Aisee umenikumbusha hii siku, na namkumbuka sana Marehemu Michael (R.I.P) nitaeleza kuhusu marehemu Michael hapo mbeleni.
Basi, ilikua siku za kawaida tuu, mwaka huu nilikua bado mwanafunzi maeneo ya Mjini kati. Kwaiyo nilikua na urafiki wa karibu na Marehemu Michael ambaye baadae alinitambulisha kwa Solomon.
Ilikua ni utaratibu kwamba Michael akitoka kwake anapita mitaa ya home saa 11 asubuhi anaita dogoooo... basi nachomoka tunatembea mpaka barabarani, kama siku ana gari basi anapiga honi chap natoka ( kumbuka 11 asubuhi ni giza totoro na tulikua tunakaa shamba kabisa).
Tukifik kituoni kama hatuna gari tunasubiri gari ya solomon hii gari yake kwanza ndani ni mziki wa congo mixer speed za hatari, yani light speeed.
Sasa siku ya tukio, Marehemu Michael hakuwepo, nikamsikilizia paleeee kimya, mpaka bimkubwa nae akamaliza kujianda ikabidi nisepe na bimkubwa mpaka kituoni.
Tunafika kituoni tuu, solomon huyu hapa. Kama kawaida light speed akasalimiana na bimkubwa maana Michael alikua kashamtambulisha kua ni dada yake na mm michael nilikua namuita uncle. Basi tukaingia safari ikaanza.
Katika story solomon akawa anamwambia dada "leo niende kucheki, moyo unaniuma" bimkubwa akamwambia kacheki ndugu yangu, lakini baadae tena akasema lakini hii siku ya leo sijui imekaaje!. Yani kama anaona wenge hivi. Hapa ndio mshana anakujaga na mazaga yake ya jicho la 3.
Siku hii ndio kamanda solomon alipambana na hao mafedhuli pale ubungo.
Namkumbuka sana, Marehemu na solomon kwasaidia Elimu yangu maana usafiri haikua shida na bado walikua wanachanga wananipa mzigo wa kutumia shule.
Nilikua don na clean, because of these two great people Solomon and Michael ( R.i.p)