Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbukumbu zangu siyo nzuri sana lakini wimbo huu wa Niliruka ukuta ulipigwa kati ya mwaka 1974 na 1975 wakati ambapo vijana Vijana Jazz walikuwa wakutumia mtindo wa Kokakoka. Vile vile Kamata Sukuma ulikuwa wimbo mmojawapo uliotolewa kipindi kile kile pamoja na Niliruka ukuta. Kama niko off, tafadhali niwieni radhi.
Najua kuwa Maneti alikuwa mfipa wa Sumbawanga aliyekulia Tanga; ila nadhani alitokea Morogoro ambako ama alikuwa akipiga na Cuban Marimba au Morogoro Jazz au TK Lumpompo ndipo akajiunga na Vijana Jazz. Kuingia kwake Vijana jazz kuliibadilisha kabisa bendi ile kimapigo na kumwondoa John Ondoro aliyekuwa akiingoza bendi hiyo na aliyepiga wimbo uliokuwa maarufu sana kukaribisha kipindi cha wagonjwa kule RTD.
Maneno yako ni kweli mkuu, lakini "Kamata Sukuma" ulikuwa mtindo wa kwanza wa Maneti alipoingia Vijana ni kweli alitokea Morogoro kwa sababu ninakumbuka wimbo wake mwingine wa pili katika hiyo "Kamata Sukuma" aliuimba Kuluguru, wa "Kalulu libweze dizojogolo dyangu" hata ule wimbo wa Bujumbura nao aliuimba kwa lugha hiyo hiyo ya Kiluguru,
Mtiondo wa Koka Koka, alianza alipotoa albamu ya pili, ambayo ilikuwa na wimbo wake maarufu wa "Operetion Maduka", otherwise mengine yote yako sawa na heshima mbele mkuuu.
son-of-alaska said:wakubwa,nakumbuka miaka ya nyuma kidogo,niliona katika magazine either Africa now au africa events, picha mbili za waanzilishi wa TANU.if my memory haijakosea the person in question was KASSELA BANTU (i stand to be corrected).kassela bantu was a founding member of tanu lakini katika hii picha hakuwepo.years later picha hiyo hiyo resurfaced,kassela bantu akiwemo,in other words hii picha mpya was doctored.mjadala ulikuwa who done it,TANU au YEYE,ANYONE REMEMBERS THIS?
Mkuu Jasusi,Na. Mohammed Said
Mwaka wa 1951 wakati Dossa na wenzake wapo katika juhudi za kuipa uhai mpya TAA Dossa aliandikiwa barua na V.M. Nazerali aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria akimuomba Dossa aunge mkono juhudi zake na za Ivor Byaldon na Brig. Scupham za kutaka kuunda chama cha siasa kitachowashirikisha watu wa rangi zote. Bayldon na Brig. Scupham walikuwa kama alivyokuwa Nazerali, wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.
Wanasiasa wengine walioombwa kuunga mkono juhudi hizi walikuwa Chifu Kidaha Makwaia, Liwali Yustino Mponda wa Newala, Dr. Joseph Mutahangarwa, Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Chifu Thomas Marealle wa Marangu, Chifu Adam Sapi Mkwawa, Chifu Harun Msabila Lugusha, Dr. William Mwanjisi, Abdulkarim Karimjee, Dr. Vedas Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, H.K.Viran, Stephen Mhando, Ally Sykes na Abdulwahid Sykes. Dossa na wenzake waliikataa ghilba hii kwa kuwa lengo lao lilikuwa ni kuanzisha chama cha siasa cha Waafrika wa Tanganyika kwa minajili ya kudai uhuru.
Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 kama mwalimu wa shule ya St. Francis' College, Pugu hakuna mtu aliyekuwa anamjua au kupata kusikia habari zake katika ulingo wa siasa. Kassela Bantu ambaye alikuwa akijuana na Nyerere kwa siku nyingi alimchukua Nyerere kwa Abdulwahid Sykes kumtambulisha. Wakati ule Abdulwahid alikuwa Rais wa TAA. Nyerere mara moja akajiunga na baraza la siasa lililokuwa likifanyika Mtaa wa Mbaruku nyumbani kwa Dossa. Ikawa kila Jumapili Nyerere anakuja kutoka Pugu kuja kumtembelea Dossa.
Ilikuwa katika baraza hii ndipo Nyerere alipokutana na wanasiasa wengi wa wakati ule kama Ramadhani Mashado Plantan aliyekuwa anamiliki gazeti lililokuwa likijulikana kama Zuhra, John Rupia, Dunstan Omari, Zuberi Mtemvu na wanasiasa wengine. Fikra za Nyerere za kudai uhuru zilisikika kwa mara ya kwanza kupitia kalamu ya Mashado Plantan na gazeti lake la Zuhra lililokuwa likitoka kila siku ya Ijumaa. Fikra za Nyerere ziliingiza msisimko mpya katika baraza lile na haukuchukua muda mwaka 1953 uongozi wa ndani ukampendekeza agombee urais wa TAA.
Dossa anasema ingawa wao kwa kuwa karibu na Nyerere walikuwa wamekiona kipaji chake cha uongozi, wanachama wengi hawakumkubali mara moja na ndiyo maana katika uchaguzi wa TAA uliofanyika Arnautouglo Hall tarehe 17 Aprili, 1953 kati ya Abdulwahid aliyekuwa Rais na Nyerere aliyekuwa anagombea dhidi yake, Nyerere alishinda uchaguzi ule kwa taabu sana. Haukupita muda chama kikaanza kuzorota na mwisho kikafa. Dossa anakumbuka kuwa yeye alikuwa anawapitia viongozi kwenda kwenye mkutano. Akipiga honi ili mtu atoke waende mkutanoni kiongozi alimtuma mkewe atoke nje na aseme kuwa hakuwepo nyumbani.
Dossa anasema ilikuwa baada ya kushauriana na Abdulwahid, Makamu Rais wa TAA ndipo lilipokuja wazo kuwa ni lazima wapate nguvu ya wazee wa Dar es Salaam ili kukifufua chama.Hivi ndivyo TAA katika miaka ya mwisho ya uhai wake ilipokuja kupata kuungwa mkono na wazee wa Dar es Salaam na kupelekea kuundwa kwa Baraza la Wazee wa TANU mwaka 1955 chini ya mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir. Nyerere amepata kusema kuwa alikuwa Dossa ndiye aliyemfahamisha aache kuvaa kaptula kwa kuwa sasa atakuwa akitoka mbele ya watu wazima na hiyo si adabu nzuri.
Dossa alikuwa kati ya wale wazalendo watano, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, John Rupia na Julius Nyerere waliokutana ndani ya ofisi ya TAA new Street (sasa Lumumba Street) katika miezi ya mwisho ya 1953 na kwa pamoja wakapitisha azimio la siri la kuibadili TAA kuwa chama cha wazi cha siasa na kukipa chama hicho jukumu la kuiongoza Tanganyika katika kudai uhuru wake. Hili ndilo lililokuwa azimio la kwanza la busara katika historia ya Tanganyika. Azimio la pili la busara ni lile la Tabora la mwaka 1958.
Tarehe 7 Julai, 1954 wazalendo hawa wafuatao wakakutana Dar es Salaam kubadili Katiba ya TAA ili kuanzisha chama cha TANU: Dossa Aziz, Abdulwahid na Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia, Julius Nyerere, C.O. Millinga,Germano Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo; Abubakar Ilanga, L.M.Bugohe, Saadan Abdu Kandoro, S.M. Kitwana na L.M. Makaranga. Dossa Aziz kadi yake ya TANU ni namba 4 iliyotolewa na kusainiwa na Ally Sykes.
Haukupita muda mrefu TANU ikampeleka Nyerere Umoja wa Mataifa. Tarehe 17 Februari, 1955 Nyerere aliondoka Dar es Salaam na kwenda New York kuhutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na ndani ya mkoba wake hakuwa na hotuba nyingine ila yale mapendekezo aliyopewa Gavana Edward Twinning mwaka wa 1950 na uongozi wa TAA.Nyerere aliporudi nchini alikuta umati mkubwa wa wananchi unamsubiri uwanja wa ndege. Haikuwezekana kwake kutoka nje ya uwanja jinsi umati wa watu ulivyojazana kumlaki.. Walinzi wa kikoloni walimruhusu Dossa aingize gari yake hadi chini ya mlango wa ndege. Nyerere akashuka na kupokelewa na swahiba wake Dossa na akaingia ndani ya gari la Dossa.
Mkuu Jasusi,
Heshima mbele, hii saafi sana unajua mkuu nilikuwa ninapita pita huko masehemu ninakuta kazi zako nzito sana kuhusu Mwalimu na siasa yetu bongo kwa ujumla, ukwieza mkuu tumwagie hapa naona uliziandika zamani kidogo.
Heshima mbele!
Huwa inatia uchungu sana kuona mambo yote mazuri tuliyokuwa nayo zamani sasa hivi ni historia. Taa za barabarani (street lights), mitaa iliyopangiliwa vizuri, barabara nzuri za mitaani, pale Chuo Kikuu Mlimani palikuwa kama peponi, wanafunzi walisoma kwa raha sana! Leo hii ukimwambia mwanafunzi wa UDSM kwamba pale Cafeteria kulikuwa na viji-fridge vinavyotoa maziwa 24/7 hatakuamini kabisa....kwani yeye hata maji ya kunywa sasa hivi ananunua!
Ila hayo mabasi yameniumiza roho sana! Ukiviona vipanya vya Dar vilivyojichokea hutaamini kama Dar pamewahi kuwa na usafiri mzuri kiasi hicho! Something must be wrong somewhere for sure!
Nimshukuru FMES kwa jinsi anavyoi-direct thread hii. Waanzishaji wengine wa thread muige mfano huu. Hii imetulia na haijayumba hata kidogo, matusi, kejeli, dharau, umbea, udaku havina nafasi hata kidogo.
Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari. Alisimamia mipango mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni. Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi. Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake. Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.
Slavery in Malawi
The Atlantic slave-trade may have ended 200 years ago, but in Malawi it went on for another 90 years, finally ending when the stockade at Karonga was destroyed in 1895. 19,000 slaves from Nyasa region passed through Zanzibar Custom House alone, though most slaves from Malawi were shipped from Mozambican ports. Thousands more were killed or died in the slave gangs and Livingstoke thought that probably not one-tenth of those captured survived to become slaves.
Petro Kilekwa was captured near Lake Bangweulu in Zambia in about 1870 and marched 1,000 miles to Samama on the southern shore of Lake Malawi. There he was made to sleep alongside his owner who had gone down with smallpox, because it was unfitting for a slave to survive his master. His owner died but Petro survived. He was twice resold, and finally marched down to the Portuguese coast and taken by a dhow to the Persian Gulf. There he was freed by a British naval vessel, on which he visited Baghdad and later, as the admiral's cabin boy sailed on HMS Bacchante for Bombay, Colombo, and Madagascar.
At Zanzibar Petro was put ashore into a UMCA school for released slaves where he ended as a teacher and then made his way back to Malawi. He pioneered the work in the hills at Ntchisi as teacher, deacon and priest. This is now the strongest archdeaconry in Malawi and this year is celebrating the centenary of its foundation by Petro.
In 1929 as priest-in-charge of Nkope he became the first African to head a mainland mission. He retired in 1951.