Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Lile tangazo la Condom lirudi aisee
"Tabasamu nipate furaha,usiwe unanuna babe"
Kuna kadada kanashikwa mkono huku kakiwekewa mwamvuli kasiloe. na mvua,lile tangazo zuri nilikuwa nalipenda.
Bila hivvo jamii itapukutika sana,Trump hana utani,Marekani kwenyewe wanaisoma namba
 
Zilikuwa zinaitwa dawa za kuongeza siku miaka hiyo pale dar temeke kulikuwa na taasisi ya kanisa la RC ikiitwa PASADA ilikuwa kituo cha afya huku kikifanya kazi kama ANGAZA, walianza kutoa dawa hizo kama kusaidia waathirika wa UKIMWI. Miaka hiyo kupima ilikuwa shughuli pevu licha ya kuwepo kwa kampeni za kupinga unyanyampaa kwa waathirika
 
Nikiwa shule salamu ilikuwa "UKIMWI UNAUA TUJIHADHARI TUSIPATWE NA UKIMWI, SHIKAMOO MWALIMU"

kama kwenu kuna mgonjwa wa ukimwi, hatupiti hiyo njia. Tunaogopa.

Pia kuna watu walipata ukimwi kwa kuuuguza wagonjwa wa ukimwi. Especially wazee.
Nakumbuka ndugu zangu wengi walioenda Mombasa walirudi na ngwengwe aise.
 
Hali ilikuwa mbaya nakumbuka kuna sehemu moja kanyigo ukipita utakuta nyumba ina mbibi alafu pembeni ni makaburi
hivyo sasa ndo hali ilivyokuwa. apo itakuwa watoto wote wameshapukutishwa ndo ayo makaburi. bi mkubwa kabaki mwenyewe na ukute hana tena wa kumsaidia
 
Vyama vya wenye UKIMWI vilianzishwa na kuunda shirikisho lao likiitwa SHDEPHA+ viongozi wake wa mwanzo kabisa walikuwa ni wale waliojitangaza wazi kuwa ni waathirika, pamoja na hali yao hiyo walijipatia umaarufu nchi nzima mpaka kufikia wengine kutaka kugombea ubunge
 
Mdogo wake rafiki angu alipotea
Tumekuja kumpata kumbe alienda house party huko wamejifungia siku 5 ni uzinzi tu nadhani walikuwa wanafanya group sex
Aisee watoto wa chuo wanapukutika na tamaa ndo zinawaponza
Hivi house party ni nn huwa nasikiaga

Aseeh poleni
 
nyumba jirani kulikuwa na familia ya baba mwenye wake watatu. wale watu walikatika wote kama masihara iviivi hlf ilikuwa kama mwaka mmoja au miwili kabla dawa hazijaanza😯.
 
Aya marazi niyakutengenezwa pia kunasiri nyingi najalibu kufikilia kama ugonjwa alipatikana kagera kwa mtu mmoja ulienea vip? Maan ilikua rahisi kuzibiti kupitia uyo mgonjwa? nawaza mbali zaid miaka ya 70 miundo mbinu haikua rafiki kusababisha muingiliano wawatu wengi, je ilikua vip ugonjwa kufika dar au mtwara? na vip kuhusu watu wa vijijini?

Mkuu, jamii iliyoanza kuathirika ni jamii kutoka Bukoba, maambukizi kuenea na kuwafikia watu zaidi ya wawili ni 💯.

Kumbuka kuna ndugu kutoka mikoa mingine waliokuwa wakiingia Kagera kwa wenyeji wao.

Kuna wanafunzi kutoka mikoa mingine waliokuwa wakichaguliwa kwenda Kagera kwa ajili ya elimu.
Nyakato sec.
Rugambwa sec.
Kahororo
Ihungo

Kuna waajiriwa pia waliokuwa wakitoka mikoa mingine.

Bila kuwasahau wavuvi kisiwa cha Goziba.
 
Enzi hizo ukipata UKIMWI watu wanaanza kukuhesabia siku wakisema hamalizi mwaka. Kuna watu tangu enzi hizo walijulikana ni waathirika mpaka leo ni wazima tena wana afya nzuri hawana hofu ya kufa kwa ugonjwa huo
Wapo wliobahatika kukutana na dawa wakasalimika itakuwa ndo hao unasema wanadunda hata sasa. ila haikuwa rahisi aisee. ila kuna webgine waliondoka miezi michache kabla dawa hazijaanza kugawiwa.
 
Wapo wliobahatika kukutana na dawa wakasalimika itakuwa ndo hao unasema wanadunda hata sasa. ila haikuwa rahisi aisee. ila kuna webgine waliondoka miezi michache kabla dawa hazijaanza kugawiwa.
ndio hao hao waliokutana na dawa, wanadunda hadi sasa
 
Vyama vya wenye UKIMWI vilianzishwa na kuunda shirikisho lao likiitwa SHIDEPHA+ viongozi wake wa mwanzo kabisa walikuwa ni wale waliojitangaza wazi kuwa ni waathirika, pamoja na hali yao hiyo walijipatia umaarufu nchi nzima mpaka kufikia wengine kutaka kugombea ubunge
wakiitwa SHDEPHA+ hao wamba wapo hata sasa.
Jamaa ilikuwa ukisikiza stori zao zikisikitisha sana maana wanakaa kikao kama leo, wakikutana tena miezi kadhaa mbele wanakuta wajumbe kibao hawajaweza kuja kwa kuzidiwa ugonjwa au ndo walishakufa.
 
Mkuu, jamii iliyoanza kuathirika ni jamii kutoka Bukoba, maambukizi kuenea na kuwafikia watu zaidi ya wawili ni 💯.

Kumbuka kuna ndugu kutoka mikoa mingine waliokuwa wakiingia Kagera kwa wenyeji wao.

Kuna wanafunzi kutoka mikoa mingine waliokuwa wakichaguliwa kwenda Kagera kwa ajili ya elimu.
Nyakato sec.
Rugambwa sec.
Kahororo
Ihungo

Kuna waajiriwa pia waliokuwa wakitoka mikoa mingine.

Bila kuwasahau wavuvi kisiwa cha Goziba.
miaka iyo sanasana wanaume ndo walikuwa wanauchota uko mijini kwenye mizunguko yao wanawaletea wake zao nyumbani.
 
Nakumbuka kijijini kwetu mgonjwa wa kwanza alikuwa mwanajeshi akaletwa akiwa hoi mwaka 1987 majira ya kiangazi.Elimu ilitolewa kwa wanafamilia katika kumtunza mgonjwa wa AIDS(ilitamkwa kama edisi).Kama ni unyanyapaa mtu yule alipitia tena wa kutisha kwani iliaminika kwamba akikugusa tu unapata edisi.Wengine tulikuwa kinda na hivyo tulionywa juu ya uzurulaji twawezakutana naye akatugusa tukapata edisi.Mpaka mwaka 1992 ugonjwa wa edisi ukapewa jina la UKIMWI.Kwa kweli tuliowauguza wagnjwa wa UKIMWI mpaka hatima ya maisha yao,kumbukumbu zikirejea mpaka hamu ya mbususu inapungua maana shughuli ilikuwa pevu.
 
Back
Top Bottom