Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

jamani wako wapi magavana kama ndugu yetu GILMAN RUTIHINDA leo mpaka shule iliyopewa jina lake inasadifu wasifu wake!!
je,hakuna vuiongozi tena kama hawa!!??
attachment.php

Kuna kitu kilikuwa kinafanyika jana na akina Profesa Ndulu katika kumuenzi huyu bwana.
 
Nikiwa mmoja wapo; nimemlaumu sana Kambarage kutokana na mambo yaliyotusibu sisi watanzania kama mahindi ya njano na mengineyo, lakini kitu kimoja nampa big Up mzee Kifimbo, ushauri! Tanzania tulikuwa washauri na 'Big brother' kwa nchi nyingi kusini mwa jangwa la sahara. Kitu kidogo kikienda mrama tu, haoooo wanakimbilia Tanzania wanajua watakuja kuwekwa sawa. siku hizi hayo yamepotelea wapi? Ina maana Kambarage kaenda nayo kaburini au ni viongozi wa sasa wanajishughulisha sana na mabiznes diliz wamesahau kuwa kuna kitu kinaitwa kuongoza? mtu na anisaidie....

Samwel Doe wa Liberia alikimbilia kwa Mwalimu kupata baraka baada ya kumwua Tolbert, lakini Nyerere akamrushia nje. Hata hivyo Thomas Sankara alibarikiwa na mwalimu, na mojawapo ya kauli mbiu yake ilikuwa ni kuwa anasikilizana sana na Mwalimu.
 
viongozi wa zamani kwa nini walikuwa hawana matumbo makubwa?

Wangeyapata wapi? Muda wote waliutumia kuwatumikia Watanzania. Hakukuwa na muda wa kulakula ovyo kwenye mabaa na mahoteli. Ulimbikizaji wa MALI haukuwa na nafasi na uchapaji kazi ulikuwa wa kiwango cha juu sana. Maofisini viti na meza vilikuwa vya mbao, havikupi raha ya kusinzia. Tembelea maofisi ya wakulu wetu hivi sasa. Angalia hata samani zilizoko kwenye Bunge letu, angalia aina ya magari wanayotembelea, fika kwenye nyumba za serikali alizojenga Magufuli hivi karibuni uone raha zilizomo. Kwa wenzetu MBINGUNI ni hapahapa!
 
Kishoka,
Baada ya mapinduzi ya Zanzibar na mwungano wa 1964 Abdulrahman Babu alihamia Dar-es-Salaam full time. Kulikuwepo rumours wakati huo kuwa aliogopa kurudi Z'bar kwa sababu alidhania Karume angemkolimba. Hata Salim Ahmed Salim alikuwa hatubutu kuweka mguu wake Zanzibar mpaka mwaka 1975. There's more about Zanzibar and Karume that we simply do not know.

Ni kweli kuna mambo mengi ya utawala wa Karume ambayo hayajulikani kwa wengi. Mbali ya kutoelimika, pia alikuwa aina fulani ya dikteta. Alitumia mabavu kutawala na alijifanya yeye ndiye mwamuzi wa mwisho wa kila kitu. Hakukuwa na mahakama wala baraza la kutunga sheria lililokuwa na nguvu kumzidi. Nimekibamba kitabu cha Shivji (Panafricanism or Pragmatism?) kina mambo mengi sana kuhusu muungano na mapinduzi wa zanzibar
 
Mkuu Kichuguu,

Na wengine wote mlibandika picha zaidi heshima mbele sana, mkuu umenimaliza sana na picha ya timu za mpira, ninaikumbuka sana na kwa makini picha ya timu ya Yanga,

1. Waliosimama kutoka kushoto ni Athumani Kilambo, Adam Juma, Elias Michael, Selemani Said, Abdurahaman Juma (Captain), na Mwamba Omar Kapera.

2. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Moshi Dayani, Maulidi "Mexico" Dilunga, Clement Joseph, Bona Max, na Sembuli.

Waliokosekana hapo ni Sunday "Computer" Manara, Kitwana Manara, Vivian, Muhidin Fadhili, Leodgar Tenga na Leornad Chitete. Ni baada ya hii safari ndipo walirudi bongo na kuja kupambana na timu maarufu sana ya Nigeria kwa jina la Enugu Rangers, ninakumbuka sana jinsi wananchi wengi tulivyolia machozi pale Uwanja Wa Taifa baada ya hii, yaani a heart breaking game ilikuwa ni pamabano la Raundi ya pili ya kombe la Afrika, yaani Osagefyo Kwame Nkurumah Cup, si unajua siku zile kipindi cha michezo saa mbili kassoro na mtangazaji Abdul Masudi Jalewa "The Jaws" yaani mkitoka mpirani ni lazima tena muikalie chini Radio Tanzania kusubiri michezo,

Mkuu siku ile wa-Nigeria walituweka bao moja tu, na ninakumbuka ile timu walikuwa na wachezaji wawili sijawasahau mpaka leo, yaani kpa wao Emmanuel Okalla, na Sentahaafu wao Chwuku, the high level ya perfomance ya ule mpira, sidhani kama imeshawahi kutokea Tanzania tena hivi karibuni, maana ule ulikuwa ni mpira hasa, na hasa Yanga, ambao walirudi kutoka Brazil na staili moja bongo tulikuwa tunaiiita Diognal style na kuwategea wachezaji wa timu ya adui waonekane wameotea kila wakati.

Ahsante mkuu Kichuguu, picha safi sana, Mkulu Kibunango, naomba mkuu ziweke sawa picha za wakulu hapo ambazo ziko kwenye link za Ochu, yaani ziweke wazi! Duh elimu kubwa sana hapa!
 
Wkuu wote nawapa heshima kwa picha mwanana.Kwa kweli zimenipa moyo na wakati huo huo nilipatwa na uchungu kwani taifa letu sasa hatujui linaelekea wapi.

Wakuu wote nawapa salute.
 
nilisikia ete temeke wailes,jina limetokana zamani kulikuwa kituo cha WIRELESS communication
alaafu kariakoo jina ni sababu watumwa wakifikishwa hapa hukata tamaa hence the word kariakoo lakini wengine usema it was because kulikuwa base ya askari wa CARRIER CORPS na pronoucement ya kiswahili ikawa kariakoo
sanamu la askari,katikati ya jiji,originally ilikuwa ni sanamu ya a german general jina nimemsahau
hivyo daraja la salender lilijengwa na nani,na mwaka gani,the name suggests,it was not german made,au it was by another name.and again oysterbay ilijengwa na mjerumani au mwingereza
 
'Development is for man, by man and to man'-Nyerere. Sasa hayo maisha bora JK na serikali yake ya mafisadi yako wapi ilihali nauli ya ku-commute hapahapa mjini DSM imezidi pato la mtanzania kwa siku. Its is very weired idea kusema hayo, Vunja hii serikali na kiongozi yeyote mwenye mawazo ya ki-dar es salaam kama hawa na tupeleke makao makuu Dodoma effectively DSM watu wafanye biashara.

R.I.P J.K Nyerere, in my heart you are always existing.
 
TANZANIA,the motherland,is rotten to the core,what wrong have we done to the almighty,to deserve this.hivi leo ni haki kweli sisi humu grown ups kulizana machozi,KUMFUFUA NYERERE,sababu nchi imepoteza direction.hivi leo tunaomba the second cming of nyerere.the present leadership have a lot to answer,and the way things are going,i just dont see light at the end of the tunnel.i hate to say this but sometimes peace and tranquility come at a price
 
FIELD MARSHALL,naona hii rank,imekuwa ndogo kwako,how about ukiwa six star general,maana hizi posting zako,we are becoming junkies,mwishowe hivi vibarua vyetu vitaota majani
 
Wajamani,
Ningeomba lifanyike Tangazo kwa nchi na dunia nzima. Kianzishwe kitabu na hizi picha ziwekwe ndani ya kitabu hicho. Pesa zitakazopatikana zilipie ghalama ya uchapaji na utangazaji na nyingine kidogo kwa JF. Zitakazobaki zisaidie kupeleka hivi vitabu mashuleni hasa vijijini na kwenye maktaba za kila sehemu. Kuna habari nyingi sana na watu wengi sana ambao wengine nilikuwa nawasikia tu nikiwa mdogo huku kwetu Sikonge. Kama wizara ya elimu na UTAMADUNI zikikubali basi na zenyewe zichangie kwa kiasi fulani. Siku moja niliona kwenye BBC siku ya UHURU WA TANZANIA. Niliona Taa ya DIOD ikiwashwa na kuweka sura ya NYERERE. nilishangaa sana kuwa kumbe hivi vitu vipo. Nafikiri Waandishi wa Habari wanaweza kusaidia ili hawa BBC na Wagerumani watupatie kumbukumbu zetu walizonazo na hizi zichapishwe pia. Ikiwezekana, ziwekwe hata kwenye DVD na ziuzwe. Hayo ni mawazo yangu.
 
Mkuu Kichuguu,

Na wenine wote mlibandika picha zaidi heshima mbele sana, mkuu umenimaliza sana na picha ya timu za mpira, ninaikumbuka sana na kwa makini picha ya timu ya Yanga,

1. Waliosimama kutoka kushoto ni Athumani Kilambo, Adam Juma, Elias Michael, Selemani Said, Abdurahaman Juma (Captain), na Mwamba Omar Kapera.

2. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Moshi Dayani, Maulidi "Mexico" Dilunga, Clement Joseph, Bona Max, na Sembuli.

Waliokosekana hapo ni Sunday "Computer" Manara, Kitwana Manara, Vivian, Muhidin Fadhili, Leodgar Tenga na Leornad Chitete. Ni baada ya hii safari ndipo walirudi bongo na kuja kupambana na timu maarufu sana ya Nigeria kwa jina la Enugu Rangers, ninakumbuka sana jinsi wananchi wengi tulivyolia machozi pale Uwanja Wa Taifa baada ya hii, yaani a heart breaking game ilikuwa ni pamabano la Raundi ya pili ya kombe la Afrika, yaani Osagefyo Kwame Nkurumah Cup, si unajua siku zile kipindi cha michezo saa mbili kassoro na mtangazaji Abdul Masudi Jalewa "The Jaws" yaani mkitoka mpirani ni lazima tena muikalie chini Radio Tanzania kusubiri michezo,

Mkuu siku ile wa-Nigeria walituweka bao moja tu, na ninakumbuka ile timu walikuwa na wachezaji wawili sijawasahau mpaka leo, yaani kpa wao Emmanuel Okalla, na Sentahaafu wao Chwuku, the high level ya perfomance ya ule mpira, sidhani kama imeshawahi kutokea Tanzania tena hivi karibuni, maana ule ulikuwa ni mpira hasa, na hasa Yanga, ambao walirudi kutoka Brazil na staili moja bongo tulikuwa tunaiiita Diognal style na kuwategea wachezaji wa timu ya adui waonekane wameotea kila wakati.

Ahsante mkuu Kichuguu, picha safi sana, Mkulu Kibunango, naomba mkuu ziweke sawa picha za wakulu hapo ambazo ziko wkenye link, yaani ziweke wazi! Duh elimu kubwa sana hapa!

Wapenzi wa kandambili utawajua tuu, hawawezi kujificha!
 
nilisikia ete temeke wailes,jina limetokana zamani kulikuwa kituo cha WIRELESS communication
alaafu kariakoo jina ni sababu watumwa wakifikishwa hapa hukata tamaa hence the word kariakoo lakini wengine usema it was because kulikuwa base ya askari wa CARRIER CORPS na pronoucement ya kiswahili ikawa kariakoo
sanamu la askari,katikati ya jiji,originally ilikuwa ni sanamu ya a german general jina nimemsahau
hivyo daraja la salender lilijengwa na nani,na mwaka gani,the name suggests,it was not german made,au it was by another name.and again oysterbay ilijengwa na mjerumani au mwingereza

Askari monument ya pale mjini Dar sidhani kuwa ni ya jenerali wa Kijerumani, ingeshangolewa, but who knows.

Salender bridge lilijengwa na muingereza na lilipewa jina kwa kumuenzi John Salender. I think lilijengwa labda 1936 kama kumbukumbu zangu za kuswaga vumbi kulivuka hazijaingia madoa!
 
nilisikia ete temeke wailes,jina limetokana zamani kulikuwa kituo cha WIRELESS communication
alaafu kariakoo jina ni sababu watumwa wakifikishwa hapa hukata tamaa hence the word kariakoo lakini wengine usema it was because kulikuwa base ya askari wa CARRIER CORPS na pronoucement ya kiswahili ikawa kariakoo
sanamu la askari,katikati ya jiji,originally ilikuwa ni sanamu ya a german general jina nimemsahau
hivyo daraja la salender lilijengwa na nani,na mwaka gani,the name suggests,it was not german made,au it was by another name.and again oysterbay ilijengwa na mjerumani au mwingereza

Ninavyofahamu ni kuwa:-
Watumwa waliambiwa wakate tamaa ni Bagamoyo. Na hasa waliambiwa BWAGAMOYO, umeshakuwa mtumwa tayari.
KARIAKOO ni kuwa kulikuwa na GOGO hapo, na hivyo hiyo sehemu walikuwa wakiita KALIA-GOGO. Msasani ni KWA MUSA HASSAN (Wamakonde hao wakasema KWA MUCHA-ACHANI)...... Chekeleni ni CHECK LINE, ShokaMzoba ni Shock Absorb, Fulumasinonda ni FULL MACHINE in ORDER, fingapointi ni Finger-Print...........
 
Carrier Corps was what Mswahili called Kariakoo.

Jamani hivi hata Idara ya mambo ya kale au wizara ya Utamaduni haiwezi kuwa na machapicho kuhusu haya mambo?
 
...naombeni somo,nimejaribu kutuma picha humu lakini nashindwa,naomba maelekezo tafadhali
 
Nikimkumbuka Nyerere nasikitika mno. Kweli kifo nakiheshimu, maana kama ingewezekana kufufuliwa nyerere hata kama kwa mabilioni ningeitisha fund raising afufuliwe. Eti wengine wanadai at vitu vimejaa madukani???? Je ni wangapi wanaweza ku afford kununua wakati hawapati mlo bora tena ni wa mara moja ka siku? Je ubora wa hivyo bidhaa? tumekuwa shamba la bibi kwa dumping na rushwa!!! shule uchwara za bora elimu kila kona, hadi ndani ya mabanda ya kuku yaliyokarabatiwa and not ventilated for children survival? Yaani nipeni rungu nimalize hawa viongozi waroho? Tufanyeje 2010 jamani au basi 2015? tutawezaje kupata fedha tuunde ka mtandao wa kufanya mass education (CIVICS) watu waelewe uozo wa serikali ya CCM au kama si viongozi wake wachache wabovu? Jamani future ya watoto wetu na kizazi kijacho kitakuwaje? Hofuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Back
Top Bottom