Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

1.
Juma Town (RIP) alikuwa mpuliza Saxaphone akishiriana na akina King Michael Enock "Teacher" (RIP) na Joseph (Yusuf) Bernad. Jina la kwanza la Bonnie alikuwa akimaanisha Boniface Kachale ambaye naye alikuwa akipuliza Trampeti akishiriakiana na Marehemu Machaku Salum na Ibrahim Mwinchande.

Sawa sawa mkuu hapo nimekupata.

2.
Bitchuka bado yupo Sikinde tangu alipotoka Ottu Jazz na Mwanyiro. Huko wanaliendeleza libeneke na kina Shabaan Dede Kamchape Kaijage wakishirikiana na vijana wachanga kama Karama Regesu, Eddo Sanga, Abdallah Hemba, Muhina Panduka na Hassan Kunyata katika safu ya uimbaji.

1. Unajua huyu Dede sikujua kuwa jina lake lina Kaijage mwishoni, kwa sababu siku zote alikuwa akiishia na Kamchape tu haendi mbele zaidi, unajua Msondo ngoma enzi zile ilikuwa inakubalika sana kama bendi ya watoto wa nyumbani, ndio maana nyimbo zao nyingi tehan zilikuwa zinatoka kwenye ngoma kumtoa mwali kule uswahilini au Zaramoni,

- kwa mfano ile yao ya zamani "....nisingekukimbia mpenzi wangu eeh, tabia za nyumbani kwenu zimenishinda...." hiki kilikuwa kibao maarufu sana huko Goba na uswahilini kwa hiyo kukubalika Msondo Ngoma, ilikuwa ni lazima uonekane mtoto wa nyumbani, nafikri ndio maana Dede alikuwa akiishia na Kamchape, very smart!

- hivi majuzi nimepata single moja ya Sikinde, "....Isaya mrithi wangu..." sikumsikia Bitchuka, ndio maana nikauliza kama yupo bado!


3.
Mkuu kinachonifurahisha Sikinde ni bendi pekee ambayo bado haijapoteza tyuni yake ya zamani. Msondo Ngoma Music Band wamezidi mno kutajataja majina. Wimbo mmoja wanataja majina mengi kuliko maneno ya wimbo. Hivi yule mpiga saxaphone wa OSS aitwaye Twahile (Twahir) yuko wapi siku hizi. Yule jamaa namvulia kofia kwa aina ya upulizaji saxa. Msikilize kwenye wimbo wa Ziada.

1. Ni kweli hii tabia ya Msondo na majina aliianzisha Mkulu Moshi (RIP), akidhani kuwa anakaribia kuwa kama kina Jibe Mpiyana wa Wenge BCBG, lakini uko right wamezidisha sana kurusha majina.

2. Twahir, ninamkumbuka kwenye ule wimbo wa Kiki, akiwa na OSS yaani "...Mimi msafiri bado niko njiani..." kwa kweli baada tu ya Kiki kutoka OSS nilikosa mapenzi kabisa nao kwa sababu nilimuona Kasheba (RIP) kama mtu aliyependa mno misifa, nikaacha kabisa kuwafuatilia kabisa, ila ninajua at one time alikuwa na bendi moja kwenye hotel za kitalii kule baharini.


Shukrani mkuu, na kwa wakulu wote wengine bado mtandao wangu haujatengemaa, lakini utakapokamilika tu tutaweka picha zaidi hapa, bado tutaendeelea hapa bila noma na picha.

Ahsante wakuu.
 
Pengine tujadili mabadiliko ya usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani... tokea yakisafiri wakati wa usiku hadi sasa yanasafiri mchana, mabadiliko ya idadi ya abiria katika mabasi hayo na mchango wake kwa wafanyabiashara wengi wa Tanzania.

Usalama wa mabasi hayo katika miaka ya 60s- 80s, mabasi yenyewe, majambazi wa kupora mabasi, ubora wa barabara za kwenda mikoani na masuala mengine ya usalama.

Kama kawaida mtililiko wa kumbukumbu hizo adhimu uandane na picha na maelezo yake...
 
...Kuna mambo mengine unaweza ku take for granted, kumbe wakati huo wenzetu ilikuwa Bonge la deal New Arusha Hotel kuwa na light bulb, maji moto, teak dancing floor, etc... 😀

View attachment 2557

...Classic cars garage, Buick, Chrysler,.., duh, we acha tu, hakuna reconditioned ya mjapani hapo...(no offence intended, mwenyewe kamkweche kangu kanatokea huko huko!)

View attachment 2558
 
Tanganyika, 1929...

Benki ilikuapo na nyaraka nyingine muhimu hizi hapa...


View attachment 2559

View attachment 2560

View attachment 2561

...Sasaaaa...hiyo "Ufiome triangle" ndio ipi tena? ...umesoma mkakati wa kuimarisha usafiri kwa treni toka reli ya kati kupitia Moshi, Arusha mpaka Engare-Nairobi? wallaaaaaahi, TRC hebu fufueni hizi njia jamani, mara ya mwisho kwenda kusafiri na gari moshi kwenda Moshi ilikuwa mwaka 1981! sijui weshaiba vyuma 'chakavu'?
 
Yaani hata wakoloni walikuwa na mipango mizuri kuliko hata sisi wenyewe jamani! Mnaonaje tungewaacha wakavuta vuta muda kidogo wakamalizia haya mambo?
 
Kuna mambo mengine unaweza ku take for granted, kumbe wakati huo wenzetu ilikuwa Bonge la deal New Arusha Hotel kuwa na light bulb, maji moto, teak dancing floor, etc

Mkuu Mchongoma, kama kawaida yako umeniacha hoi sana na hii kitu ya Arusha Hotel, yaani siku hizo sanitaion na Hot water ilikuwa big deal mpaka inatangazwa kwenye ad,

Saafi sana na heshima mbele sana.
 

...not so sure, lakini, nadhani nilishaioana hii picha ya kati huko nyuma(?), ngoja nikumbushie tena CHIFU wetu huyu,...


View attachment 2562

Chief Simeon Laiseri posing with British Government officers at the official inauguration of the first leadership of the United Waarusha community on January 14, 1948.

View attachment 2563

...Chief Simeona Laiseri 1979...

View attachment 2564

...Nimeipenda hii "3D" -Map ya Tanganyika enzi hizo, gari moshi kwenye Reli ya kati hiyooooooooooooo...
 
Chief Simeon Laiseri posing with British Government officers at the official inauguration of the first leadership of the United Waarusha community on January 14, 1948.

Huyu naye alikuwa ni Chifu wa huko Moshi tena, mbona sijawahi kumsikia mwenye historia msaaada kidogo!
 
Huyu naye alikuwa ni Chifu wa huko Moshi tena, mbona sijawahi kumsikia mwenye historia msaaada kidogo!

Hapana mkuu, huyu alikuwa chifu wa kabila la "waarusha", hawa wanapatikana Arusha wana lugha na mila zinazokaribiana sana na za wamasai lakini wao ni wakulima na wafugaji, pia huwa hawahami kama wamasai, wame-settle eneo moja.
 
Yaani hata wakoloni walikuwa na mipango mizuri kuliko hata sisi wenyewe jamani! Mnaonaje tungewaacha wakavuta vuta muda kidogo wakamalizia haya mambo?


😀😀😀... ngoja waamke, jiandae kujibiwa na kuulizwa iweje unawapendelea 'wakoloni!'

...labda ndio maana baada ya somo hilo, milango imefunguliwa tena hata kwa kina Barclays Bank ambao nao walikuwapo zama hizo...
 
Yaani hata wakoloni walikuwa na mipango mizuri kuliko hata sisi wenyewe jamani! Mnaonaje tungewaacha wakavuta vuta muda kidogo wakamalizia haya mambo?

Kithuku,
Mipango ya wakoloni ilikuwa si kwa ajili yetu. Nakumbuka pale Mwanza Hotel hata Julius Nyerere hakuruhusiwa kunywa kikombe cha chai mwaka 1952. Sitashangaa kama Arusha Hotel ilikuwa hivyo hivyo wakati wa ukoloni.
 
Hapana mkuu, huyu alikuwa chifu wa kabila la "waarusha", hawa wanapatikana Arusha wana lugha na mila zinazokaribiana sana na za wamasai lakini wao ni wakulima na wafugaji, pia huwa hawahami kama wamasai, wame-settle eneo moja.

Kithukuu si useme ukweli wanaitwa Wamasai Koko..😉
 
Mchongoma,

Hiyo ramani nzuri uliipata wapi? tafuta nyingine bwana uzilete tuzione.

Sasa unaona hiyo Lupa Goldfields na Sekenke? sasa Tangu Naintini Kweusi mzungu alishajua kuwa tuna dhahabu tosha.

Angalia pale jirani na Pangani kuna Power station!

Ari Mpya hawana hata ramani moja au blue print ya maendeleo zaidi ya win win situation!
 
...Wakuu, najiandaa kwenda Bongo kula Eid,

...nawaacha na picha za New Arusha Hotel, mwaka 1929, mjionee Chrysler, na Buicks enzi hizo...😀


View attachment 2573

Kwa Remtulla...Arusha mjini na Bendera ya Tanganyika, 1962

View attachment 2574

natanguliza *****EID NJEMA KWA WOOOTE*****!!!
 
Mkuu Mchongoma, heshima mbele bro yaani ubarikiwe tu maana this is incredible, hizi picha mwihso wa zote.
 
Hii picha ya ya Arusha jengo la Remtula Pirbhai ni classic, imaging 1962 barabara lami safi taa za barabarani mitaa misafi.... halafu mtu akisema bora mkoloni mnakuja juu
 
Back
Top Bottom