Mkuu Kichuguu,
Na wenine wote mlibandika picha zaidi heshima mbele sana, mkuu umenimaliza sana na picha ya timu za mpira, ninaikumbuka sana na kwa makini picha ya timu ya Yanga,
1. Waliosimama kutoka kushoto ni Athumani Kilambo, Adam Juma, Elias Michael, Selemani Said, Abdurahaman Juma (Captain), na Mwamba Omar Kapera.
2. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Moshi Dayani, Maulidi "Mexico" Dilunga, Clement Joseph, Bona Max, na Sembuli.
Waliokosekana hapo ni Sunday "Computer" Manara, Kitwana Manara, Vivian, Muhidin Fadhili, Leodgar Tenga na Leornad Chitete. Ni baada ya hii safari ndipo walirudi bongo na kuja kupambana na timu maarufu sana ya Nigeria kwa jina la Enugu Rangers, ninakumbuka sana jinsi wananchi wengi tulivyolia machozi pale Uwanja Wa Taifa baada ya hii, yaani a heart breaking game ilikuwa ni pamabano la Raundi ya pili ya kombe la Afrika, yaani Osagefyo Kwame Nkurumah Cup, si unajua siku zile kipindi cha michezo saa mbili kassoro na mtangazaji Abdul Masudi Jalewa "The Jaws" yaani mkitoka mpirani ni lazima tena muikalie chini Radio Tanzania kusubiri michezo,
Mkuu siku ile wa-Nigeria walituweka bao moja tu, na ninakumbuka ile timu walikuwa na wachezaji wawili sijawasahau mpaka leo, yaani kpa wao Emmanuel Okalla, na Sentahaafu wao Chwuku, the high level ya perfomance ya ule mpira, sidhani kama imeshawahi kutokea Tanzania tena hivi karibuni, maana ule ulikuwa ni mpira hasa, na hasa Yanga, ambao walirudi kutoka Brazil na staili moja bongo tulikuwa tunaiiita Diognal style na kuwategea wachezaji wa timu ya adui waonekane wameotea kila wakati.
Ahsante mkuu Kichuguu, picha safi sana, Mkulu Kibunango, naomba mkuu ziweke sawa picha za wakulu hapo ambazo ziko wkenye link, yaani ziweke wazi! Duh elimu kubwa sana hapa!