Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Mkuu Gaijin,

Very strong point, maswali yako ni valid saafi sana, labda tusubiri majibu!
 
Sijui kama haya nayo bado yapo hapo Dar. Tulitamba nayo sana wakati wetu, na sidhani kama kweli Dar tuliwahi kuwa na usafri mzuri zaidi ya huu. je vijana wa leo mnayafahamu? tulikuwa tukiyaita kumbakumba


Huwa inatia uchungu sana kuona mambo yote mazuri tuliyokuwa nayo zamani sasa hivi ni historia. Taa za barabarani (street lights), mitaa iliyopangiliwa vizuri, barabara nzuri za mitaani, pale Chuo Kikuu Mlimani palikuwa kama peponi, wanafunzi walisoma kwa raha sana! Leo hii ukimwambia mwanafunzi wa UDSM kwamba pale Cafeteria kulikuwa na viji-fridge vinavyotoa maziwa 24/7 hatakuamini kabisa....kwani yeye hata maji ya kunywa sasa hivi ananunua!

Ila hayo mabasi yameniumiza roho sana! Ukiviona vipanya vya Dar vilivyojichokea hutaamini kama Dar pamewahi kuwa na usafiri mzuri kiasi hicho! Something must be wrong somewhere for sure!
 

Mara yangu ya mwisho kwenda pale, ilikuwa wakati Msekwa ni boss pale longtime ago, lakini majuzi nilipta pale bro duh siku hizi unakuatna harufu mbaya sana, pole sana kwa walioko pale sasa!
 
ZANZIBAR, niliyokuwa naijua mimi,ni mambo ya sultani,mapinduzi,strongman karume,karafuu,birthplace ya fred mercury etc etc.hii forum imenifungua macho sana.kumbe zanzibar kulikuwa na reli,umeme,streetlighting na even space stations enzi hizo!! tukichukua law of averages na time span ya haya mambo,ZANZIBAR,ilitakiwa iwe HONG KONG ya africa.what exactly went wrong? je kulikuwa na capital flight to the arab world? au the opportunity cost ya kuwa na nyumba nzuri,television,raba mtoni etc etc ni education which was not invested in?
 

...waliwapa vilaza kuongoza nchi yao na matokeo ndio haya unyoyaona sasa,umaskini kwa kwenda mbele na wasipobadilika watarudi 1800s!
 

 


Tatizo ni kuwa na viongozi wasokuwa na dira wala vision, matokeo yake ndio hayo kama yetu bara.
 
Hapo Marekani alikuwa keshaanza vitu vyake,haikupita mda Karume akamtimua.

...Waasisi wa Mapinduzi nao walikuwa na 'darubini kali' miaka hiyo 😀

...wenzao dakika yeyote mpaka sasa wanatuchungulia kwa setelaiti na kutuona kama hivi...


 

Duh! Hii babu kubwa yaani mbarikiwe wakuu, historia saaafi sana maana hata mimi hapa nilikuwa nimeachwa nyuma, yaani Zenji kuna wakati kulikuwa na space station! Baaaaabu kubwa!
 
...Waasisi wa Mapinduzi nao walikuwa na 'darubini kali' miaka hiyo 😀

...wenzao dakika yeyote mpaka sasa wanatuchungulia kwa setelaiti na kutuona kama hivi...

Na zaidi with Google earh unapata picha nzuri zaidi



 

Attachments

  • znz1.jpg
    51.1 KB · Views: 253
  • znz2.jpg
    52.5 KB · Views: 248
  • znz3.jpg
    61.8 KB · Views: 251
  • znz4.JPG
    45.9 KB · Views: 247
Zanzibar imewahi kutoa vichwa viwili safi navyo ni SAS na BABU vinginevyo ni viazi vitupu mtatake msitake huo ndo ukweli ingawa unauma.
 
Zanzibar imewahi kutoa vichwa viwili safi navyo ni SAS na BABU vinginevyo ni viazi vitupu mtatake msitake huo ndo ukweli ingawa unauma.
...afanaleik wallahi, bora FMES umeanzisha hii mada, tuangalie 'mseto' wa wanazuoni wa zamani mpaka siku hizi, ...au labda sijakuelewa, maana ya 'vichwa' lazima awe ni kiongozi wa serikali, au?...

Baadhi yao ni hawa;



Abdulrazak Gurnah was born in Zanzibar and is now best-known as a novelist. His fourth novel Paradise was short-listed for the Booker Prize in 1994. His latest novel is Desertion. His main academic interest is in postcolonial writing and in discourses associated with colonialism


Sheikh Abdullah Saleh Farsy, A 20th Century example of a very long line of Islamic Scholars from Zanzibar. His most famous contribution to Islam was the publication of his 807-page QUR'AN TAKATIFU (Glorious Qur'an),

Sheikh Abdullah was appointed the Inspector General of primary schools on Zanzibar and Pemba in 1949, the Headmaster of the Arabic medium School in 1957 and the Chief Kadhi of Zanzibar in 1960. He left the Isles after the revolution of 1964 and died in Oman on November 9, 1982.


Barghash Bin Said, The third Sultan of Zanzibar, he ruled from 1870 until 1888. His mother was a slave (who was freed upon his birth; many Zanzibar Sultans were sons of slave women). His father was the settler king and first Sultan of Zanzibar, Seyyid Said (Said bin Sultan). Barghash is credited with building much of the infrastructure of Stone Town, including piped water, public baths, a police force, roads, parks, hospitals and large administrative buildings such as the House of Wonders.


Shafii Adam Shafii, the Author. Hukupata kusoma kiswahili?, Kiswahili fasihi na Kiswahili sanifu? hujapata kisanifu kitabu cha KULI?


Professor Haroub Othman wa kitengo cha sheria Chuo kikuu Dar es Salaam?
 
...afanaleik wallahi, bora FMES umeanzisha hii mada, tuangalie 'mseto' wa wanazuoni wa zamani mpaka siku hizi, ...au labda sijakuelewa, maana ya 'vichwa' lazima awe ni kiongozi wa serikali, au?...

Mkuu Mchongoma,

Ahsante sana kwa mchango wako katika hii thread, ninasema hivi sisi hapa tunatafuta wa-Tanzania wote waliowahi kwa namna moja au nyingine, kuchangia historia yetu ya taifa kwa anything they did, kama ni siasa, michezo, accademic world, na anything in general,

We are not done, bado tunaendelea, picha tunazo na historia trunayo, binafsi I am humbled na this thread kwa sababu hata mimi sikutegemea kabisa kuwa bongo tulikuwa na yote niliyoyaona humu ndani, na hasa Zanzibar nimejifunza mengi niliyokuwa siyajui kuhusu visiwani,

Na kila siku ya Mungu ninapokea salaam nzito kutoka kwa wananchi mbali mbali kuhusiana na historia nzito kutoka members kwenye hii thread, Mkuu Mchongoma Demokrasia ni kuvumliana mawazo na sauti mbali mbali,

Again ninatoa heshima mbele sana kwa wote manoshiriki kwa michango mizito sana, na tuendelee kusonga mbele wakuu.
 
kwa haya tunayoonyeshwa ya zanzibar ,ndio maana hatushangai kuona watu wazima wengi kule wanaona mapinduzi yalikuwa miyeyusho tu. kwa sababu waliopindua hawakuwa wamejitayarisha kuongoza wala kuwa na vision, ......leo unakuta maji ya kunywa tabu.....nchi iliyokuwa na mifereji mijini miaka mia naa nyuma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…