Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Mkandara,
Nipo likizo ya kuandika ila nimeona niulizie zaidi juu ya hili.
Pana wakati nilikutana na aliyekuwa waziri huko Ghana wakati wa Jerry Rawlings. Huyu jamaa aitwaye Yaw, alianza kunipa story za Nyerere na Muungano wetu. Akasema kuwa "Muungano wenu ulikuwa umepangwa na Waingereza pamoja na USA - CIA". Lengo la huu Muungano ilikuwa ni kuwazuia Warusi wasijenge BASE yao hapo Zenji wakati huo wao USA walikuwa na base yao Kenya. Hivyo, badala ya KWENDA Zenji na kupigana, wao wakaona dawa ni KUIUNGA Zenji Tanganyika na kuunda Tanzania na JKN awe BOSS na hapo Warusi walie tu.
Anyway, sijui hili lina ukweli kiasi gani. Maana hata Uganda kama ni hivyo basi angelisema TUUNGANE. Inawezekana kuwa watu wanaungaunga kamba na kusema ilikuwa hivi ingawa ukweli uko vingine. Ila ukisoma hapo juu maelezo yako, unaona kuwa "KUNA KAMUUNGO katika matukio."
NA labda ndiyo maana Muungano hadi leo unautata. Walifanya Muungano kwa jambo jingine kabisa ila leo mambo yanafumuka. Bila ya kujali malengo yao, nafikiri Muungano unasaidia sana sisi Watanzania tusiingie sana kwenye ukabila. Muungano ukafa, Wachaga watakuwa na hali mbaya maana wanashambuliwa hata kwa Mtoto wa Kikwete kuowa dada yao.
MUUNGANO UDUMU.
Sikonge,
Alikuwa ni Peter Enahoro au Ralph Uwechue wakiwa New African au Africa Now waliandika makala moja miaka ya 80 iliyokuwa ikisema "100 days that made Tanzania"!
Hii stori ya CIA na Warusi si ya kuzusha ni ya kweli na nafikiri nyaraka za CIA ambazo zilikuwa classified, zimefunguliwa na zinatamka wazi ni jinsi gani walisukuma Tanganyika au Kenya waungane na Zanzibar.
Sasa kwa mkao wa Pan-Africanism na One Afrika, nafikiri hii ilikuwa opportunity nzuri kwa Mwalimu katika zile njozi zake za Afrika moja. Labda ushawishi wa Marekani kwa Karume, ulimrahisishia kazi Nyerere ambaye aliona opportunity ya kuonyesha umma na dunia kuwa Afrika moja inawezekana.
Kuna haja kubwa sana ya kupata hizo de-classified nyaraka za CIA na ziwekwe hadharani ili tuachane na udanganyifu wa wanasiasa wetu na tuamue kwa mazingira ya sasa kama tunataka muungano au la!