Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Mkuu elewa nilichosema, nimekutana na Kanali Nyirenda, Lusaka, Zambia in the early 80s, alikokuwa akiishi in exile na nimefika mara nyingi sana nyumbani kwake kule alikuwa akiishi kwenye mtaa unaoitwa Katimamuliro Road, mtaa ambao una bunge la Zambia, na pia viongozi wote wa juu huishi, ndipo alipokuwa akiishi,

Sikusema nimemuona jana au mwaka jana, toka early 80s, nilipokuwa nikimuona kule, mpaka leo 2008 ni miaka mingi sana, kwa hiyo inawezekana kuwa alirudi au hakurudi na inawezekana ulimuona Muhimbili, lakini I doubt it kwa sababu kwa status aliyokuwa nayo then financially na politically, siamini kama unayemsema ni yeye, na sitashangaa sana kama kweli bado yupo mzima duniani, maana nilipokuwa ninamuona kule alikuwa ni mtu wemnye umri ulioenda kidogo, kwa yeye kuwepo mpaka leo!

Ahsante Mkuu!
 
Nashukuru kwa kuliweka sawa. Kama alikuwa uhamishoni, basi kesha rudi nyumbani na ninaweza kukuhakikishia kuwa huyu aliyekuwa wodini ndiye yule kapteni Nyirenda
 
Nashukuru kwa kuliweka sawa. Kama alikuwa uhamishoni, basi kesha rudi nyumbani na ninaweza kukuhakikishia kuwa huyu aliyekuwa wodini ndiye yule kapteni Nyirenda

Pia captain Nyirenda kwa mara ya mwisho alisafirishwa kwa gaharama za serikali kwenda kupata matibabu nje ya nchi na viongozi kadhaa walitoa habari ya kuwa alikuwa anaendelea vizuri. Bahati mbaya nimesahau nchi aliyoenda kutibiwa, siku alipoondoka alionyeshwa katika TV zote za Bongo, na alitajwa kama miongoni mwa mashujaa wa Tz na aliongelea kidogo kuweka mwenge juu ya mlima Kilimanjaro, na kwanini ilikuwa yeye. Hali ya Afya na kifedha ilionekana kuwa imezorota sana wakati anaondoka nchini.

Serikali iliingilia kati baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa yupo Muhimbili ana hitaji msaada zaidi.
 
Mwenzenu hii picha inanivutia mpaka wa leo.
b00766-p04544-d01485.jpg

Natambua kuwa hii sio Thread ya maelzo mengi lakini kuweka Record straight naomba nibandike hutu tumalezo.

Hatimaye Nyirenda aenda India kwa matibabu

2008-02-14 11:41:20
Na Godfrey Monyo


Hatimaye shujaa aliyepandisha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mlima Kilimanjaro, Mzee Alexander Gwebe Nyirenda ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu.

Awali, familia ya mzee Nyirenda ilijitokeza hadharani kuomba msaada wa Dola 10,000 kwa ajili ya kugharamia matibabu ya koromeo nchini humo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu.

Hata hivyo gharama halisi za matibabu itakayotumika haikuweza kufahamika mara moja.

Awali Bw. Nyirenda alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo (THI) kwa matibabu kabla ya kuhamishiwa Hosptali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza na Nipashe jana Jijini Dar es Salaam jana, mtoto wa Bw. Nyirenda, Bi. Tima Gwebe Kuwani Nyirenda alisema baba yake alitarajiwa kuondoka kwa Air India jana saa 10:00 jioni.

Alisema taratibu zote za safari zilikwisha kamilika na kwamba yeye pamoja na muuguzi mwandamizi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bi. Clay Said watamsindikiza mgonjwa hadi India.

Alisema katika safari hiyo serikali inagharamia matibabu ya Bw. Nyirenda pamoja na gharama ya safari ya muuguzi lakini yeye amekwenda kwa fedha zilizotolewa na familia na marafiki.

Siku ya Uhuru wa Tanganyika, Desemba 9, 1961, Bw. Nyirenda akiwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipandisha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mlima wa Kilimanjaro.

SOURCE: Nipashe http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/02/14/108349.html
 
attachment.php

Baada ya Picha hii ndipo upepo mkali ulipokipiga chombo, nacho kimekuwa hakiendi sawa toka wakati huo. Kimekuwa kikiyumba karibu kuvunjika. Mabaharia walipoamua kupunguza shehena yao kwa kutupa baadhi ya mizigo bharini, nao wakakubaliana kupiga kura ya kumtafuta nani aliyesababisha tatizo hili. Kura ikawaangukia mafisadi, wakawauliza mafisadi tuwafanyaje, nao wakajibu tupeleke Ukonga. Kwa mshangao wa walio wengi, Nahodha akatangaza Msamaha, Chombo kingali baharini, Upepo ni Mkali, Tunaomba msaada Rescue scuad.
picha_ya_mwisho_ya_nyerere.jpg
 
field marshall,asante kwa maelekezo,kuhusu nyirenda,lakini bado nina kiu ya maelezo kuhusu hii MUTINY,it cannot be shrouded in mystery kiasi kwamba hata humu JF asiwepo mtu ambaye can quench my thirst
 
Mkuu Mbogela,

Duh! Ahsante kwa maelezo yako mazito sana, I mean hii imeniacha hoi sana, kama huyu mzee alirudi bongo na kufikia kulazwa Muhimbili mpaka serikali ikabidi im-rescue kwa kukosa pesa za kwenda kutibiwa nje? Wallahi makubwa sana kwangu,

Mara ya mwisho nilimuona akiwa anacheza tennis kwenye viwanja vya hotel ya wabunge wa Zambia, unajua kule Lusaka wenzetu wana Hotel maalum kwa ajili ya wabunge wao, inayoitwa Parliament Hotel ambako wote hukaa hapo wakati wa vikao vyote vya serikali, hapo pana viwanja vya michezo mbali mbali ndipo alipokuwa hakosekani,

Maisha aliyokuwa akiishi kule mkuu, ilikuwa ni balaa na watoto wake walikuwa wakisoma London, sasa leo mkuu kufikia hivi kweli dunia ni tambala bovu sana, lakini sio siri mkuu hii imenitisha sana! Ila ahsante sana kwa info hizi.
 
field marshall,asante kwa maelekezo,kuhusu nyirenda,lakini bado nina kiu ya maelezo kuhusu hii MUTINY,it cannot be shrouded in mystery kiasi kwamba hata humu JF asiwepo mtu ambaye can quench my thirst

Maelezo unayoyataka ninaamini kuwa yapo kwenye topic moja inayomuhusu Mwalimu, humu ndani ya JF yapo somewhere ambapo nakumbuka hasa Mkuu Jasusi aliichambua sana hiyo kitu, labda uwaombe Mods wakutafutie hiyo mkuu, lakini ipo somewhere humu!
 
kichuguu,

..katika picha uliyoileta inamuonyesha Nyerere,Mkapa,na Dr.Peter Onu wa Nigeria.

..Peter Onu alikuwa acting SG wa OAU baada ya Edem Kodjo wa Togo kumaliza muda wake.

Son-of-Alaska,

..wako wana-historia wanaodai maasi ya 1964 were nothing more than a labour dispute.

..askari Non-Commissioned Officers[NCO] walikuwa wanadai vyeo na mazingira bora ya kazi.

..maasi ya 1964 yaliongozwa na Sajenti Hingo Ilogi.

..Hingo Ilogi alishitakiwa na, ama alihukumiwa, au alitumikia, kifungo cha miaka 15 jela.

..Hingo Ilogi na wenzake waliwatimua askari wa ngazi za juu wa Kiingereza, na badala yake kugawa senior ranks kwa maofisa wa kizalendo.

..askari waasi, kwa mfano, walimpandisha cheo Captain Kavana kuwa Brigadier na "kumteua" kuwa Mkuu wa Majeshi.

NB:

..baada ya maasi kuzimwa na Waingereza Jeshi letu liliundwa upya, na Sam Mirisho Sarakikya akapandishwa cheo kuwa Brigadier, na CDF mzalendo wa kwanza.

..Chief of Staff mzalendo wa kwanza alikuwa ni Kavana akiwa na cheo cha Major.
 
nani kakwambia kama Nyerere hakulimbikiza mali ,kama unaijua sababu ya Mkapa kufungua genge la biashala ikulu ,usingesema hayo ?
Kifo cha Nyerere kinajulikana ni ni baada ya kufa Jamal ambae ndie aliekuwa anahifazi feza ya Nyerere kwa jina lake,ghafla Jamal alipofariki Nyerere akafunga safari hadi kwa mke wa Jamali na kuulizia ela yake ,mke wa Jamali akamjibu Bana haikuacha kitu kwa jina lako ,hapo ndipo ugonjwa ulipoanza kumtambalia Mwalim na kumuondoa duniani.
Mwiba,
Sikujua wewe ni mwongo. Jamal alikuwa hana mke alipofariki. Aliyemtunza kule Canada mpaka mauti inampata alikuwa binti yake. Sasa naelewa kwa nini FMES amenishauri niachane na the likes of you.
 
field marshall,asante kwa maelekezo,kuhusu nyirenda,lakini bado nina kiu ya maelezo kuhusu hii MUTINY,it cannot be shrouded in mystery kiasi kwamba hata humu JF asiwepo mtu ambaye can quench my thirst
Son of Alaska.
Kuna vitabu viwili vinaelezea kwa kirefu hiyo mutiny. Kimoja ni The Making of Tanganyika kiliandikwa na Judith Listowell, kingine ni We Must Run While They Walk kiliandikwa na Mmarekani William Edget Smith.
 
mzee Nyirenda lienda India kutibiwa mwezi wa Pili mapka leo haifahamiki kama alirudi au laaa? kuna mtu ana habari ya maendeleo yake hapa?
 
The commettee of fourteen


View attachment 2041

Ninaowajua kwenye hii picha ni Okelo, Ramadhani Haji Faki (mzee wa 1+1=3,kulia kwa Okelo waliokaa). Waliosimama Khamis Hemed Nyuni (wa kwanza kulia) Hafidh Suleiman Almasi (wa tatu kulia) Natepe (wa tano) na Bavuai ( wa sita)

Where is Karume? or which one is Karume?
 
Yaani huoni kama hizi picha ni nuksi tupu ,hata ukitazama kwa kina utaona haziendani na hii Jamii forum inabidi ulete tambala lile lililokuwa linatumika na zile senema za bure akina Omo na Fakcho ,si mnazikumbuka ,wakituletea filamu kwenye viwanja vya mpira.
hawa ndio waliokuwa wakihimiza siasa za ujamaa na kujitegemea ,hebu angalia Madini ya Shinyanga yalianza kuchimbwa lini ,ni wakati huo huo wa siasa zao.
Halafu mnaleta mapicha ya maiti eti tukumbuke ? hivi mkisikia kulogwa ,jamani si ndio huku ? baada ya kuzungumza mambu ya maana na maisha haya ambayo yanayokwenda na kupanda kwa kasi ya Kikwete ,mnaleta picha sasa niwaulize hivi mnafaidika na kitu gani na picha hizo wakati mpo kwenye ziki za kimaisha ? Au ndio mnajiliwaza ? Sasa kujiliwaza mngetafuta angalau mapicha mazuri yanayoburudisha moyo lakini si picha za waliotuzamisha ,mpo ?
Upinzani hauwezi kwenda mbele kwa kutazama picha za watawala au Chama cha walioko madarakani au waliokufa.
Tuna msemo wa kiswahili usemao samaki akioza mmoja ndio wameoza wote.CCM wameoza wote waliokufa na hawa waliokuwepo hai ndio usiseme ni harufu mbaya tupu.

Mwiba,

Kwa mara ya kwanza nafikiri umepoteza dira kwa maoni yangu. Kama hutaki kuzitazama picha na sinakupa matapishi, ni kwanini uendelee kupekenyua kurasa zenye picha?

Ulipofungua hii thread ukakuta Picha ya Kambarage na ukapata kichefuchefu, kwa nini ulisubiri picha za Muungano, Shamte, Malecela na Kamati ya 14 ili kichefuchefu chako kigeuke matapishi na kuwa kilio?

Waache wenye kupenda zitazama picha na wajikumbushe. Sawa na wale wasiopenda jihusisha na mambo ya Kadhi na OIC huwezi kuwashurtisha waingie wachangie ikiwa kwao OIC na Kadhi ni sawa na wewe na hizi picha!
 
Rev.Kishoka,

karume hawezi kuwepo kwenye picha hizo kwa sababu sio yeye wala Afro - Shiraz waliopindua nchi isipokuwa hawa wajomba ktk picha ambao walikuwa watu wa abrahaman babu na chama cha Umma party. baada ya mapinduzi tu propaganda zilipigwa kuwa hawa jama ni Makomunist na kuwa sasa Zanzibar imechukuliwa na utawala wa kidhalimu wa Kikomunist..

Jamaa walidumu muda wa mwezi mmoja tu kabla ya Nyerere kuwaingiza mkenge, akawavuta viongozi wa Umma party bara ati kuwapa security, akamfukuza Okello na kumachika Karume kama alivyofanya Uganda kumweka Bina Issa baada ya kundolewa kwa Idd Amin huku azma yake kubwa ni kumrudisha Obotte..
Kwa hiyo kulikuwa na mapinduzi ya aina mbili kwanza yale ya kuwaondoa Hizbu kisha kuwaondoa Umma Party ktk picha.
 
Mwenzenu hii picha inanivutia mpaka wa leo.
b00766-p04544-d01485.jpg

Icadon,

Imagine jinsi tulivyokuwa organized mwaka 1961 wakati Uwanja wa Taifa Gavana anamlisha Julius Kambarage Nyerere Kiapo na kutupa uhuru, wakati huo huo, mwenge na bendera inawekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Afande Nyirenda na timu yake!

Sasa kunkuaje tunafungua daraja huko Ruvuma/Mtwara lisilo kamilika na kukosa kivuko imara kumpeleka Raisi wetu kuvuka mto kwenda kushangilia FRELIMO?

Are retarding, going backwards in organization?
 
Rev.Kishoka,

karume hawezi kuwepo kwenye picha hizo kwa sababu sio yeye wala Afro - Shiraz waliopindua nchi isipokuwa hawa wajomba ktk picha ambao walikuwa watu wa abrahaman babu na chama cha Umma party. baada ya mapinduzi tu propaganda zilipigwa kuwa hawa jama ni Makomunist na kuwa sasa Zanzibar imechukuliwa na utawala wa kidhalimu wa Kikomunist..

Jamaa walidumu muda wa mwezi mmoja tu kabla ya Nyerere kuwaingiza mkenge, akawavuta viongozi wa Umma party bara ati kuwapa security, akamfukuza Okello na kumachika Karume kama alivyofanya Uganda kumweka Bina Issa baada ya kundolewa kwa Idd Amin huku azma yake kubwa ni kumrudisha Obotte..
Kwa hiyo kulikuwa na mapinduzi ya aina mbili kwanza yale ya kuwaondoa Hizbu kisha kuwaondoa Umma Party ktk picha.

Mkandara,

Nimeliuliza kwa makusudi kabisa ili kupata jibu kutoka kwa wajuzi humu ndani wa mambo ya Zanzibar.

Okello na wenzake katika picha, ndio mashujaa walioleta Mapinduzi. Karume na wenzake, wao waliteka nyara Serikali na kuunda Baraza la Mapinduzi, huku hawakushiriki kikamilifu katika mapinduzi.

Ukiangalia mgogoro wa Zanzibar, ni rahisi kuunda kambi tatu kuu. Kambi ya Shamte na Sultani ambao nafikiri ndipo walipo Wapemba wengi na nguvu ya CUF, Kambi ya Okello na Wenzake kina Natepe, Nyuni ambao waliishia kuingizwa JWTZ na kufifia kimya kimya na Kambi ya Karume (nadhani humu hata Mzee Thabit Kombo Jecha anaweza kuwamo) ambao ndio walitwa madaraka ya Zanzibar na kuendeleza utawala wa SMZ na kuipitisha Zanzibar katika Muungano wa Nchi 1964 na Muungano wa Vyama 1977.

Ninachojaribu kujifunza na kuchambua ni mgawanyiko ndani ya Kundi la Karume au na kuingiliwa na kundi la Okello ambako kulifikia CCM Zanzibar kupata misukosuko iliyosababisha Jumbe kuvuliwa Urais wa Zanzibar na kina Sefu ambaye yeye ni wa Kambi ya Shamte kujitenga.

Sasa kwenye vurugu kati ya Karume wa leo na Salmin Amour ni yupi anawakilisha kundi la Okello au ni mgawanyiko mpya wa Kambi ya Karume?
 
Rev.Kishoka,

karume hawezi kuwepo kwenye picha hizo kwa sababu sio yeye wala Afro - Shiraz waliopindua nchi isipokuwa hawa wajomba ktk picha ambao walikuwa watu wa abrahaman babu na chama cha Umma party. baada ya mapinduzi tu propaganda zilipigwa kuwa hawa jama ni Makomunist na kuwa sasa Zanzibar imechukuliwa na utawala wa kidhalimu wa Kikomunist..

Jamaa walidumu muda wa mwezi mmoja tu kabla ya Nyerere kuwaingiza mkenge, akawavuta viongozi wa Umma party bara ati kuwapa security, akamfukuza Okello na kumachika Karume kama alivyofanya Uganda kumweka Bina Issa baada ya kundolewa kwa Idd Amin huku azma yake kubwa ni kumrudisha Obotte..
Kwa hiyo kulikuwa na mapinduzi ya aina mbili kwanza yale ya kuwaondoa Hizbu kisha kuwaondoa Umma Party ktk picha.

Mkandara,
Nipo likizo ya kuandika ila nimeona niulizie zaidi juu ya hili.
Pana wakati nilikutana na aliyekuwa waziri huko Ghana wakati wa Jerry Rawlings. Huyu jamaa aitwaye Yaw, alianza kunipa story za Nyerere na Muungano wetu. Akasema kuwa "Muungano wenu ulikuwa umepangwa na Waingereza pamoja na USA - CIA". Lengo la huu Muungano ilikuwa ni kuwazuia Warusi wasijenge BASE yao hapo Zenji wakati huo wao USA walikuwa na base yao Kenya. Hivyo, badala ya KWENDA Zenji na kupigana, wao wakaona dawa ni KUIUNGA Zenji Tanganyika na kuunda Tanzania na JKN awe BOSS na hapo Warusi walie tu.
Anyway, sijui hili lina ukweli kiasi gani. Maana hata Uganda kama ni hivyo basi angelisema TUUNGANE. Inawezekana kuwa watu wanaungaunga kamba na kusema ilikuwa hivi ingawa ukweli uko vingine. Ila ukisoma hapo juu maelezo yako, unaona kuwa "KUNA KAMUUNGO katika matukio."
NA labda ndiyo maana Muungano hadi leo unautata. Walifanya Muungano kwa jambo jingine kabisa ila leo mambo yanafumuka. Bila ya kujali malengo yao, nafikiri Muungano unasaidia sana sisi Watanzania tusiingie sana kwenye ukabila. Muungano ukafa, Wachaga watakuwa na hali mbaya maana wanashambuliwa hata kwa Mtoto wa Kikwete kuowa dada yao.
MUUNGANO UDUMU.
 
Back
Top Bottom