William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
- Thread starter
- #981
1.
Sawa sawa mkuu hapo nimekupata.
2.
1. Unajua huyu Dede sikujua kuwa jina lake lina Kaijage mwishoni, kwa sababu siku zote alikuwa akiishia na Kamchape tu haendi mbele zaidi, unajua Msondo ngoma enzi zile ilikuwa inakubalika sana kama bendi ya watoto wa nyumbani, ndio maana nyimbo zao nyingi tehan zilikuwa zinatoka kwenye ngoma kumtoa mwali kule uswahilini au Zaramoni,
- kwa mfano ile yao ya zamani "....nisingekukimbia mpenzi wangu eeh, tabia za nyumbani kwenu zimenishinda...." hiki kilikuwa kibao maarufu sana huko Goba na uswahilini kwa hiyo kukubalika Msondo Ngoma, ilikuwa ni lazima uonekane mtoto wa nyumbani, nafikri ndio maana Dede alikuwa akiishia na Kamchape, very smart!
- hivi majuzi nimepata single moja ya Sikinde, "....Isaya mrithi wangu..." sikumsikia Bitchuka, ndio maana nikauliza kama yupo bado!
3.
1. Ni kweli hii tabia ya Msondo na majina aliianzisha Mkulu Moshi (RIP), akidhani kuwa anakaribia kuwa kama kina Jibe Mpiyana wa Wenge BCBG, lakini uko right wamezidisha sana kurusha majina.
2. Twahir, ninamkumbuka kwenye ule wimbo wa Kiki, akiwa na OSS yaani "...Mimi msafiri bado niko njiani..." kwa kweli baada tu ya Kiki kutoka OSS nilikosa mapenzi kabisa nao kwa sababu nilimuona Kasheba (RIP) kama mtu aliyependa mno misifa, nikaacha kabisa kuwafuatilia kabisa, ila ninajua at one time alikuwa na bendi moja kwenye hotel za kitalii kule baharini.
Shukrani mkuu, na kwa wakulu wote wengine bado mtandao wangu haujatengemaa, lakini utakapokamilika tu tutaweka picha zaidi hapa, bado tutaendeelea hapa bila noma na picha.
Ahsante wakuu.
Juma Town (RIP) alikuwa mpuliza Saxaphone akishiriana na akina King Michael Enock "Teacher" (RIP) na Joseph (Yusuf) Bernad. Jina la kwanza la Bonnie alikuwa akimaanisha Boniface Kachale ambaye naye alikuwa akipuliza Trampeti akishiriakiana na Marehemu Machaku Salum na Ibrahim Mwinchande.
Sawa sawa mkuu hapo nimekupata.
2.
Bitchuka bado yupo Sikinde tangu alipotoka Ottu Jazz na Mwanyiro. Huko wanaliendeleza libeneke na kina Shabaan Dede Kamchape Kaijage wakishirikiana na vijana wachanga kama Karama Regesu, Eddo Sanga, Abdallah Hemba, Muhina Panduka na Hassan Kunyata katika safu ya uimbaji.
1. Unajua huyu Dede sikujua kuwa jina lake lina Kaijage mwishoni, kwa sababu siku zote alikuwa akiishia na Kamchape tu haendi mbele zaidi, unajua Msondo ngoma enzi zile ilikuwa inakubalika sana kama bendi ya watoto wa nyumbani, ndio maana nyimbo zao nyingi tehan zilikuwa zinatoka kwenye ngoma kumtoa mwali kule uswahilini au Zaramoni,
- kwa mfano ile yao ya zamani "....nisingekukimbia mpenzi wangu eeh, tabia za nyumbani kwenu zimenishinda...." hiki kilikuwa kibao maarufu sana huko Goba na uswahilini kwa hiyo kukubalika Msondo Ngoma, ilikuwa ni lazima uonekane mtoto wa nyumbani, nafikri ndio maana Dede alikuwa akiishia na Kamchape, very smart!
- hivi majuzi nimepata single moja ya Sikinde, "....Isaya mrithi wangu..." sikumsikia Bitchuka, ndio maana nikauliza kama yupo bado!
3.
Mkuu kinachonifurahisha Sikinde ni bendi pekee ambayo bado haijapoteza tyuni yake ya zamani. Msondo Ngoma Music Band wamezidi mno kutajataja majina. Wimbo mmoja wanataja majina mengi kuliko maneno ya wimbo. Hivi yule mpiga saxaphone wa OSS aitwaye Twahile (Twahir) yuko wapi siku hizi. Yule jamaa namvulia kofia kwa aina ya upulizaji saxa. Msikilize kwenye wimbo wa Ziada.