Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

...mwaka 1965

 
hivi,is there any institution,landmark or any major road in tanzania named after dr louis leakey? kama hakuna basi inasikitisha sana.
 
Hivi kuna mtu anaweza kuniambia MWAKITWANGE yuko wapi?

alikuwa anapatikana sana pale Salamander miaka hiyoooooo

.........jamani mnamuongelea mwakitwange aliyekuwa amepanga nyumba namba 8....tandamti [mission kota]..brazameni koko.....,Hivi bado yupo na yule mwanamke wake mweupe aliyekuwa ATC....??

NASIKIA ile nyumba aliyokuwa anajifanya yake[kumbe amepanga]..imeuzwa na amehamia ukweni???
 
1.
Mkuu Gotee,

Heshima mbele sana, hii ndio iliyokuwa hasa Marquis Kamanyola, yaani walikuwa wanaringa ukienda muziki wao Chinyama, Nguza, na Kiki wao hutokea saa nane usiku, wakiingia tu ngoma ya kwanza ni "chakula chakula kwa bombeee" halafu wanangusha wimbo wa "taifa" then, yaani "Habari zakoooo, nimeshapata yoo, maneno yako nimeshajua yoo!" umenikumbussha sana Odax na Parash, saafi sana bro! kwa kweli ulikuwepo mkuu!

2.
Hiii ilikuwa ni awamu ya pili, unaikumbuka ngoma ya "Mayanga", na 'Huba"?

Ahsante mkuu, kwa kweli nimekukubali kuwa na wewe umo sana!
 
Machifu wa Kingoni waliokamatwa wakati wa vita ya Maji Maji baadaye walinyongwa.

Kumbe huu uhuru wetu kuna walioutolea damu, ili leo tuwe huru! na wengine kutufisadi?

Mungu Awalaze Mahali Pema Mbele Ya Haki!
 


Mkuu, Heshima mbele. Nataka tu kuwa na uhakika. hebu cheki tena kumbukumbu zako. Za kwangu zinaniambia kuwa huyu aliye na zahir Ally ndiye Nana 'Mzuri' Njige na yule mwingine mwenye mwili mkubwa ni Rahma Shalli na kama sikosei sana na miili yao ndivyo ilivyokuwa. Nana Mzuri alikuwa kipotable na Shalli alikuwa amejaa jaa! Hebu cheki tena....
 




Mkuu, teh teh. Nadhani ilikuwa ni hivi...

'Habari zako, habari zako.
Nazipata hapa mjiini,
Umekwisha pata bibi mwingine,
Nasikia Osterbeei.................'


Kile mkuu, kilikuwa kigongo, hadi leo ukikisikia damu inasisimka. sikia:

'mama njoo mama njoo mama njoo uoone,
uchungu wa moyo maudhi natesekaa,
nimeechoka tena kuvumiliaaa,
leo yamezidi ya siku zote,
uchungu mwingi umenipataa,
nitulize moyo sina rahaa,
 

Sawa sawa, tupo pamoja hapo.
 
Mkuu hakuna noma, ukiniwekea mawasiliano kwenye pm by this weekeend nitakuwekea kwenye posta, yaani hizo nyimbo zake zote Salama, Matilda, Magreti na the rest, ahsante mkuu!

asante sana, nitakubip. ngoja nitengeze katalog ya nyimbo ninazotafuta kusudi tupige ndege wengi kwa mpigo iwapo utakuewa nazo
 

Ni kwa sababu ya serikali yetu kutojua jukumu lake kwa raia wake; viongozi wengi wapo wapo tu.
 

Inasikitisha sana. Je kuna tunaloweza kujifunza kutokana na yaliyomkuta Marijani ili turekeibise mfumo wetu kusudi mambo kama haya yasitokee tena?
 
Ford aliyeimbwa na mlimani Parki? Tuliambiwa eti alilipa kusudi Mlimani wamtungie wimbo kwa kutumia jina lake. Je ni kweli?

Mwalimu,

Ford nafikiri ilimbwa na OSS muda mfupi baada ya wanamuziki kadhaa kuihama Sikinde na kwenda OSS, ndio maana wimbo ulifanana na kuonekana kuwa ni wa Sikinde.
 
Ford aliyeimbwa na mlimani Parki? Tuliambiwa eti alilipa kusudi Mlimani wamtungie wimbo kwa kutumia jina lake. Je ni kweli?

Siwezi kushangaa kwa hili, Mr. Ford kama alivyokuwa akijiita alikwua ni kijana wa mjini, mwenye minimum elimu na akafanikiwa kuwa mshikaji wa mkurugenzi wa soko la Kariakoo, kwa hiyo ndoto zake za kuwa baharia siku moja zikabadilika, akaanza kuwa na deals nyingi za sokoni za ujanja ujanja ambazo in the end zilimnufaisha sana yule mkurugenzi,

Lakini na yeye pia zilimpa nafasi ya kutanua, mpaka akajenga nyumba nzuri sana kule Kimara, karibu na Safari Resort, halafu mlinzi wa mlangoni wa Safari Resort, "Mkulu Killer" alikuwa ni ndugu yake, kwa hiyo ndiye aliyemuunganisha na wanamuziki wa OSS au Ndekule, mapaka kumuimbia ule wimbo,

Halafu pia ni tabia ya wabongo wengi sana, kuwalipa wanamuziki ili kama wanavyoita "Wawarushe" au kuwataja na ikibidi kuwaimbia wimbo kabisa, hii tabia inaanzia kwa wanamuziki wa ki-Zaire, maana huko kwao ni kawaida sana na ndio waliotuambukiza na bongo siku hizi.

Otherwise, Ford was a good man na hustler pia, Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi.
 
Jumba la Maajabu huku Zenj leo hii linatimiza miaka 125... Karibuni sana katika sherehe hii..

kwa maelezo ya Jumba hilo bonyeza hapa
 
Pan African

Simba


Yanga




Picha kwa niaba ya issa michuzi-blogspot.com
 

Attachments

  • pan africa.jpg
    48.2 KB · Views: 410
  • simba.jpg
    53.7 KB · Views: 417
  • yanga.jpg
    61.8 KB · Views: 435
  • yanga bingwa.jpg
    83.7 KB · Views: 418
  • yussuf bana.jpg
    71.4 KB · Views: 433
Pan African

Mkuu Kibunango,

Heshima mbele sana na ubarikiwe, lakini hapa kule Michuzi wamekosea, hii ya kwanza ni Yanga mix, kati ya watoto na wakubwa na ilikuwa mechi na timu ya Fluminense, kutoka Brazil uwanja wa taifa, hawa Yanga ni kina:-

1. Waliosimama kutoka kushoto:-

Boi Wickens, Juma Pondamali, Zitto Kiaratu, Adolph Rishad, Abdulrahaman "Mpishi" Juma "Captain", Omar Kapera, Jaffari Abdulrahaman, Hussein Mkweche, Muhidini Fadhili.

2. Waliochuchumaa kutoka kushoto:-

Gordian Mapango, Moshi, Mohamed Yahaya "Tostao", Kitwana Manara "Popat", Leornad Chitete, Kassim Manara, Adam Juma, Muhaji Mukhi.

- Hii ni Yanga kwa sababu, Zitto Kiaratu, Boi Wickens, Abdulrahaman Juma, Muhidin Fadhil, Moshi, Chitete, Adam Juma, hawakuwahi kuichezea Pan African hata mara moja.

Mkuu Kibunango, heshima mbele tena mkuu, na salute!.
 

(Kumradhi Moderators, picha hii imenishinda kuipunguza bila kuathiri ujumbe wake, msaada wenu tafadhali...)
[COMMENT BY Invisible: Tumeifanyia kazi wenyewe! Ahsante]
...'chama' kabambe ya Pazi Basketball team!... ujenzi wa hoteli ya Sheraton pale Gymkhana ulituondolea burudani sie wengine.

R.I.P Ray, Adam "HUNTER" Cassidy, etc...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…