Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Kichuguu,Jasusi,FMES,Rev.Kishoka,son-of-alaska,

..hii thread nimeipitia na kila kumbukumbu tunayoletewa ni ya WANASIASA tu.

..kulikuwa na thread nyingine ambapo member walijaribu ku-list idols/mashujaa wao, basi huko nako kulijaa wanasiasa.

..hivi katika jamii yetu hakuna watu wengine wa kuwaenzi zaidi ya wanasiasa? hakuna madaktari, ma-injinia, bankers, wachumi, industrialists, wanasheria, mathematicians,physicists,biologists,...ambao tunaweza kuwaenzi kwa utumishi na michango yao?

Sidhani kama tunao hata watano tu!!!!!
 
jokaKuu,
Unajua, for better or worse, Genesis ya nchi yetu ilikuwa ni siasa. Katika elimu hatukuwa hata na madaktari 100 wakati wa uhuru, kwa kutofautiana na wenzetu wa Afrika magharibi kama vile Nigeria, Sierra Leone, Ghana. etc. Utakumbuka hata Chief Justice wetu wa kwanza baada ya uhuru tulimtoa Trinidad and Tobago na tulikuwa na lawyers chungu nzima kutoka Nigeria na Ghana. Wafanyikazi wengi wenye ujuzi hata katika benki zetu walikuwa Wakenya.
 
Nyani Ngabu,

..nadhani hatuheshimu tu michango ya wataalamu wetu ndiyo maana unafikiri hatuna wa kuwaenzi.

..kwani hao wanasiasa tunaowaenzi na kuwatukuza wamefanya nini cha maana?

Jasusi,

..it is almost half a century tangu tupate uhuru.

..what happened kipindi chote hicho hatuna la kusifia kwa wanataaluma wa kitanzania?

NB:

..on the other hand, if i could agree with you, tufanye nini kama taifa ili kuwa na wataalamu wa uhakika watakaoenziwa na wenetu na wajukuu zetu?
 
Picha ya juu hapo ni Idi Amin alikuwa akitowa hotuba na kuna kitu kilimchekesha mwalimu pale...Labda mzee Malecela anaweza kutuambia ni kiti gani mwalimu alikuwa akisema hapo wakati wa hotuba ya hasimu wake mkuu....Kwasababu hata sura yake inaonuesha kama kicheko flani hivi cha kiubezaji...

JMushi,
Lakini umeona Mwalimu amemgeuzia mgongo na badala yake anachati na mojawapo ya mabalozi wetu.
 
Nyani Ngabu,

..nadhani hatuheshimu tu michango ya wataalamu wetu ndiyo maana unafikiri hatuna wa kuwaenzi.

..kwani hao wanasiasa tunaowaenzi na kuwatukuza wamefanya nini cha maana?
NB:

..on the other hand, if i could agree with you, tufanye nini kama taifa ili kuwa na wataalamu wa uhakika watakaoenziwa na wenetu na wajukuu zetu?

Wanasiasa wanaoenziwa hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuongoza juhudi za kugombea uhuru. Hatuna wataalamu wa maana ktk hizo fani zote ulizozitaja. Tungekuwa nao tungekuwa tumeendelea. Ngoja nikuulize, hivi kuna mtaalam gani wa maana ktk uchumi ambaye angeendelea kukumbatia sera ya ujamaa na kujitegemea huku akiona kuwa haifanyi kazi? Hao ma injinia unaotaka tuwaenzi wameshindwa hata kutatua matatizo ya kilimo, umeme, maji masafi, n.k. Sasa tuwaenzi kwa kitu gani? Watu bado wanaugua magonjwa kama ya kichocho, utapiamlo, kisonono, na mengine mengi tu. Hao wataalamu wa afya na tiba wamefanya nini kuangamiza magonjwa kama hayo yanayoweza kuangamizwa? Jibu ni hakuna!! Sasa tuwaenzi wataalamu wa fani ulizotaja kwa minajili ipi?
 
Nyani Ngabu,

..umezungumza ya msingi kabisa. kwa kiasi kikubwa tuko pamoja.siamini kama wataalamu wote wa uchumi waliunga mkono hata mambo yalipokuwa yanaenda kombo. i would like to hear about DISENTERS waliopinga uendeshwaji mbaya wa uchumi wetu.

..labda nitoe mifano michache midogo tu:

..kuna kipindi Tanzania tulikuwa tunaongoza ktk literacy kwa nchi changa. sasa mtaalamu aliyeandaa na kusimamia elimu ya watu wazima kipindi hicho definetely ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko hawa wanasiasa tunaowasifia kila kitu.

..pia nchi yetu iliwamiwa na Iddi Amini wa Uganda. siyo kwamba tulikomboa ardhi yetu tu, bali tulimuondoa Amini, tukaweka serikali ya mpito, tukaandaa na kuendesha uchaguzi Uganda, tuka-train polisi na jeshi, na kuondoka kwa heshima zote. hivi hakuna makamanda na wapiganaji wanaopaswa kuenziwa hapa, tuna-list wanasiasa waliofeli tu.

NB:

..ndiyo maana sasa hivi vijana wanamaliza chuo kikuu moja kwa moja wanataka kujiingiza kwenye siasa.

..ukienda mashuleni hatuna watoto wanao-dream kuwa waalimu.

..nadhani kinachoendelea hapa ni matokeo ya propaganda za muda mrefu za wanasiasa kwamba they were doing something for the country, lakini leo hii hamna cha kuonyesha.
 
Nyani Ngabu,

..nadhani hatuheshimu tu michango ya wataalamu wetu ndiyo maana unafikiri hatuna wa kuwaenzi.

..kwani hao wanasiasa tunaowaenzi na kuwatukuza wamefanya nini cha maana?

Jasusi,

..it is almost half a century tangu tupate uhuru.

..what happened kipindi chote hicho hatuna la kusifia kwa wanataaluma wa kitanzania?

NB:

..on the other hand, if i could agree with you, tufanye nini kama taifa ili kuwa na wataalamu wa uhakika watakaoenziwa na wenetu na wajukuu zetu?

jokaKuu,
Umeuliza swali muhimu sana. Jibu lake pia nadhani litatokana na uamuzi wa kisiasa. Mishahara ya wataalamu kama vile madaktari lazima iongezwe.
That is a political decision. Lazima tuwe na political culture ya kuheshimu na ku-nurture our experts. Hakuna sababu ya wataalamu wetu kumaliza masomo na kukimbilia Botswana, SAF kutafuta maisha wakati huo huo tunatafuta wataalamu kutoka nje ambao tunawalipa mara nne, mara tano ya mshahara wa Watanzania.
 
..hivi katika jamii yetu hakuna watu wengine wa kuwaenzi zaidi ya wanasiasa? hakuna madaktari, ma-injinia, bankers, wachumi, industrialists, wanasheria, mathematicians,physicists,biologists,...ambao tunaweza kuwaenzi kwa utumishi na michango yao?

Doctors: Mwaisela - Alileta mapinduzi katika sekta ya afya ya kikoloni
Economist/Industrialist: Rweyemamu - alianzisha Kituo cha Ubunifu cha IPI
Mathematicians: Shayo - alianzisha Kijiji cha Teknolojia
Physicst: Njau - alivumbua njia mbadala ya kutabiri hali ya hewa
Biologist: Mshigeni -alivumbua aina fulani ya mimea
Bankers: Msuya - alianzisha benki maarufu ya watu wa Mwanga
Lawyers: Nyalali- aliongoza tume iliyoyeta mabadiliko ya kisiasa nchini
Engineers: Kinjeketile - alivumbua mtambo wa kugeuza risasi kuwa maji
 
Jasusi,

..basi na tuwaenzi hata hao wataalamu wetu waliokwenda Botswana na kufanya mambo ya maana. kwani Mwalimu naye si tunamuenzi kwa juhudi zake kukomboa majirani zetu?

Companero,

..thank you very much.

..Prof.Keto Mshigheni alipewa tuzo na UN kutokana na utafiti ktk biology. he was the 1st recepient wa tuzo hiyo toka Africa South of sahara.

..hivi kile kijiji cha Mwalimu Nyerere na Prof.Shayo bado kipo? mimi nadhani badala ya kungangana na wanasiasa kina Butiku na foundation ya Mwalimu bora fedha zote zipelekwe kuendeleza watoto kwenye hicho kijiji cha science and technology.

..ningependa sana kujua mchango wa Mwaisela mpaka kufikia wodi pale Muhimbili kupewa jina lake.
 
Wanasiasa wanaoenziwa hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuongoza juhudi za kugombea uhuru. Hatuna wataalamu wa maana ktk hizo fani zote ulizozitaja. Tungekuwa nao tungekuwa tumeendelea. Ngoja nikuulize, hivi kuna mtaalam gani wa maana ktk uchumi ambaye angeendelea kukumbatia sera ya ujamaa na kujitegemea huku akiona kuwa haifanyi kazi? Hao ma injinia unaotaka tuwaenzi wameshindwa hata kutatua matatizo ya kilimo, umeme, maji masafi, n.k. Sasa tuwaenzi kwa kitu gani? Watu bado wanaugua magonjwa kama ya kichocho, utapiamlo, kisonono, na mengine mengi tu. Hao wataalamu wa afya na tiba wamefanya nini kuangamiza magonjwa kama hayo yanayoweza kuangamizwa? Jibu ni hakuna!! Sasa tuwaenzi wataalamu wa fani ulizotaja kwa minajili ipi?

Nahisi wewe unataka kumrejesha Raj Patel, akiiona hii ataruji mbio kukupongeza!!
 
HII NI KATI YA THREADS ZINAZOONGOZA....! bravoooooo.......!
 
Doctors: Mwaisela - Alileta mapinduzi katika sekta ya afya ya kikoloni
Economist/Industrialist: Rweyemamu - alianzisha Kituo cha Ubunifu cha IPI
Mathematicians: Shayo - alianzisha Kijiji cha Teknolojia
Physicst: Njau - alivumbua njia mbadala ya kutabiri hali ya hewa
Biologist: Mshigeni -alivumbua aina fulani ya mimea
Bankers: Msuya - alianzisha benki maarufu ya watu wa Mwanga
Lawyers: Nyalali- aliongoza tume iliyoyeta mabadiliko ya kisiasa nchini
Engineers: Kinjeketile - alivumbua mtambo wa kugeuza risasi kuwa maji

kwi kwi kwi kwi kwi
 
Dah,

Engineer Kinjekitile kiboko. Photos pls...
 
HII NI KATI YA THREADS ZINAZOONGOZA....! bravoooooo.......!

Mkuu Mahesabu,

Heshima mbele, ninashukuru sana kwa maneno yako mazito sana ingawa ni machache sana, nimetiwa nguvu sana na haya maneno, ninaomba kuwashukuru Kichuguu, na hasa Mkulu Wangu Icadon kwani wengi tumefirijika sana na mchango wenu hapa,

Ninaomba kuwakumbusha wananchi wote hapa kuwa huu mjadala ndio kwanza umeanza, bado tuna picha nyingi sana za kuweka hapa, tunaenda kwa mwendo ule ule mdundo, lakini pole pole, picha na dawa yaani maneno heshima kwa wachangiaji wote katika hii topic,

Niwahakikishie tu kwua hii topic ndio kwanza imeanza, mambo bado kabisa na pole pole tutaweka picha zaidi. So far compyuter yangu imerushiwa virusi vikali sana, sasa wajuzi wameniwekea special window temporary mpaka week end watajaribu kuirekebisha hivyo ndio nitaweza kuweka picha zaidi maana sasa siwezi ku-scan picha, lakini mkuu Icadon na wengine hesima mbele tuendelee kuweka vitu hapa!

Ahsante Wakuu!
 
Kutokana na uzee wangu, ninapenda sana kujikumbusha ya Zamani. Mmojawapo wa ninaowakumbukua sana ni Mbaraka Mwinshehe Mwaruka pamoja na timu yake ya akina Kulwa Salum, Kasembe na wengineo.

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • mbaraka1.jpg
    mbaraka1.jpg
    90.5 KB · Views: 1,139
  • mbaraka2.jpg
    mbaraka2.jpg
    38.8 KB · Views: 1,117
Nyani Ngabu,

..umezungumza ya msingi kabisa. kwa kiasi kikubwa tuko pamoja.siamini kama wataalamu wote wa uchumi waliunga mkono hata mambo yalipokuwa yanaenda kombo. i would like to hear about DISENTERS waliopinga uendeshwaji mbaya wa uchumi wetu.

..labda nitoe mifano michache midogo tu:

..kuna kipindi Tanzania tulikuwa tunaongoza ktk literacy kwa nchi changa. sasa mtaalamu aliyeandaa na kusimamia elimu ya watu wazima kipindi hicho definetely ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko hawa wanasiasa tunaowasifia kila kitu.

..pia nchi yetu iliwamiwa na Iddi Amini wa Uganda. siyo kwamba tulikomboa ardhi yetu tu, bali tulimuondoa Amini, tukaweka serikali ya mpito, tukaandaa na kuendesha uchaguzi Uganda, tuka-train polisi na jeshi, na kuondoka kwa heshima zote. hivi hakuna makamanda na wapiganaji wanaopaswa kuenziwa hapa, tuna-list wanasiasa waliofeli tu.

NB:

..ndiyo maana sasa hivi vijana wanamaliza chuo kikuu moja kwa moja wanataka kujiingiza kwenye siasa.

..ukienda mashuleni hatuna watoto wanao-dream kuwa waalimu.

..nadhani kinachoendelea hapa ni matokeo ya propaganda za muda mrefu za wanasiasa kwamba they were doing something for the country, lakini leo hii hamna cha kuonyesha.

JokaKuu,

Naungana na Jasusi kusema kuwa makosa makubwa ya watendaji wengi na wanasiasa yalikuwa ni kushindwa kuimarisha na kulijenga Taifa kwa kuinua viwango vya maisha na mapato ya watu.

Washauri wengi wa Nyerere na wafuasi wake, walikuw ani watu waliokubaliana kila kitu na Mwalimu bila hata kumbishia kwa kumpa data au facts on ground.

Ukirejea kwenye ile thread ya Azimio la Arusha, Bibi Ntilie kalonga wazi kuwa ni vipi kulikuwa na viongozi wafuata upepo au walioimba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na kulisifu Azimio kwa kutokulielewa na hivyo kushindwa kuboresha maisha ya Mtanzania kwa kisingizio cha siasa ya Ujamaa.

Tukirudi kwenye watu mashuhuri ambao si Wanasiasa na waliokuwa na impact katika Taifa, anza na mbeba Mwenge, Nyirenda, njoo Elisha Kavana, Afande Sawaya, Mzee Kisasi, Mwalimu Geofrey Mmari, Bernard Mulokozi, Mbotto wa TFC, Nsekela, Elias Mshiu wa Tanganyika Farmers, Ng'owi wa KNCU, Ole Kambaine, Damas Mbogoro, Kipokola, Dr. Lema wa Muhimbili, Mama Mlama, Kezilahabi, Mbaraka Mwinshehe, Sembuli, Morris Nyunyusa, Yombayomba, Bwana Mianzi, Peter Mayagilo wa Police brass band na wengine wengi katika fani nyingi.
 
Mkuu Icadon,

Heshima mbele bro, duh tuendelee kuweka vitu hapa maana so far tunakula elimu safi na ya bure, Ashante sana mkuu,

Mkuu Jasusi,

Please, acha kupoteza muda wako, maana ukiona bin-adam anapigana na picha zisizosema, basi utajua ni kwa nini tuna matatizo kwenye muungano! Sio kwamba hatujamuona na hiyo crying yake for attention, ila tumemdharau,

Najua kuwa unazo picha nyingi za kumbu kumbu, please weka picha hapa achana na kelele za mlango!

Mkuu Invisible,

Ahsante kwa marekebisho naomba uipitie hii topic mara kwa mara kurekebisha picha na maneno yasiyokuwa sawia kuambatana na hizi picha, za viongozi wetu mashuhuri waliotuwekea msingi wa taifa hili, ambalo some of us we are proud citizens wake.

...Thanx! You have said it all.....!
 
Back
Top Bottom