Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Mkuu Kibunango,

Heshima mbele sana na ubarikiwe, lakini hapa kule Michuzi wamekosea, hii ya kwanza ni Yanga mix, kati ya watoto na wakubwa na ilikuwa mechi na timu ya Fluminense, kutoka Brazil uwanja wa taifa, hawa Yanga ni kina:-

1. Waliosimama kutoka kushoto:-

Boi Wickens, Juma Pondamali, Zitto Kiaratu, Adolph Rishad, Abdulrahaman "Mpishi" Juma "Captain", Omar Kapera, Jaffari Abdulrahaman, Hussein Mkweche, Muhidini Fadhili.

2. Waliochuchumaa kutoka kushoto:-

Gordian Mapango, Moshi, Mohamed Yahaya "Tostao", Kitwana Manara "Popat", Leornad Chitete, Kassim Manara, Adam Juma, Muhaji Mukhi.

- Hii ni Yanga kwa sababu, Zitto Kiaratu, Boi Wickens, Abdulrahaman Juma, Muhidin Fadhil, Moshi, Chitete, Adam Juma, hawakuwahi kuichezea Pan African hata mara moja.

Mkuu Kibunango, heshima mbele tena mkuu, na salute!.

yanga na fluminence kama sikosei ilikuwa mechi y kwanza ya zitto kiaratu kuichezea yanga tangu atoke cosmo. nakumbuka sana mechi hiyo kwani siku hiyo game ilimkubali haswa zitto.
 
kwenye trupu la yanga hapo chini namuona "chama" aliyetokea kama si pamba basi toto afrika. huyu mcheza alikuwa akikutana na zamoyoni mogela uwanjani (yanga na simba) ilikuwa hapatoshi nadhani chama alikuwa na tenda ya kuhakikisha mogela hafanyi uharibifu.
 
jamani mimi naomba mwenye picha za kile kikundi cha taarab cha pale kariakoo cha EGYPTIAN aziweke hapa...na nataka sana kujua wale wazee ni wangapi wamebaki na royalties zaozinatunzwa na nani.
 
(Kumradhi Moderators, picha hii imenishinda kuipunguza bila kuathiri ujumbe wake, msaada wenu tafadhali...)

...'chama' kabambe ya Pazi Basketball team!... ujenzi wa hoteli ya Sheraton pale Gymkhana ulituondolea burudani sie wengine.

R.I.P Ray, Adam "HUNTER" Cassidy, etc...

Sahihisho dogo sana: Waliochuchumaa jina ni Menrad Rwabutaza na sio Menrad ruta.....
 
...Twende mbele tukikumbukia ya nyuma, pamoja na mazuri ya ufadhili mfano wa kina;

Jabir Shikamkono baadae Azim Dewji Simba
Kaka -Tukuyu Stars
Naushad- Malindi Zbar
Shafii Bora- Majimaji
mussa Kiluvia baadae Gulamali- Yanga

...'kuwezeshwa', kulipelekea wachezaji wengi kupotelea kwenye anasa...

R.I.P Hamisi Thobias Gagarino, Method Mogella, Ramadhan Lenny,...etc

attachment.php

...'Eddo Boy', Edward Chumila alikuwa Goal getter mkali sana enzi zake ndani ya jezi ya "mnyama mkali", hapo wanaonekana na kina Zamoyoni Mogella na kina Born City wakila maraha ndani ya Club Washirika, miaka hiyo...
 
'Eddo Boy', Edward Chumila alikuwa Goal getter mkali sana enzi zake ndani ya jezi ya "mnyama mkali", hapo wanaonekana na kina Zamoyoni Mogella na kina Born City wakila maraha ndani ya Club Washirika, miaka hiyo...

Hapo nimewaona Chumila, Za-mogella, Shebby B, na Born City aliywakua akimiliki Dsco la YMCA under DJ Kali Kali na DJ Nigger Jay, kabla ya kuondolewa na kupewa Disco Space 1900 ya Sudi na DJ Super Deo,

Na DJ Kali Kali kuhamia RSVP Club!, akishirikina na DJ Seydou na DJ Jerry Kotto.

Ahsante kwa picha mkuu.
 
...Twende mbele tukikumbukia ya nyuma, pamoja na mazuri ya ufadhili mfano wa kina;

Jabir Shikamkono baadae Azim Dewji Simba
Kaka -Tukuyu Stars
Naushad- Malindi Zbar
Shafii Bora- Majimaji
mussa Kiluvia baadae Gulamali- Yanga

...'kuwezeshwa', kulipelekea wachezaji wengi kupotelea kwenye anasa...

R.I.P Hamisi Thobias Gagarino, Method Mogella, Ramadhan Lenny,...etc

View attachment 2523

...'Eddo Boy', Edward Chumila alikuwa Goal getter mkali sana enzi zake ndani ya jezi ya "mnyama mkali", hapo wanaonekana na kina Zamoyoni Mogella na kina Born City wakila maraha ndani ya Club Washirika, miaka hiyo...
Du! Hamis Thobias Gaga 'Gagarino' (RIP)
 
Siwezi kushangaa kwa hili, Mr. Ford kama alivyokuwa akijiita alikwua ni kijana wa mjini, mwenye minimum elimu na akafanikiwa kuwa mshikaji wa mkurugenzi wa soko la Kariakoo, kwa hiyo ndoto zake za kuwa baharia siku moja zikabadilika, akaanza kuwa na deals nyingi za sokoni za ujanja ujanja ambazo in the end zilimnufaisha sana yule mkurugenzi,.

Du! Ule wimbo wa Ford mbona kama ilikuwa anatupiwa madongo. Nakumbuka baadhi ya maneno ya wimbo huo.

Ford eee wewe bado kijana mdogo Ford,
Umeweza kununua gari, na kujenga nyumba hivi sasa,
Pombe ulikuwa hunywi sasa LEVI la kupindikia Ford!

Maisha uliyonayo sasa Ford ... Jihadhari na anasa.....

-----
Tabia ya watu kupendwa kutajwatajwa kwenye Nyimbo ilimtokea puani jamaa mmoja wa Uhamiaji aitwaye Ally Kileo Mwaduga. Ukienda Msondo lazima atajwe, ukienda FM Academia lazima atajwe.

Nasikia siku moja wale waimbaji wa FM Academia waliamua kurekodi wimbo wa kumsifia Ally Kileo kwa kuwasaidia kupata passport. Mkurugenzi wa Uhamiaji akisikiliza redio garini akasikia, "Pedeshee Ally Kileo asante Baba kwa kutuwezesha kupata Passport" Kilichotokea ni jamaa kupewa Uhamisho kwenda Kerando, Wilaya ya Nkasi..... sijamsikia tena siku za karibuni....

Leo nimewaza kuhusu 'Nginde' nikawakumbuka watu wawili. Meddy Kitendawili Mpakanjia na Machaku Salum. Katika 'Friends of Sikinde' waliokuwa na mapenzi ya dhati Meddy alikuwa mmojawapo. Jamaa huyu nakumbuka tangu akiwa fundi gereji ulikuwa humkosi pale DDC Kariakoo. Meddy kwa kutumia fedha zake za mfukoni alifanikisha Sikinde kumchukua mwanamuziki yeyote waliyekuwa wakimtaka. Ndiye aliyezuia Benno asihamie Ndekule na ndiye aliyewarudisha Bitchuka na Mwanyiro Sikinde kwa mara ya mwisho.

Nimemkumbuka Machaku (Chaks). Huyu pamoja na Habib 'Jeff' Mgalusi ndio wanamuziki ambao ni waanzilishi wa Sikinde ambao hawajawahi kuhama. Chaks ametangulia kwenye njia ya Haki, Jeff bado yupo Nginde.

Unawajua "friends of Sikinde' wengine? Miongoni mwao wamo Hamis Kinye na Juma Pondamali 'Mensah'
 
Mkuu Gottee,

Safi sana, Med Mpakanjia ni kijana wa mjini ambaye amekuwa akitajwa sana kwenye nyimbo za bendi mbali mbali, kuotknaa na ukaribu wake na wanamuziki, nafikiri yeye sasa na Papa Musofe, ndio vinara wa kutajwa sana na hizi bendi zetu.

Hivi naomba kuuliza, Machaku kuliwa na wawili au mmoja kwa sababu najua kuan mmoja alikuwa mwanamuziki pia wa Sikinde, kama sikosei alikwua akiitwa Habibu Machaku, au?
 
Pan African
attachment.php

Simba
attachment.php

Yanga
attachment.php

attachment.php

attachment.php

Picha kwa niaba ya issa michuzi-blogspot.com

Picha ya chini kabisa naweza kum recognize Athumani China hapo katikati na mwenye mpira nadhani Zamoyoni Mogella "Golden Boy" kama sikosei.
Na huyo anayeonekana Mkoba wa Yanga ni Salum Kabunda "Ninja" ama?
 
Mkuu hao ni Yusuf Bana wa Yanga, Zamoyoni Mogella wa Simba, kati kati ni Athumani China wa Yanga, na kule mbalii ni Malota Soma wa Simba.
 
FMES said:
Mkuu hao ni Yusuf Bana wa Yanga, Zamoyoni Mogella wa Simba, kati kati ni Athumani China wa Yanga, na kule mbalii ni Malota Soma wa Simba.

..Yussuf Bana, Zamoyoni Mogela, katikati ni MUHIDIN CHEUPE wa Yanga.
 
Mkuu Gottee,
Hivi naomba kuuliza, Machaku kuliwa na wawili au mmoja kwa sababu najua kuan mmoja alikuwa mwanamuziki pia wa Sikinde, kama sikosei alikwua akiitwa Habibu Machaku, au?

Jemedari Mkuu FMES,

Unajua katika ule wimbo ambao Bitchuka anataja majina ya wanamuziki wa Sikinde alikuwa akitaja jina moja moja. Kwa mfano kuna kipande anaimba.
"Bitchuka, Gurumo, Cosmas, Hamis, Mbwana Ibrahim, Habibu Machaku.

Kwa hiyo utaona pale alikuwa akimaanisha, Hassan Bitchuka, Muhidin Gurumo, Cosmas Chidumule, Hamisi Juma Kinyasi, Mbwana, Ibrahim Mwinchande, Habibu 'Jeff' Mgalusi na Machaku Salum 'Chaks'

Kipande kingine Bitchuka anaimba, "Abel, Mulenga, Joseph na Gama, George Kessy, Mwanyiro, Chuma na Kitwana....

Kama unakumbuka Kitwana (RIP) ndio alikuwa mfunga vyombo wao na 'Baunsa' pale mlangoni.

George Kessy ndio alikuwa mpiga Organ wa Sikinde wakishindana wa Waziri Ally aliyekuwa JUWATA! Sikiliza organ yake kwenye zile nyimbo za Selina, Barua kutoka kwa mama namba moja na Kasimu.

Tuko Pamoja.
 
..Yussuf Bana, Zamoyoni Mogela, katikati ni MUHIDIN CHEUPE wa Yanga.

Nafikiri inaweza kuwa Cheupe...Unajuwa miguu ya ke imenikumbushia..Lakini uchezaji wake ulikuwa unafana na China...Ila China yeye alikuwa sharp zaidi na Cheupe alikuwa na yeye ana mbwembwe.
 
Jemedari Mkuu FMES,

Unajua katika ule wimbo ambao Bitchuka anataja majina ya wanamuziki wa Sikinde alikuwa akitaja jina moja moja. Kwa mfano kuna kipande anaimba.
"Bitchuka, Gurumo, Cosmas, Hamis, Mbwana Ibrahim, Habibu Machaku.

Kwa hiyo utaona pale alikuwa akimaanisha, Hassan Bitchuka, Muhidin Gurumo, Cosmas Chidumule, Hamisi Juma Kinyasi, Mbwana, Ibrahim Mwinchande, Habibu 'Jeff' Mgalusi na Machaku Salum 'Chaks'

Kipande kingine Bitchuka anaimba, "Abel, Mulenga, Joseph na Gama, George Kessy, Mwanyiro, Chuma na Kitwana....

Kama unakumbuka Kitwana (RIP) ndio alikuwa mfunga vyombo wao na 'Baunsa' pale mlangoni.

George Kessy ndio alikuwa mpiga Organ wa Sikinde wakishindana wa Waziri Ally aliyekuwa JUWATA! Sikiliza organ yake kwenye zile nyimbo za Selina, Barua kutoka kwa mama namba moja na Kasimu.

Tuko Pamoja.

Sawa sawa mkuu, vipi jina moja pia analitaja kwenye hiyo safu yaani ....bwana iburahimu, born Juma town...." huyu naye alikuwa mpigaji au?

Ni kweli namkubuka Bwana Waziri na Organ Msondo Ngoma, kwenye ile ngoma ya Bitchuka, "......nilikupeleka kwa wakwe zangu...." , mkuu Bitchuka siku hizi yupo wapi? Unajua siku hizi ninawafuatilia wazee wa ngwasuma tu yaani FM Academia, maana nawaona kama wanaendeleza Marquis Kamanyola ingawa kwa mtindo tofauti, kwa sababu to this day bado ninawakumbuka sana Marquis, siku huwa wanapiga karibu sana na kijiji changu Kinyerezi, dakika kama 10 kutoka kwangu kabla hujafika kwenye gereza la Segerea, kuna Bar maarufu inaitwa Pentagone, lakini wamechoka mno wala huwezi amini kuwa ni Marquis kweli, imebakia mfano tu!

Lakini siku hizi ninazimia sana na FM Academia, ya kina Nyoshe El-Sadat, na Mkulu Kitokololo, wananikumbusha sana Mbuya Makonga Adios na Nkurlu Wabangoi, Twanga ninashindwa kuwaelewa na wanaiga mno mpaka wanaharibu, ingawa nina heshima sana na Mkulu wangu Banzanstone ingawa ninapata taabu sana kumuelewa Diof Soko La Mandondo, yaani huyu raper wao, kwa sababu anaingia kwenye nyimbo bila mipangilio na most of the time anaishia kuharibu the flow ya nyimbo zao, wimbo unaonekana wa kiswahili then huyu mkulu anakuja na kuingiza mbwe mbwe zake na kuharibu kabisa,

Otherwise tuko pamoja na heshima juu.
 
Mjomba nahitaji kujua wale EGYPTIAN MUSICAL CLUB waliishia wapi?

Mkuu ninaikumbuka, lakini nafikiri ilijifia kifo cha mende maana ndombolo unajua iliua bendi nyingi sana ambazo zilishindwa kubadilika, hivi unajua siku hizi hata taarabu imeanza kugeuka kuwa na ndombolo kwa ndani yake.
 
Sawa sawa mkuu, vipi jina moja pia analitaja kwenye hiyo safu yaani ....bwana iburahimu, born Juma town...." huyu naye alikuwa mpigaji au?
.

Juma Town (RIP) alikuwa mpuliza Saxaphone akishiriana na akina King Michael Enock "Teacher" (RIP) na Joseph (Yusuf) Bernad. Jina la kwanza la Bonnie alikuwa akimaanisha Boniface Kachale ambaye naye alikuwa akipuliza Trampeti akishiriakiana na Marehemu Machaku Salum na Ibrahim Mwinchande.

Bitchuka bado yupo Sikinde tangu alipotoka Ottu Jazz na Mwanyiro. Huko wanaliendeleza libeneke na kina Shabaan Dede Kamchape Kaijage wakishirikiana na vijana wachanga kama Karama Regesu, Eddo Sanga, Abdallah Hemba, Muhina Panduka na Hassan Kunyata katika safu ya uimbaji.

Mkuu kinachonifurahisha Sikinde ni bendi pekee ambayo bado haijapoteza tyuni yake ya zamani. Msondo Ngoma Music Band wamezidi mno kutajataja majina. Wimbo mmoja wanataja majina mengi kuliko maneno ya wimbo.

Hivi yule mpiga saxaphone wa OSS aitwaye Twahile (Twahir) yuko wapi siku hizi. Yule jamaa namvulia kofia kwa aina ya upulizaji saxa. Msikilize kwenye wimbo wa Ziada.

Aahhh kumbe ni mshabiki wa Wazee Pamba nyepesi, wazee wa Bring bring! Kinachonifurahisha mimi kwa hawa wazee ni kujituma stejini. Wanamuziki wetu wa kibongo wakiwa stejini mawazo yao yanakuwa hayapo labda mpaka wamuone Ally Kileo au Fikiri Madinda au Papa Musofe au Shabaan Didi ndio wanaanza kukazana kutaja majina yao hadi ya wake zao na watoto wao na wajukuu zao.

Heshima mbele tena kwako Mkulu na tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom