Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Ngoja nitumie TANO bora zangu vizuri hapa.

(3) Kwa waliokuwa wafuasi wa Marquiz na Double "O," je mnafahamu huyu dada ni nani na alikuwa akifanya nini kwenye picha hii, na sasa hivi yuko wapi?
attachment.php

Ili kupata majibu ya maswali yenu, nipeni mji.

Baada ya dada za Frank Humplick kuacha kujishughulisha na mambo ya muziki mwanzoni mwa miaka ya sitini, wanawake wa kitanzania hawakujishughulisha tena na sanaa hiyo kwa muda wa takriban muongo mmoja hadi mwishoni mwa miaka sabini ambapo mwanadada Tabia Mwanjelwa aliibuka kama mmojawapo wa waimbaji katika safu ya Marquis. Kuanzia Tabia ajiunge na muziki Tanzania, wanawake wa kitanzania wameendelea kuwa msitari wa mbele katika fani hiyo kiasi kuwa hivi sasa wanawake wanashikilia chati za juu sana. Inawezekana kabisa kusema kuwa muasisi wa muziki kwa wanawake wa Kitanzania ni huyu Tabia Mwanjelwa. Katika picha hiyo alikuwa akiimba na bendi ya Orchestra Double 'O' iliyokuwa imeanzishwa na Kivumbi Mwanza Mpango King Kikii, baada ya kuhama Marquis alikotamba na kibao chake cha 'Safari Sio Kifo'.

Tabia alitoweka jijini Dar es Salaam mwaka 1987 akavumishiwa kuwa amefariki kwa Ukimwi; ninakumbuka kukutana na jamaa fulani kwenye baa moja pale Kinondoni akidai kwa nguvu kabisa kuwa alikuwa ametoka kwenye mazishi ya Tabia Mwanjelwa, na alikuwa ameshiriki kwa mkono wake kumzika. Baada ya uvumi kusambaa kwa nguvu, ndipo dada yake akaukanusha na kusema Tabia alikuwa mzima ila yuko Ulaya matembezi. Kuanzia wakati huo Tabia hajarudi Tanzania na kwa sasa hivi anapiga solo na inasemekana ameolewa huko Ujerumani mjini Saabrucken. Website yake ni TabiasSite
 
Ngoja nitumie TANO bora zangu vizuri hapa.

(4) Kwa waliokuwa wafuasi wa kandanda, je mnamfahamu huyu mchezaji mwenye sharafa ni nani na kwenye picha hii alikuwa akifanya nini na sasa hivi yuko wapi
?
attachment.php

(5) Kwa waliokuwa wafuasi wa muziki tena, na mnakifahamu kikosi hiki kilikuwa kinajulikanaje na leo hii wapigaji wake wako wapi?
2474d1221765101-tukumbuke-zamani-historia-ya-taifa-letu-katika-picha-tanzanites.jpg

Ili kupata majibu ya maswali yenu, nipeni mji.
(4) mmh huyo naamini ni haidari abeid alikuwa mchezaji babu kubwa sana wa simba

(5) hapo waliosimama kutoka wapili kulia nawaona george kapinga, amato kapinga, john mhina,abraham kapinga, na mpiga congas (mwisho kushoto) ambaye jina lake limenitoka lakini mkuu huyu alisoma azania kama sikosei. wengine naona majina yamenipita pembeni
 
Last edited:
Ngoja nitumie TANO bora zangu vizuri hapa.

(4) Kwa waliokuwa wafuasi wa kandanda, je mnamfahamu huyu mchezaji mwenye sharafa ni nani na kwenye picha hii alikuwa akifanya nini na sasa hivi yuko wapi
?
attachment.php

Ili kupata majibu ya maswali yenu, nipeni mji.

Baada ya mabadiliko katika mfumo wa kandanda Afrika ya Mashariki ambapo kombe la Gossage lilibadilishwa na kuwa kombe la Challenge likishindaniwa na timu za Taifa za Kenya, Uganda, Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar (je tulikuwa tunapendelewa kwa kuwa na wawakilishi wawili au Zanzibar ni nchi?), lilianzisha pia kombe la kushindaniwa na vilabu bingwa vya nchi hizo mwaka 1974. Mwaka huo kombe hilo lilinyakuliwa na Simba ya msimbazi. Katika picha hii, Haidari Abeid "Muchacho" anapokea kombe la ubingwa wa Afrika ya Mashariki kutoka kwa Mheshimiwa Joseph James Mungai, ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Kilimo na pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Haidari atakumbukwa sana na wana Yanga kwani ndiye aliyewatundika bao liliwakosesha ubingwa wa mwaka 1973 na hivyo kukosa nafasi ya kuwa wawakilishi wetu wa kwanza kwenye kombe la Ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Kutokana na ushindi huo wa mwaka 1973, Simba ilijipatia nafasi ya kuwa timu ya kwanza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Baada ya kufarakana na Simba, katikati ya mwaka 1975, haidari aliondoka Simba na kuanzisha timu yake ya Red Devils au Shetani Wekundu. Ingawa timu hii ilianza kwa kasi vile vile kama wenzao wa Pan, nayo iliishia kwa kasi sana.

Kwa sasa hivi sielewi mahala alipo bwana Muchacho ingawa kulikuwa na tetesi mwishoni mwa miaka ya sabini kuwa alikwenda uarabuni kucheza soka la kulipwa. Haidari alikuwa mzaliwa wa Shinyanga na bado kuna ndugu zake kule Shinyanga, huenda alisharudi yuko pamoja na ndugu zake huko Shy au anafanya biashara hapo Dar.
 
Mwaka 1987, kampuni ya Film Tanzania iliwaunganisha wapigaji mziki maarufu kutoa wimbo kwa ajili ya kurekodiwa na kampuni hiyo. Kikosi hicho kilijulikana kama Tanzania All Stars. Waliopo pichani
kutoka kulia ni Muhidin Maalim Gurumo (aliyekuwa JUWATA-Msondo), Max Bushoke (aliyekuwa DDC Mlimani Park-Sikinde), Marijani Rajab (Jabari- aliyekuwa (Dar International, Super Bomboka), Melisa na Zahir Ally (waliokuwa JKT- Kimulimuli), Fresh Jumbe (aliyekuwa Dar International, Super Bomboka), Nana Njige (aliyekuwa Vijana Jazz- Pambamoto Awamu ya Pili), Mabruki (aliyekuwa Mwenge Jazz, Panselepa) na Hamisi (aliyekuwa JKT, Kimbunga). Aliyeko nyuma kulia DJ Seydou.

...naukumbukia wimbo ule "usipowajibika ole wako, utakumbwa na fagio la chuma!"
 
Mkuu Kichuguu,

1. Kofia chini bro, damn! hapo nimewaona The Barkeys, enzi hizo tulikuwa tunawaita mabitozi wa Ukonga, nimeuona Mkulu Castro, The Muhinas, Mkulu Baruani, longtime sana!

2. Halafu finally, umemleta Mkulu Marijani Rajabu, jabali la muziki, aka Mwana Manyema, ninakumbuka siku moja pale DDC nilimuona akiimba wimbo wa "Salamaaa", I mean ungedhani jengo linataka kuanguka kwa mawimbi ya sauti yake, ninawakumbuka washirki wake kina Davis Musa, na Chris Kazinduki wakiwa na Safari Trippers,

Mungu amuweke mahali pema peponi, Mkuu Mkandara hebu ukiomuna Mkulu Jagan huko mkubushie Marijani maana yeye siku zote ndiye aliyekuwa akituimbia nyimbo zake darasani kule Primary school, hasa nyimbo za "Mateso Mingi na Mateso" na "Heko Hayati Karume",

Marijani, alikuwa akimpenda sana Kabasele ya mpanya, yaani Pepe Kale enzi hizo akiwa na Emperio Bakuba, siku zote Marijani katika uimbaji wake hasa akiwa na Safari Trippers, alijaribu sana kumuiga Pepe lakini binafsi alikwua na kipaji kikubwa sana cha sauti saafi sana, kutoka Safari Trippers na mtindo wa sokomoko aliihamia Dar International na mtindo wa Super Bomboka, baadaye mambo hayakumuendea vizuri na moja ya sababu inaaminika kuwa ni pamoja na kuwa mgumu sana kushirkiana na wanamuziki wenziwe, matokeo yake wapigaji wengi maarufu hawakutaka kupiga naye,

Mwishoni alifkia kuwa na hali mbaya sana kimaisha, ndipo ikabidi kwa shingo upande ajiunge na Mwenge Jazz, iliyokuwa bendi ya JWTZ mpaka alipofikia kuitwa kwenye haki.

Mungu Amuweke Mahali Pema huko Mbele ya Haki!
 
Aisee umenikumbusha wimbo huu ambao kwa bahati mbaya hauko hata kwenye makusanyo yangu. Katika wimbo ule kweli Marijani alitamba sana na sauti yake
 
wow!!!!

kumbukumbu safi sana,...! naruhusiwa kutoa majibu kwa kuigilizia mwalimu?... nimekuja na mlungula wangu huu .hapa chini..😀

katika picha zote imenifurahisha hiyo ya Tanzania All stars, kina Chongo, Jabali,...

mbona "mlungula" wako siuoni mzee?
 
Marijani, alikuwa akimpenda sana Kabasele ya mpanya, yaani Pepe Kale enzi hizo akiwa na Emperio Bakuba, siku zote Marijani katika uimbaji wake hasa akiwa na Safari Trippers, alijaribu sana kumuiga Pepe lakini binafsi alikwua na kipaji kikubwa sana cha sauti saafi sana, kutoka Safari Trippers na mtindo wa sokomoko aliihamia Dar International na mtindo wa Super Bomboka, baadaye .............

Kabla Dar International haijachukua mtindo wa Super Bomboka, ilikuwa na mtindo wa aina nyingine uliodumu muda mfupi sana. Binafsi siukumbuki ila wenye kumbukumbu hawatashindwa kuuleta. Super Bomboka ni mtindo uliobuniwa na Marijani baada ya wapigaji mahiri wote kuondoka na kwenda kuunda Mlimani Park (kabla haijawa DDC Mlimani park). Nakumbuka wakati ule
tuliambiwa kuwa walishindana na Marijani kwa kumtaka abadilishe sauti yake ili muziki wao usiwe kama wa Safari Trippers
 
2474d1221765101-tukumbuke-zamani-historia

Barkeys,miaka ya themanini wanapiga Mount Meru Hotel....

Waliosimama toka kushoto,Kizibo,Abraham,John Mhina(Kidevu),Amato,George(G) na Yona.Waliochuchumaa,Pepe na Sticks
 
Aisee umenikumbusha wimbo huu ambao kwa bahati mbaya hauko hata kwenye makusanyo yangu. Katika wimbo ule kweli Marijani alitamba sana na sauti yake

Mkuu hakuna noma, ukiniwekea mawasiliano kwenye pm by this weekeend nitakuwekea kwenye posta, yaani hizo nyimbo zake zote Salama, Matilda, Magreti na the rest, ahsante mkuu!
 
Twende mbele turudi nyuma, zamani jamani ndio kulikua kuna muziki...yani unapata kitu mpaka roho inasuuzika...na ukitaka ku prove hilo..angalia tu nyimbo nyingi za zamani mpaka sasa ivi zikipigwa bado zina kugusa na unapata hamu ya kuzisikiliza tena...nitofauti kabisa na nyimbo za hapa siku za nyuma kidogo..ambazo husikika mwaka mmoja tu inazimika na kufa kabisa..hata ukiisikiliza unaona haina kitu cha maana....i do beleave kwamba a quality thing last longer....sijui zamani walikua wanatumia vyombo gani vya muziki?????? au wanamuziki wa sasa ivi wamevamia fani?????????? Maana hainiingii akilini kua wimbo wa mwaka 70...na vyombo vilevile vya zamani unakuja kurudiwa mwaka 2000 na vyombo vya kisasa kabisa lakini unakosa ile ladha kamili ya muziki...wakati ningetegemea kuwa huu uliorudiwa kwa nyakati hizi ndio ungekua mzuri zaidi sababu umerokodiwa kwenye studio za kisasa na vyombo vya kisasa kabisa......... Mimi nilidhani ni kwenye miundo mbinu tu na maendeleo kijamii ndio tuna rudi nyuma kumbe na muziki pia??? lol!!!
 
...babu wa watu yuko wodi 10 mwaisela anasota kwa maumivu ya mguu, na ukiacha familia yake ni watu wachache wanamtembelea mzee wetu huyu ambaye sifa za kazi yake haina mfano na anafananishwa na mashujaa wengine kama kina mzee makongoro, morris nyunyusa na wengineo wa aina hiyo. chozi lilinitoka nilipomtembelea na kumkuta mkiwa pale kitandani, na ukizingatia haoni sawasawa ndio basi tena. alizaliwa mwaka 1922 na kujiunga na polisi mara tu baada ya vita kuu ya pili ya dunia

View attachment 2484

Kwa wale tuliokuwa washabiki wa Police Brass band kila siku za maadhimisho ya uhuru, mashujaa na muungano, siwezi kumsahau mzee huyu ambaye alilitumikia taifa kwa moyo wote katika kipindi chote cha Uongozi wake katika Brass band na mbwembwe zake nyingi akiwa anaongoza gwaride enzi hizooo...

ulifariki ukiwa mpweke ukiwa na familia na marafiki wa karibu tu, lakini ulituvutia wengi, na kamwe historia haitawasahau wewe pamoja na Father Kanuti Mzuwanda wa Brass Band ya Morogoro ambayo ni chimbuko la wanamuziki wengi sana Tanzania, wakiwemo familia ya kina Uvuruge...

Mwenyezi Mungu awalaze pema peponi mzee Justin Dotto Mayagilo, pamoja na fr Kanuti Mzuwanda.
Amen.
 
Mwaka 1987, kampuni ya Film Tanzania iliwaunganisha wapigaji mziki maarufu kutoa wimbo kwa ajili ya kurekodiwa na kampuni hiyo. Kikosi hicho kilijulikana kama Tanzania All Stars. Waliopo pichani
kutoka kulia ni Muhidin Maalim Gurumo (aliyekuwa JUWATA-Msondo), Max Bushoke (aliyekuwa DDC Mlimani Park-Sikinde), Marijani Rajab (Jabari- aliyekuwa (Dar International, Super Bomboka), Melisa na Zahir Ally (waliokuwa JKT- Kimulimuli), Fresh Jumbe (aliyekuwa Dar International, Super Bomboka), Nana Njige (aliyekuwa Vijana Jazz- Pambamoto Awamu ya Pili), Mabruki (aliyekuwa Mwenge Jazz, Panselepa) na Hamisi (aliyekuwa JKT, Kimbunga). Aliyeko nyuma kulia DJ Seydou.

Kichuguu nadhani unaizungumzia Tanzania Film Company....Moja ya masharika ambayo nilisikitika sana Serikali yalipo yasaliti....sasa ivi angalia jamii inavyolia na maadili mabovu ya watoto na wadogo zetu..yote hayo ni kutokua na udhibiti wa filamu zinazoingia nchini...kila kitu ruksa..!!!!!
 
Kwa kweli thread hii imezidi kunifurahisha...na nachukua fursa hii kuipongeza thread hii kwa kufikisha posts 1,000...ilianza kimasihara lakini sasa naona ndio itakua ''The father of all Posts''....na najipongeza mimi mwenyewe pia kwa kuweka post ya 1,000..... god bless this Thread..tuzidi kujifunza mengi tuliyokua hatuyafahamu.... who Knows??...............
 
Mkuu Kichuguu,

1. Kofia chini bro, damn! hapo nimewaona The Barkeys, enzi hizo tulikuwa tunawaita mabitozi wa Ukonga, nimeuona Mkulu Castro, The Muhinas, Mkulu Baruani, longtime sana!

2. Halafu finally, umemleta Mkulu Marijani Rajabu, jabali la muziki, aka Mwana Manyema, ninakumbuka siku moja pale DDC nilimuona akiimba wimbo wa "Salamaaa", I mean ungedhani jengo linataka kuanguka kwa mawimbi ya sauti yake, ninawakumbuka washirki wake kina Davis Musa, na Chris Kazinduki wakiwa na Safari Trippers,

Mungu amuweke mahali pema peponi, Mkuu Mkandara hebu ukiomuna Mkulu Jagan huko mkubushie Marijani maana yeye siku zote ndiye aliyekuwa akituimbia nyimbo zake darasani kule Primary school, hasa nyimbo za "Mateso Mingi na Mateso" na "Heko Hayati Karume",

Marijani, alikuwa akimpenda sana Kabasele ya mpanya, yaani Pepe Kale enzi hizo akiwa na Emperio Bakuba, siku zote Marijani katika uimbaji wake hasa akiwa na Safari Trippers, alijaribu sana kumuiga Pepe lakini binafsi alikwua na kipaji kikubwa sana cha sauti saafi sana, kutoka Safari Trippers na mtindo wa sokomoko aliihamia Dar International na mtindo wa Super Bomboka, baadaye mambo hayakumuendea vizuri na moja ya sababu inaaminika kuwa ni pamoja na kuwa mgumu sana kushirkiana na wanamuziki wenziwe, matokeo yake wapigaji wengi maarufu hawakutaka kupiga naye,

Mwishoni alifkia kuwa na hali mbaya sana kimaisha, ndipo ikabidi kwa shingo upande ajiunge na Mwenge Jazz, iliyokuwa bendi ya JWTZ mpaka alipofikia kuitwa kwenye haki.
Mungu Amuweke Mahali Pema huko Mbele ya Haki!

Ni kweli kabisa, Mkuu. Na kabla ama baada ya kujiunga na Mwenge nadhani alijaribu kujipanga tena na akina George Kifunda na kuanzisha bendi ya AfriCulture na mtindo wa 'Mahepe Ngoma ya Wajanja Wajinga Hawaoni Ndani' ambayo hata hivyo haikuweza hata kurekodi nyimbo RTD. Nakumbuka Siku za mwisho alifungua duka pale nyumbani kwake Kariakoo na akawa anauza kanda za muziki za nyimbo zake na za bendi nyingine. Kwa mtu aliyepata kulitikisa Tanzania kwa midundo yake, hali yake haikuwa nzuri sana kimaisha.
 
Siku ya kwanza ya mazoezi ya Tanzania All Stars inasemekana Gurumo kwa kutumia kipaza sauti alimwambia, "Mwanangu Bitchuka itabidi ukaze uzi kuna Mkulima (Zahir Ally Zoro) katoka Kijijini anaimba kama hana akili nzuri"

Mhhhhh! Tabia Mwanjelwa... namkumbuka kwa ule wimbo wake.... 'Kweli maisha ni safari ndefu.... ambayo haina mwishoooooo.... mwisho wake ni kifo..... Maquiz ilikuwa imekamilika siku zile... nani atawasahau akina Chinyama Chiaza, Mukumbule Lulembo Parash, Mutombo Lufungula Odax, Mbuya Makonga Adios, Mwema Mujanga (Mzee Chekecha) Nguza Mbangu Vicking, Kaumba Kalemba, Nkulu Wabangoi, Ilunga Lubaba, Dekula Vumbi Kahanga (Vumbi, Vumbi, Sendema Sendema Kalasendema), Bobo Sukari, Freditto Utamu (Chini ya Muti, Chini Ya Mwembe) Mtoto Mzuri Assossa na wimbo wake wa Promosheni (Tulipoanza mimi nayeeeee...Jamani Leo ni kama ndoto yuko mikononi mwangu iyoyo iyoyo iyoooo) Kasongo Mpinda Clayton (Nataka kucheka sina mbavu yoooo…. Wa kufa kwa sumu ya Chanicha) Mafumu Bilali Bombenga, Issa Nundu (Kama umenichoka nieleze mpenzi...Nilisimulia sana jina lako mbele ya wenzangu naona yote hayo huyakumbuki) na Baadaye Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa.

Nyimbo kama Tafadhali, Kalubandika, Malokele, Mimi Msafiri, Safari Yetu Mbeya, Mama Kabibi, Haruna, Tusherekee Krismasi, kwenye wimbo huu kuna yale maneno... Ohhh Noele Mama... Noele mama tuimbe sote.....ohhh krismas oyeee....

Wakati huo OSS nako kulikuwa kunatisha, huko walikuwepo akina Twahilee (Twahir), Kimeza Abdallah, Otrish, Ndala Kasheba, Kawelee Mutimwana, Mobale Jumbe, na yule mtunzi wa ule wimbo wa Ziada Kabea Badu... bado nakumbuka baadhi ya maneno ya wimbo huo. "Umenionyesha mazuri toka ndani ya mdomo wako.... bila kuficha nikaaamini ooo dada... kumbe mwenzangu una yako moyooni, niachie mimi nilieee nimekwishazoea".... halafu kwenye kiitikio, "Bibi yangu walimtamani Ziada... oo walimpenda ziada... olele ohhh mama ohhhh, mimi namlia Ziada, walimtamani Ziada" Nyimbo zingine za OSS zilikuwa kama Dunia Msongamano, Mpaka Manga (Ohhh Mpaka Manga, kulala kwa vidonge), Maria Nyerere, Marashi ya Pemba na nyingine nyingi.

Naendelea kumkumbuka Ndala Kasheba na maneno ndani ya nyimbo zake kama "Wakati tulioana mpenzi ukumbuke, Mapatano yetu pale mbele ya Hakimu Bomani, Habari zako nimezipata toka kwa Mshihiri, nasikia umeshapata Bibi mwingine Oyster Bay" na yale "Ashura wazazi wako Sumbawanga" RIP Freddie Ndala Kasheba Supreme.

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • kashebamakutistudio01.jpg
    kashebamakutistudio01.jpg
    18.6 KB · Views: 302
  • ndala.bmp
    ndala.bmp
    441.1 KB · Views: 290
  • Assosa.bmp
    Assosa.bmp
    216.7 KB · Views: 289
  • kingkiki01-01.jpg
    kingkiki01-01.jpg
    10.6 KB · Views: 288
Hivi kuna mtu anaweza kuniambia MWAKITWANGE yuko wapi?

alikuwa anapatikana sana pale Salamander miaka hiyoooooo
 
Machifu wa Kingoni waliokamatwa wakati wa vita ya Maji Maji baadaye walinyongwa.

africa-maji-maji.jpg

Ndanda Miaka hiyooooo

Ndanda.jpg

Ndanda siku hizi (miaka 100 baadaye)

abbeyview.jpg
 
Back
Top Bottom