...naombeni somo,nimejaribu kutuma picha humu lakini nashindwa,naomba maelekezo tafadhali
...naombeni somo,nimejaribu kutuma picha humu lakini nashindwa,naomba maelekezo tafadhali
Wakuu wenye maarifa ya huu mchezo wa picha, tafadhali msaada hapa kwa ndugu, wazee heshima mbele kwa kuweka vitu hapa elimu ya bure na picha ni murua, historia mbele na siasa kwa pembeni yake,
Makamanda,
Kuna njia mbili, moja ni kutumia attachment na ya pili kama kutumia link ya picture ambayo inapatikana kwenye properties ya picture, ni baada ya right click katika picha hiyo. kopi link na tumia kibatoni hiki kuweka link hiyo
Du! nimechukua muda wa kutosha kuipitia hii thread toka mwanzo hadi mwisho, sio siri machozi yamenilengalenga. Imebidi nifiche uso wangu kwa wenzangu wasinione, maana kuanza kuwa na emotion za namna hii ugenini ni hatari. Ukweli nimekumbuka mbali, serikali ilipokuwa na uwezo wa kutosha enzi za mwalimu wala hali haikujificha matunda yalisambazwa ktk kuwahudumia wananchi. Leo hii kila mafanikio yanayopatikana yanaenda kwa wachache wanaojiona wana haki ya kuishi, inatia huzuni.
usafiri wa anga;
...enzi hizo, East African Airways wanatesa na Dakota ilokuwa inatua mpaka Kilwa Airport!, halafu kulikuwa na DC-8, DC-9 na DC-10 ilokuwa na regular trips to London!
...enzi hizo 'waving bay' kama inavyoonekana, ilikuwa ruksa pale terminal one, mkisindikiza shurti mpungie mpaka ndege inaporuka 😀 !!!
yule nyoka,anayeitwa CENTRAL LINE,hatumjui historia yake vizuri,what i know ujenzi wake,ndio uliwaleta wahindi nchini,eti sisi waafrika hatufundishiki,ndio maana akaletwa ponjoro ambao waliitwa COOLIES,kwa kiswahili sisi tukaita KULI naadhani hii ilikuwa 1905
HUKO kenya ujenzi wa reli ya mombasa ulimtoa kamasi mkoloni,simba wa tsavo(wanasema hawa walikuwa simba watu)wanavamia behewa usiku,wanazima taa,na kuondoka na coolie(hili swala lilijadilwa mpaka na bunge la uingereza)Alaafu wenyeji wanakata waya za mawasiliano na kutengeneza bangili,by the time hii reli inakamilika gharama ilipanda mara tatu