Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

aiseee acha kabisa maticha walikatika sana nazan ni mambo ya kulana wao kwa wao. mdudu anazunguka umoumo
Teh teh tehee!!,ilikuwa ni hatari,mzunguko ulikuwa mkubwa,na hapo ndo ilijulikana baadae sana kwamba hata mzazi fulani kamla mwanae au ndugu wamekulana,huu ugonjwa uliibua siri nyingi sana,lkn pia wengine walipata maambukizi kwa kushear vitu vya ncha kali, hasa uko kagera watu walishear zile pini zakutolea wale funza miguuni,vidoleni,sindano za hospital nk,ilikuwa hatari usipime.
 
Watu walipukutika sana aisee. Mimi nilikuwa UDSM tukawa tunazika karibu kila baada ya siku mbili; pale Kinondoni makaburini kulikuwa na baa moja ya container wakatuzowea sana kwani baada ya mazishi wengi wetu tulikuwa tunapata moja baridi pale kabla ya kurudi zetu mlimani.

Wakati huo serikali ya Kenya ilitupatia Kemron lakini haikusaidia
Mlikua mnazika wanachuo ?
 
kuna jamaa aliugua kwa muda mrefu sana. ilifikia wkt kila sehemu ya mwili ilikuwa imeisha amechonga mwili mzima umebaki mifupa kichwa kimekongoroka ila akawa bado yu mzima tu hafi. watu wengine wazima wanakufa yeye yupo tu.

miaka inakata yeye bado yupo! kuna wakati anaweza akaumwa sanaaa mkasema huyu kesho hataamka au wiki ijayo hafiki, lakini wapi kunakucha na mawiki na miezi na mwaka unakata jamaa yupo anadunda zake fresh tu.

alikaa kwenye hali iyo muda mrefu adi yeye mwenyewe akachoka maana maumivu yalikuwa ni makali sio ya apa kiasi hata yeye mwenyewe hafurahii tena uwepo wake apa duniani lakini ndo ivyo mungu anaendelea kumtunza. bdae sana alifariki lakini kwakweli palichimbika aisee yani acha kabisa
Wagonjwa wengi kipindi hicho walikua na asila walkua ni watu wa kufokea kila mtu tena bila kumkosea wala unakua huja msemesha ila akiona una muangalia tu kosa ana kua mkali.
 
Wagonjwa wengi kipindi hicho walikua na asila walkua ni watu wa kufokea kila mtu tena bila kumkosea wala unakua huja msemesha ila akiona una muangalia tu kosa ana kua mkali.
hii ni kweli kabisa kiongozi ilikuwa ni risk sana kumtazama mtu mara mbilimbili
 
hii ni kweli kabisa kiongozi ilikuwa ni risk sana kumtazama mtu mara mbilimbili
Naam,alikua anaona kama vile unamchulia kifo,,usione sasa jamaa wanadunda tu,kuna jamaa namfahamu anatembeza bakora ile mbaya,anajivunia sana kiafya chake kimwonekano,atakuwa ana supply virus huyu,ila wengi wameshamjua.
Sijui akikosa ARvs itakuwaje!!!
 
Naam,alikua anaona kama vile unamchulia kifo,,usione sasa jamaa wanadunda tu,kuna jamaa namfahamu anatembeza bakora ile mbaya,anajivunia sana kiafya chake kimwonekano,atakuwa ana supply virus huyu,ila wengi wameshamjua.
Sijui akikosa ARvs itakuwaje!!!
sasa izo ARVs zisitopishwe basi kama watu hawataki kuacha ngono wafe
 
sasa izo ARVs zisitopishwe basi kama watu hawataki kuacha ngono wafe
Kabisa nakuunga mkono, maana zinachochea maambukizi kuenea,wazungu waliona waafrika wanapenda sana ngono,wakaona watengeneze hivi dawa ili weusi waendelee kumalizana,ndicho walicholenga,,kiutaalamu na kwa akili za kuzaliwa ilitakiwa ku deal na chanzo(kushawishi na kuhimiza watu waache zinaa),sio kudeal na matokeo,,ambayo itakuwa too late.
 
Watoto wa 2000 hawajui mgonjwa wa ukimwi ambae yupo kitandani anakuaje
Kipindi ferooz ametoa heat song starehe..Kuna jirani mmoja KIJANA TU WAKATI huo aliukwa.

Jamaa huyu Alijiua sababu ya kuimbiwa huo wimbo kimzaha mzaha na vijana wa mtaani enzi izo.

Yaani mtu mwenye ukimwi akikohoa mlio karibu yake mnasogea kwa kuogopa.
 
Kabisa , Gen Z hawajashuhudia live wagonjwa wa "NGOMA" wale wa zamani bila ARV.
Screenshot_20250223-214045_Chrome.jpg
 
hii ni hadithi ya kusisimua ya bwana Josefu wa nchini Haiti. Mwaka 2003 bwana huyu alipatikana katika hali ngumu sana akikabiliwa na magonjwa ya TB na HIV/AIDS.

Kwa bahati nzuri bwana huyu akapatiwa matibabu kiasi cha kuimarika afya yake na kumuondoa kwenye hatari dhidi ya uhai wake. Miaka kumi mbeleni (2013) taswira ya Josefu inaonesha ni mtu aliyejaa uso angavu wenye nuru na matumaini tele. huwezi hata kuthubutu kumdhania kuwa ni yule mgonjwa mahututi wa 2003. Josef alifariki 2015.
 
Halafu kuna mswahili akishashiba ugali na maharage, akashushia na kidugugu anakuja humu kusema kwamba ukimwi haupo ni utapeli tu!
 
haya mambo ya imani ni magumu kama jina lenyewe ''imani" lilivyo. kuna mwaka nazani 2009 alitokea tabibu uko loliondo kule umasaini akiitwa babu wa loliondo. uyu alidai kuwa na dawa inayotibu magonjwa 5 ikiwemo hiv.

akapata wateja wengi sana hata viongozi wengi wa serikali na wazungu walienda uko. watu wengine wengi kutoka nchi zingine wakaenda uko.

wale waliokuwa na wagonjwa kwenye haya mahospitali wakawatoa wagonjwa wao mahospitalini wakaenda nao uko. tena wagonjwa wengine wakisafiri wametundikwa drip zao za hospitali. lakini ndoivo tena bdae ikaonekana ile dawa haikuwa kitu na wale walioacha kabisa dawa walizopewa mahospitalini wengi walipotea.

Dah Umenikumbusha mbali sana, Mzee wa kikombe,
Walikuwa wanasema ameoneshwa meli kubwa ya raia wa kigeni wakienda kupata kikombe,
Watu walitiririka sana Loliondo.

Ila Babu aliwaweza watu 🙌🙌🙌

Mchungaji Ambilikile Mwasapile RIP
 
Back
Top Bottom