Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

"Ni Kwamba"--huyu alikuwa mwalimu wetu wa Siasa enzi hizo. Alikuwa kila baada ya sentesi 2 anatumbukiza "ni kwamba",siku moja tukaamua kumuhesabia hizo ni kwamba zinakuwa ngapi ktk kipindi cha dk 45;jamaa yetu akahesabu zikafika 78,basi ndo likawa jina lake hilo.
Kama Isn't it!
 
Kilimanjaro boys high school, Rombo
1. Domo chemba- mwalimu wa history na geography
2. Maza moka mathematicsa
 
Aisee ndo swali pekee nilikuwa naanza kulijibu kwny paper ya math...all really number(kama sijasahau)
Mwalimu Domain, alikuwa anafundisha hesabu na alophamia shuleni kwetu topic aliyoanza nayo ni ya mambo ya domain na range. Kwa hiyo kila dakika utamsikia akiuliza what is the domain?
 
Kuna sir alikuwa anatufundisha biology alikuwa na alama kama ya DC jokate tukawa tunamuita kidot
 
Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:

1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo

2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.

3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka

4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake

tupeni majina zaidi
Paree kutokana na jina parenchyma😂😂😂😂😂😂
 
  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Boom - mwalimu wa History O level Geita secondaru, alikuwa mkuda sana.Alipewa jina hilo alipokuwa anaelezea athari za economic vita vya pili vya dunia kwenye uchumi mojawapo ikiwemo boom na recession.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fuvu:
huyu alikuwa discipline master. noma. mwembambaaaa kama snoop dogg.

Kisu:
Bonge la headmaster niliyewahi kumuona. Aligeuza shule iliyokuwa ya wahuni kuwa shule yenye heshima inayofaulisha kwa kiwango cha juu bila mitihani kuvuja. Huyu jina yake kamili ni Kisusange. Kuna wakati alihamaki, akauliza wanafunzi: "naskia kuna wanafunzi wananiita Kisu, hivi wewe baba yako unaweza kumuita ba?"
fuvu sio moro sec kweli
 
chief nanga- mwl wa lg2 form6 kila akitoa mfano wa character kwenye things fall apart,lazma amtaje chief. Kilaza-mwl. wa history1 alikua anapenda kutuita vilaza,hatimae jina likamgeukia yeye. Continental drift- ticha wa jog1, hata akiwa anaadhibu wanafunzi,utaskia cont.drift hiyooo...Vinyoya-rector alikuwa anapenda kuvaa pensi kubwa na tsht alaf miguuni vinyweleo kama simba dume
Tosa hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom