Siku ya kwanza ya mazoezi ya Tanzania All Stars inasemekana Gurumo kwa kutumia kipaza sauti alimwambia, "Mwanangu Bitchuka itabidi ukaze uzi kuna Mkulima (Zahir Ally Zoro) katoka Kijijini anaimba kama hana akili nzuri"
Mhhhhh! Tabia Mwanjelwa... namkumbuka kwa ule wimbo wake.... 'Kweli maisha ni safari ndefu.... ambayo haina mwishoooooo.... mwisho wake ni kifo..... Maquiz ilikuwa imekamilika siku zile... nani atawasahau akina Chinyama Chiaza, Mukumbule Lulembo Parash, Mutombo Lufungula Odax, Mbuya Makonga Adios, Mwema Mujanga (Mzee Chekecha) Nguza Mbangu Vicking, Kaumba Kalemba, Nkulu Wabangoi, Ilunga Lubaba, Dekula Vumbi Kahanga (Vumbi, Vumbi, Sendema Sendema Kalasendema), Bobo Sukari, Freditto Utamu (Chini ya Muti, Chini Ya Mwembe) Mtoto Mzuri Assossa na wimbo wake wa Promosheni (Tulipoanza mimi nayeeeee...Jamani Leo ni kama ndoto yuko mikononi mwangu iyoyo iyoyo iyoooo) Kasongo Mpinda Clayton (Nataka kucheka sina mbavu yoooo
. Wa kufa kwa sumu ya Chanicha) Mafumu Bilali Bombenga, Issa Nundu (Kama umenichoka nieleze mpenzi...Nilisimulia sana jina lako mbele ya wenzangu naona yote hayo huyakumbuki) na Baadaye Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa.
Nyimbo kama Tafadhali, Kalubandika, Malokele, Mimi Msafiri, Safari Yetu Mbeya, Mama Kabibi, Haruna, Tusherekee Krismasi, kwenye wimbo huu kuna yale maneno... Ohhh Noele Mama... Noele mama tuimbe sote.....ohhh krismas oyeee....
Wakati huo OSS nako kulikuwa kunatisha, huko walikuwepo akina Twahilee (Twahir), Kimeza Abdallah, Otrish, Ndala Kasheba, Kawelee Mutimwana, Mobale Jumbe, na yule mtunzi wa ule wimbo wa Ziada Kabea Badu... bado nakumbuka baadhi ya maneno ya wimbo huo. "Umenionyesha mazuri toka ndani ya mdomo wako.... bila kuficha nikaaamini ooo dada... kumbe mwenzangu una yako moyooni, niachie mimi nilieee nimekwishazoea".... halafu kwenye kiitikio, "Bibi yangu walimtamani Ziada... oo walimpenda ziada... olele ohhh mama ohhhh, mimi namlia Ziada, walimtamani Ziada" Nyimbo zingine za OSS zilikuwa kama Dunia Msongamano, Mpaka Manga (Ohhh Mpaka Manga, kulala kwa vidonge), Maria Nyerere, Marashi ya Pemba na nyingine nyingi.
Naendelea kumkumbuka Ndala Kasheba na maneno ndani ya nyimbo zake kama "Wakati tulioana mpenzi ukumbuke, Mapatano yetu pale mbele ya Hakimu Bomani, Habari zako nimezipata toka kwa Mshihiri, nasikia umeshapata Bibi mwingine Oyster Bay" na yale "Ashura wazazi wako Sumbawanga" RIP Freddie Ndala Kasheba Supreme.