Tukumbushane tukio la Ujambazi pale Ubungo Mataa mwaka 2006

Aisee watu mna kumbukumbu sana nakumbuka nilikua mdogo chalii hivi darasa la saba Asubuhi nilikua Nafuatilia kwenye kipindi cha magazeti Radio Free Africa kinaitwa "Watanzania tuzungumze magazeti" msomaji alikua Tom Chilala [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jioni mzee akirudi na magazeti story ninayo kwa Muda km wa mwezi mzima hivi.

Namkumbuka sana yule askari aliyekua akiongoza magari ubungo akageuka shujaa Koplo Solomon Mwangamilo.

Mungu azilaze roho za marehemu wote waliofariki kwenye Ile mikikimikiki.
 
Tukio la kariakoo walimwaga begi zima,ili kublock njia polisi wasiweze kupita,watu wakawa wanagombania eka ,polisi kweli walishidwa kupita
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] daah ningekuwepo
 
Tukio la kariakoo walimwaga begi zima,ili kublock njia polisi wasiweze kupita,watu wakawa wanagombania eka ,polisi kweli walishidwa kupita
Hii wafanye tena hali ngumu tukiokotee vitita vya milion milion[emoji3]
 
Nimeona hii kitu jasho jembamba limetoka ghafla, I was there; wakati huo nasoma Jitegemee A- level, that day nimepata ruhusa nikawa naenda Kimara kutembelea ndugu.

Nimepanda hiace nikakaa siti ya nyuma kabisa, tuko pale mataa tunasubiri gari za kutoka Mwenge zilikuwa zina cross kuelekea mitaa ya Mabibo hostel ( hii njia nimeisahau jina) na mengine yana cross toka Sam Nujoma kuelekea Kimara.

Ghafla nikasikia sauti nikahisi tairi la gari limepasuka, nikaisikia tena, mara tena, na tena, nikajua hapa sio poa, kuna shida, natazama nje, naona kupitia dirishani barabara nyeupe hakuna mtembea kwa miguu hata mmoja, nikatoka kule nyuma nilipokuwepo nikaenda zile siti mbili pale mbele nyuma ya siti ya dereva, sio kukaa kujibanza pale chini abiria wanapoweka miguu..

Wale jamaa waliokuwa nimekaa nao, na siti iliyofuata nao wote wakanifuata, tukajazana wote pale mbele wake kwa waume, nilifanya vile nikijua risasi inaweza kutoboa bati la gari nyuma ikanila mgongo ndio maana nikakimbilia mbele, tumekaa pale km dkk kumi ni majibizano tu ya risasi nje, wote kimya hakuna anayeongea na mwenzake wala nini.

Baada ya muda nikasikia ukimya umekuja, sasa nani aanze kunyanyua kichwa, nachungulia pembeni kumbe kondakta nae alikimbia akaacha mlango wa gari wazi hata sikujua, baadae ndio nasikia km sauti za wawili watatu wanaongea nje ndio tukapata nguvu tukaanza kujiinua pale chini, tukatoka nje eneo lote la ubungo anzia pale jengo la Tanesco, mataa, kote hapakuwepo na mtu hata mmoja barabarani nakumbuka ilikuwa kam saa sita mpk nane mchana hivi, palikuwa peupe..

Nimetoka pale naanza kuangalia baadhi ya magari nayaona yana matundu ya risasi, ndio nikajua huu mchezo uliokuwa unachezwa hapa haikuwa movie, na traffic mmoja ndio alisimamia ile show sijui alipata wapi silaha wakati ule, wale abiria wenzangu nao sijui walipotelea wapi.

Hakuna aliyeongea na mwenzake wala nini, kila mmoja alikula kona yake hakuna aliyekuwa na hamu ya barabara tena siku ile, baadae ndio nasikia ni majambazi waliiba NBC Ubungo branch walisababisha yote yale, na mmoja wao aligundulika alikuwa mwanajeshi Mgulani JKT baada ya kukamatwa ila sikumbuki km walifungwa au vipi..
 
Ile siku nilishuhudia tukio la kipekee yule mmimina manjugu alizimiminaa mara zikaacha kutoka akalikita limkanda likakatika akaendelea kumimina hovyo.

Karibu na nilipokuwa nimelala kulikuwa na mzee mmoja akainuka kwenda fungua mlango wa gari niliishia kusikia mlio tu wa risasi
 
Attacker wao huyo mweusi na kipara kinachong'aa ni Juma huyo na alikuwa mwanajeshi wa JWTZ kule Zanzibar. Alikuja kamatwa na baadae akaachiliwa jamaa hamfahamu tulikuwa wote kwenye utoto wetu. Alikuwa anakula ganja toka primary school.
 
Nilikuwa pale sheli nakumbuka tullingia kwenye mivungu ya magari yaliyokuwepo pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…