Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

Not to take anything away from Pelle ila tukumbuke hakukuwa na offside rule miaka yake, bila offsides goal-poachers kama Inzaghi, Crespo, R9 wangekua na magoli karibu au zaidi ya hayo.
 
Not to take anything away from Pelle ila tukumbuke hakukuwa na offside rule miaka yake, bila offsides goal-poachers kama Inzaghi, Crespo, R9 wangekua na magoli karibu au zaidi ya hayo.
Swali dogo na jepesi offside rule imeanza mwaka gani mkuu, usisikilize story za vijiweni mkuu,
Mie pele nimemfatilia hakuwa mchezaji wa kuvizia na kufunga, alikuwa ni mtu wa kukusanya kijiji, anakusanya kijiji, lubambawe, anawakusanya wa nanjilili, sijui kisarawe, anaenda kuwaacha kolomije halaf ndio anatupia mpira wavuni.
 
Offside rule imekuwa ikifanyiwa amendment every now and then, offsides za miaka hii na miaka ile ni tofauti. There was literally no offsides miaka yao.

Alikuwa mchezaji mzuri sana tu na sipingi kuhusu kukusanya kijiji ila kutokuwepo kwa offsides kulimpa magoli mengi zaidi.
 
Bado hujajibu swali, offside rule imeanza mwaka gani, hili ndio swali la msingi.
 
Sasa wewe kwa mpira aliokuwa anacheza pele hiyo offside itatoka wapi maana alikuwa anatoka katikati ya uwanja mpaka anaenda kufunga bao
Kasi, chenga maridhawa, miguu kama sumaku ya mpira, jicho la kuliona goli kutoka mbali au karibu acha tu mkuu nakosa namna ya kumuelezea
Ingia youtube umtazame na umlinganishe na huyo maradona au messi au yeyote hutaona kama yeye
 
Bado hujajibu swali, offside rule imeanza mwaka gani, hili ndio swali la msingi.

Offside rule ilianza kutumika rasmi 1990 miaka 13 baada ya Pelle kutandika daluga. Mwaka 2003 na 2005 ilifanyiwa marekebisho tena.

Pelle anahesabu hadi magoli aliyofunga kwenye unofficial games mathalani magoli aliyofunga wakati akiwa coastal guard kitu ambacho players wengine hawafanyi hususan miaka hii

Pamoja na goal ratio yake kuwa incredibly amazing ila hakuwahi kuwa mfungaji bora wa world cup hata mara moja.
 
Na gwiji wa madrid fundi di stefano.. Na balaa lake lote alikubali pele si wa dunia hii..
Swadakta mpira ule ilikuwa kama vita wachezaji walaini haikuwa sehemu yao ilitakiwa uwe nunda sugu na fundi pia haikuwa lelemama. Gwiji la kiargentina huyu Alfred di stefano aliutambua uwezo wa edson akiwa na Francisco gento na Maria zarraga walifanya yao.
 

Katika hili la offside sikupingi, Nikikupa magoli ya pele utizame sijui kama utaona goli la offside, offside imo kwenye sheria za soka toka miaka hyo ila 90 ndio ikarekebishwa ikawa official ambayo ina utofauti na ya miaka ya nyuma, miaka ikisogea sheria pia zinarekebishwa, ila msingi wa sheria ni ule ule sheria za soka hazijawahi kubadilishwa, kama sikosei offside imo katika sheria namba 11 ya soka.

Unataka official games chukua hii santos alipiga games 656 goli 643,new york cosmos 107 goli 64 brazil apps 92 goal 77 unapata total goals 784, si jambo jepesi nitafutie mtu hatari kama huyu mtu, ligi ya brazil alikiwa mfungaji bora mara 11(9 ni mfululizo)
Hapo national team kapunguziwa goli 18 katika games 22 kitu ambacho naona si sahihi mechi za kirafiki nazo ni mechi na alikuwa akifunga kwa miguu wala sio mikono kama basketball[emoji23] [emoji23]

Twende sasa katika hyo world cup, unajua mashabiki wengi wa soka, hawamjui vizuri pele ukiwatajia pele akili zinakuja kwenye ufungaji tu, unajua kama pele alikuwa anacheza as a playmaker wakati mwingine!?
Sasa world cup kweli hakuwahi kuwa mfungaji bora ila katika games 14 alifunga goli 12 akiwa na assist 10, kombe la dunia mwaka 70 kule mexico alifunga goli 4 na assist 7..

Ukinitajia mchezaji yoyote kati ya hao mnaotaka kulinganisha mwenye rekodi kama hii world cup mie najipa ban ya week 2.
 
Watu hawaangalii ugumu waliopitia watu, watu wamecheza katika viwanja vibovu, sheria haziwalindi kwa kias kikubwa eti siku hizi mchezaji anavutwa jez penat[emoji23] [emoji23]
 
Hivi unafikiri ni rahisi kwa wazungu kuamua kusema pele (black), kuwa ndiyo number moja???,, Ujue kuna kitu cha ziada alikuwa nacho,, na takwimu si hizo hapo??, Mbona hakuna mwingine kazifikia hata huko santos??
 
Hata baada ya miaka 50-60, akitokea mchezaji mwingine bora, wataanza kusema messi alikuwa anapiga chenga anaangaliwa tu,, binadamu hawakosagi sababu
 
Uko deep
 
Hebu mfatilini pele na santos yake
Walikuwa wanacheza na team kutoka ulaya kule ambapo soka lilikuwa juu enzi hizo kama Italy na walicheza na team kama Ac milani juventus na zile zilizokuwa na viwango vya juu na huko ndiko Pele alikokutana na magwiji ukiacha team ya taifa lake
 
Pele ni mchezaji hodari kwa wakati wake, Mpira wa zamani si sawa na wa leo. Sheria za mpira wa zamani si sawa na za sasa. Zamani wachezaji walicheza mpaka wakiwa wazee. Siku hizi miaka 35 unakuwa shaibu.
 
Pele ni mchezaji hodari kwa wakati wake, Mpira wa zamani si sawa na wa leo. Sheria za mpira wa zamani si sawa na za sasa. Zamani wachezaji walicheza mpaka wakiwa wazee. Siku hizi miaka 35 unakuwa shaibu.
Mpira wa sasa hauvutii kabisa mabeki hakuna siku hizi
Pele ukibahatika kuona vidio zake na za wachezaji wengine utakiri mwenyewe kuwa hakuna kama pele kwa sasa labda miaka 50 ijayo huko
 
Mpira wa sasa hauvutii kabisa mabeki hakuna siku hizi
Pele ukibahatika kuona vidio zake na za wachezaji wengine utakiri mwenyewe kuwa hakuna kama pele kwa sasa labda miaka 50 ijayo huko
Mkuu unamaanisha au!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…