao ndio 'WENYE CHAMA NA NCHI'(wanajidanganya saaaana)
Kwakuwa wao hawakukubaliana naye na walishindwa kumfanya afanye vile walivyotaka wao ,basi wakajiaminisha kuwa hata wafuasi wake wanamuunga mkono kwa sababu tu ya kujipendekeza ili kupata chochote kitu au sababu ya kuogopa mamlaka yake kama ambavyo wao walikuwa wakimuogopa na kumuunga mkono kinafiki
Sasa cha ajabu ni zaidi ya mwaka JPM ameshatangulia mbele za haki,wao ndio wenye madaraka kwa sasa,na wanafanya vile wanavyoona wao sawa,lakini wafuasi wa Yule 'WAKUJA MSHAMBA' wanazidi kuongezeka kila Leo,na karibu kila wafanyalo
Wanajikuta wanakosolewa na kukumbushwa kwamba JPM alifanya hivi na vile ama hakufanya hivi na vile
Sasa hapo ndio ROHO ZINAPOWAUMA na sasa wameamua kupambana na Hayati kwa namna zote ikiwemo kutumia VICHECHE WA KISIASA kama Zitto
We jiulize kwanini katika kipindi hiki,ambacho nchi inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi hasa kwa wananchi wa kawaida,wanasiasa wa dizaini ya Zitto wamekazania kumzungumzia Hayati JPM na si matatizo yanayoitatiza jamii kwa sasa?
Ila wasichokijua ni kwamba katika kipindi alichokaa madarakani,JPM amefanikiwa kupanda mbegu ya mageuzi katika siasa za nchi hii,kamwe hazitorudi kuwa kama walivyozoea
Ukitaka kuthibitisha hilo angalia hata hapa hapa tu JF,kuna members kibao walikuwa wanaisapoti CCM hata kabla JPM hajawa Rais, lakini leo hii wapo mstari wa mbele kwenye kuikosoa na kutokubaliana na hiyo hiyo CCM pamoja na viongozi wake,na watu wa namna hii wapo kuanzia chamani, serikarini na mitaani,ni suala la muda tu TUTAELEWANA
hivyo ndugu zangu katika falsafa za JPM,kama nilivyowaambia hapo mwanzoni,
HAMPASWI KUHUZUNIKA wala KUUMIA kwa haya yanayoendelea sasa kwa sababu USHINDI U DHAHIRI UPANDE WETU,ndio maana WANATAPA TAPA kwa kulitambua hilo
VIVA ITIKADI ZA JPM..VIVA WAZALENDO WE KWELI WA YAIFA HILI
Nb: MODERATERS mkiona hii thread inawakera,futeni tu kama mlivyofuta ule wa juzi