Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

Sisi tuliohitimu 1985 tuchangie wapi hapa maana Chuo Kikuu Mlimani na Muhimbili jumla tulikuwa 2320 kwa miaka yote! Nyinyi mnaongea ya jana ambapo Chuo kins wanafunzi zaidi ya 16,000!
Unaweza ukachangia hata kama haukuwapo kipindi cha Bibo na Campus.
Kuna uzi wa UDSM wa wale waliosoma msosi bure hakuna boom pia jaribu kuupitia.
 
Ni kweli jamaa alikuwa na nyota ya kupendwa lakini pia mshindani wake aliyewekwa alikuwa dhaifu na alipata ufadhili wa chama cha majambazi. Sasa hii iliwaongezea watu monkari wa kumpa Odong kura. Kipindi hiki mlimani ilikuwa sifa sana kujitambulisha kama mwanaharakati na aibu kubwa kujihusisha na serikali kwa namna yoyote ile.
Shida kubwa ya huyu ndugu Odong aliupenda sana uraisi wa DARUSO. Na kwa sababu hiyo vijana wa system wakamdanganya kwamba ili aungwe mkono na serikali achukue kadi ya UVCCM. Baada ya kumpa tu, usiku wakamvamia na kesho yake akawa deported! Wana tulipopewa taarifa kwamba jamaa alikamatwa na kadi ya UVCCM hakuna aliyeangaika naye. Hata hivyo serikali iliyochaguliwa haikudumu, ilipinduliwa na wazee wa DARUSO board wakaongoza kwa mwaka mzima. Ni furaha yangu kwamba tuliwatendea haki wanamapinduzi na familia ya wanafunzi wa Udsm kwa ujumla.
 
Sisi wa Kunjii ya Al shabab Japokua Rev Square ilikuwepo na Katibu wa uenezi ACT wazalendo nilimuona anamwaga nondo pale miaka hiyo
 
😂😂😂😂😂😂 bila ya shaka ulikuwa mteja wake mzuri sana ili kuepuka mchupi wa kupepea 🤣🤣🤣🤣🤣
 
First year niliishi Hall 7 ila habari za kubebana ndio sipendi mana watu wakiomba uwabebe huwezi kataa.,
2nd na 3rd Yr nkaishi Mabibo raha mustarehe
Mi na besti angu tulikua tunatoka mabibo asbh tunarudi jioni most of the times mana foleni lile mataa Ubungo miaka hio sio poa kabisa tuliokaa mabibo ndio tunaelewa..tukishinda campus mchana tunasoma zetu km hatuna vipindi, wa Main campus wanaenda kulala na kuoga huko na kufua sijui,..tulifaulu vizuri tu Alhamdullilah mana shule ilikua km kwenda kazini daily😅

sipendi kufua long time wale wafanya usafi Mabibo kule walikua wanafua kwa sh 100/200 likewise kuchotewa maji...ni mteremko...sibebi maji sifui...

chakula cha cafeteria nmekula first year, Mungu mkubwa kuna kazi fulani nilikua nafanya part time basi most of 2nd Yr na 3yr nimekula HillPark na TUKI kule..

it was a good time.,
Ila na changamoto zingine zilikuwepo
Mungu Mkubwa katuvusha tulikua bado wadogo🙏🏽
 
Vp wenzako walikuelewa kwelii?

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 

Hall 7 ground floor na Block B
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…