Ndotomtaa, Son of Alaska, Maane,
Hakuna sababu ya kulia ndugu zangu. Sisi sote ni wafu watarajiwa. Nyerere alikuja, akafanya yale yaliyokuwa katika uwezo wake na akaenda mbele ya haki. Lakini hakutuacha yatima. Ametuacha na wosia, na pia ametuachia mfano. Ni wajibu wetu sisi tuliopo kuuchukua mfano huo na kuufanyia kazi. Nilipoonana naye mara ya mwisho pale NY alikuwa na masikitiko ya kutoamini kuwa Watanzania wameukataa ujamaa na Azimio la Arusha. Nikamkumbusha stori moja ya Biblia juu ya yule jamaa mpanda mbegu. Nyingine zilianguka mchangani, nyingine zikaanguka kwenye miamba, lakini pia kuna mbegu zilizoanguka kwenye udongo wa rutuba. Nikamwambia, Mwalimu wewe kwangu ni kama yule mpanda mbegu. Akaniangalia, akanyamaza. Ni wajibu wetu kuendelea kurutubisha zile chache zilizoweka mizizi kwenye udongo wa rutuba. Naamini Tanzania zipo.