Tukumbuke kisa hiki cha msanii Noorah na Fiesta

Tukumbuke kisa hiki cha msanii Noorah na Fiesta

NOORAH Kitandani…..FIESTA Uwanjani!!

Japo muda kidogo umepita tangu utokee huu mkasa lakini sio mbaya tukikumbushana hii kitu. Jinale halisi ni Haji Nurah Ngarama almaarufu kama ‘Noorah’ au Baba Stylz.

Mwaka 2005 Noorah mwanachemba Squad alipata bahati ya kushiriki kwenye tamasha la Fiesta. Sasa akiwa katika hiyo Tour ya Fiesta alipata ajali mbaya sana,angalau kwa kipindi hicho ajali haikutangazwa sana kama kulivyotangazwa kufana kwa show hizo.

Noorah alipata ajali akiwa kazini. Baada ya kwenda hospital daktari akasema hatakiwi tena sio tu kufanya show bali hata kufanya kazi yoyote ngumu. Hapo ndipo mtihani kwa MwanaChemba huyu ulipoanzia.

Noorah akaona hapana, sasa ntaishije aisee? Akaamua kujivuta hadi muhimbili kwa uchunguzi zaidi ndipo ndipo ilipogundulika kuwa ajali ile imesababisha sehemu ya fuvu la kichwa chake kupata ufa.

Daktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili akashauri kwamba sio tu kutofanya kazi ngumu bali mgonjwa huyo anatakiwa apumzike kabisa. Hakuwa na namna Noorah akapumzika na kuwa baba wa nyumbani.

Noorah akapumzika lakini show za Fiesta ziliendelea na zingalipo zinaendelea mpaka leo, kwao yaliyotokea kwa Noorah ni kama ajali kazini tu. Hapo kwenye ajali kazini ndipo hasa kwenye mzizi wa matatizo. Kwanini ajali kazini kwa wasanii hazina bima? Mikataba karibia yote ya wasanii haizungumzii wasanii watafidiwaje wakipata ajali ya kupelekea ulemavu/ugonjwa/kufariki wakiwa kazini. Mikataba mingi haitambui show kama nazo ni kazi iwe ya muda mfupi au mrefu. Kuburudisha kunachukuliwa juu juu tu.

Katika wimbo NSSF Mbeleni wimbo unaopatikana katika mixtape za Anti Virus, Mapacha walizungumzia hii kitu. Nini mustakabali wa msanii katika maisha yake ya baadae? Hii sio kwa Noorah tu bali wengi wanakutana na changamoto kama hizi wakiwa kwenye mikataba ya kazi.

Noorah alikaa nyumbani mpaka alipoona sasa inatosha,akaamka na kwenda shule pale IFM na baadae akarejea tena kwenye muziki ingawaje haikuwa kama zile zama akiwa katika ubora wake.
Na Iddy Mwanaharam
Shame on you.
 
Ulilisoma wapi na mimi nikalisome kisha nimuulize maswali yangu?
bytheway, you sound kama mleta mada with another ID, (just curious) lol.
Usipende kuongozwa na hisia ID mbili mimi za kazi gani, kama hata ukitaka jina langu halisi naweza kukupatia, mimi si Iddy Mwanaharamu wala mleta mada na JF si chanzo pekee cha habari. Mtafute Facebook
 
mleta mada huyo kaja na ID nyingine kujitetea umemuuliza aliisoma wapi hii habari hajajajibu 😂😂😂
Punguza Hisia, nimeshajibu nilisoma kwa Iddy Mwanaharamu Facebook. Jf si chanzo pekee cha habari. ID mbili za kazi gani hata ukitaka jina langu halisi naweza kukupatia.
 
SIKUMBUKI KAMA AJALI YA NOORAH ILIKUWA NA UHUSIANO NA FIESTA

NOORAH hakupata ajali akiwa kazini alipata ajali akiwa na demu wake (sandra)

nakumbuka gari ilikuwa rav 4 huyo demu wa noorah alikuwa anasoma uganda (Kenya ndio sahihi nimesahihishwa) na alikuja tanzania bila kwao kujua

lengo lilikuwa kumuona bwana ake akiperfom sasa baada ya noorah kumaliza show yake wakawa wanarudi wote wamelewa na wako speed ulitokea ubishani

maana noorah alikuwa anataka kumrudisha yule demu kwao(oysterbay) na yule demu hataki kurudi kwao maana nyumban kwao walikuwa wanajua yupo shule Kenya

katika mabishano huku gari ikiwa speed yule demu aliisukuma gear kwenye parking

kama ujuavyo gari za zaman hazikuwa na sensor za kutema gear ya packin gari inapokuwa speed kali basi ilifanya tairi zote nne kufunga ghafla na gari ilibingirita mara nane

noorah hakufunga mkanda alitupwa nje ya gari na akapata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu alikuwa anamkumbuka huyo demu tu...

na siyo kwamba alijipeleka hospital noorah alitoka eneo la ajali akiwa hajitambui kabisa alikuja kupata fahamu akiwa hospital

alikaa sana muhimbili hadi alipokuja kupona na kuendelea na mziki pamoja na masomo (IFM)

hawa jamaa fiesta wana mapungufu yao ila sometimes mnazidisha kuwaonea

Ya yule bo.y.a ilikua fix
 
Watoto wa Luge wameamua kujazana hum kutetea Unyama aliofanyiwa Baba Style....
BILA hata andiko la Iddy...Mimi Noorah mwenyewe kanipa malalamiko haya...
Na nimeishi nawanchemba wote hakuna aliyewahi Kuacha kulalamikia show hizi za kidwanzi.
Nani asiyejua waliopinga mikataba waliishia kutengenezewa sura na taswira mbaya ili waendelee kuogopwa na kuonwa miungu mtu.
 
Inamaana Unapingana na Muhusika...
Chanzo changu ni Muhusika wewe umehadithiwa...
MBONA hutaki kusema ilikuwa show ya nini?
Ilifanyika wap?
Msipende kuwa mawakala wa Shetani.....
Hata kama ilikuwa show ya FIESTA jamaa hakupata ajali akiwa stejini kapata hiyo ajali kaishatoka huko Fiestani kwahiyo waandaji wa show hawahusiki tena hapo,mfano umetoka ofisini saa kumi na moja umepita sehemu then saa tatu usiku unaelekea home ukapata ajali utasema hiyo ajali umeipata kazini??
 
kama sio Yeye ni vibaraka wake
kama sio Yeye ni vibaraka wake
IMG-20181127-WA0012.jpg
oya babu tale unajua mwisho wa siku bado we ni mfanyakazi wa kusaga....kweli naanza muelewa lowasa kuhusu watanzania kukosa elimu
 
Back
Top Bottom