Tukumbushane tukio la Ujambazi pale Ubungo Mataa mwaka 2006

Tukumbushane tukio la Ujambazi pale Ubungo Mataa mwaka 2006

Naomba link ya huo Uzi wa mwaka huo, maana wengine tulikuwa shamba miaka hiyo
 
Miaka hiyo nafanya kazi dsm posta huko.

Ujambazi ulienea kila upande wa jiji.

Kwa simulizi ya baba aliyekuwa ndani ya daladala sekeseke lilipoanza abiria walilala chini.

Huyo baba alisema alipolala akaja mama mmoja kibonge akalala juu yake.

Alipoinuka alikuta amelowa mikojo mwili wote.

Was so bad. Sijui alikuwa nani President that time

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sawa kabisa,hicho kijeba JB,kuna siku wakapiga tukio pale Sea Cliff kwenye bureau de change.

Huyo mzee wa kihindi mwanae akauliwa on the spot, Yule kijana alikua karudi toka masomoni UK. Akauliwa pale ndio alikua na fuko la pesa. Wametoka bank na babaake

Yule mzee sikuwai kumuona tena pale ofisini.baada ya tukio, Kaka wa huyo kijana alikua nae Mafia fulani. Aka take -over aliwapata wote,kuna siku Sinza huko kijeba na wenzie walienda kupiga mahali akawalia timming. wakachabangwa kunde wote huyo kijeba akiwemo.

Ndo ikawa mwisho na huyo muhindi alitoroka kabisa akahama nchi.

Kama movie vile aisee
 
Mwangamilo is his surname.
Jina hili linaanza kunikumbusha issue ya Laura Nkunda na Major General Mwakibolwa wa JWTZ alipokuwa pamoja na majeshi ya UN kule Congo. Jamaa aliibuka siku moja kwenye media akasema huyu Nkunda tutamshughulikia vizuri tu na wala hakuna shida yoyote.

Kuna watu wanaojiamini kwenye haya mambo, yaani ni professional perce
 
Kipindi kile DSM haikuwa ajabu kusikia matukio matatu mpaka manne kwa wiki halafu yote ya hatari lazima damu imwagike,mimi huwa nashangaa mtu anaposema ujambazi umerejea leo 2022 unajiuliza huyu ana umri gani?ilikuwepo miaka mtu kutembea na 500K mfukoni unakuwa hatarini.

Nakumbuka siku ilianzwa kwa majibizano makali ya risasi pale Kariakoo mtaa wa Swahili na Mafia ambapo polisi waliondoka na point zote tatu hiyo ilikuwa mapema tu saa 8:35 asubuhi,mchana majira ya saa saba mtaa wa Livingston na Mkunguni ule muda wa kwenda msikitini jamaa wakaingia sonara moja ilikuwa kubwa sana wakati ule.

Wakauwa mlinzi mwarabu boss wakamvunja nyonga wakachukua vyao wakaondoka,huku mitaa ya Jangwani na Congo kwa wale wauza vipodozi likapigwa tukio kupishana kama dk 40 hivi alikuwaga bwashee kaambiwa akabidhi fuko la hela yeye macho yamemtoka jamaa wakaona anawachelewesha wakamchapa ya mbavu wakachukua fuko wakaondoka (huyu alipona)

Pale police Msimbazi siku hii pale counter askari walibaki wawili tu wote waliingia mtaani kipindi hiki RPC alikuwa Alfred Tibaigana nakumbuka kumuona ndani ya defender pale mtaa wa Msimbazi akiongoza kikosi.

Funga kazi ni hiyo ya Ubungo jamaa waliuwa stuff wa Nmb na askari,attacker wao alikuwa kijeba hivi amejazia amevaa kawoshi na bukta ana kipisi anamimina njugu kama ana-act movie halafu mweusii kichwani ana kipara kinang’aa!

Yupo jamaa yangu aling'ang'aniwa baada ya kuonekana pikipiki iliyoshiriki lile tukio imeingia nchini kwa jina lake alikaa jela miaka nane na matukio mengi kipindi kile wapigaji walikuwa wanashirikishwa na wabongo refer tukio la kupigwa bomu kwa ATM machine pale Temeke hospital jamaa walivyofanyiwa ambush na askari Chang'ombe waliuwawa sikumbuki idadi but mmoja wao alikuwa na id ya Rwanda.
Lakini Magufur aliwaweza wote majambaz
 
Aisee watu mna kumbukumbu sana nakumbuka nilikua mdogo chalii hivi darasa la saba Asubuhi nilikua Nafuatilia kwenye kipindi cha magazeti Radio Free Africa kinaitwa "Watanzania tuzungumze magazeti" msomaji alikua Tom Chilala [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jioni mzee akirudi na magazeti story ninayo kwa Muda km wa mwezi mzima hivi.

Namkumbuka sana yule askari aliyekua akiongoza magari ubungo akageuka shujaa Koplo Solomon Mwangamilo.

Mungu azilaze roho za marehemu wote waliofariki kwenye Ile mikikimikiki.
Matukio yote hayo ya ukatili alifanya Magufuri
 
Nimeona hii kitu jasho jembamba limotoka ghafla, I was there, wakati huo nasoma Jitegemee A- level, that day nimepata ruhusa nikawa naenda Kimara kutembelea ndugu.

Nimepanda hiace nikakaa siti ya nyuma kabisa, tuko pale mataa tunasubiri gari za kutoka Mwenge zilikuwa zina cross kuelekea mitaa ya Mabibo hostel ( hii njia nimeisahau jina) na mengine yana cross toka Sam Nujoma kuelekea Kimara.

Ghafla nikasikia sauti nikahisi tairi la gari limepasuka, nikaisikia tena, mara tena, na tena, nikajua hapa sio poa, kuna shida, natazama nje, naona kupitia dirishani barabara nyeupe hakuna mtembea kwa miguu hata mmoja, nikatoka kule nyuma nilipokuwepo nikaenda zile siti mbili pale mbele nyuma ya siti ya dereva, sio kukaa kujibanza pale chini abiria wanapoweka miguu..

Wale jamaa waliokuwa nimekaa nao, na siti iliyofuata nao wote wakanifuata, tukajazana wote pale mbele wake kwa waume, nilifanya vile nikijua risasi inaweza kutoboa bati la gari nyuma ikanila mgongo ndio maana nikakimbilia mbele, tumekaa pale km dkk kumi ni majibizano tu ya risasi nje, wote kimya hakuna anayeongea na mwenzake wala nini.

Baada ya muda nikasikia ukimya umekuja, sasa nani aanze kunyanyua kichwa, nachungulia pembeni kumbe kondakta nae alikimbia akaacha mlango wa gari wazi hata sikujua, baadae ndio nasikia km sauti za wawili watatu wanaongea nje ndio tukapata nguvu tukaanza kujiinua pale chini, tukatoka nje eneo lote la ubungo anzia pale jengo la Tanesco, mataa, kote hapakuwepo na mtu hata mmoja barabarani nakumbuka ilikuwa kam saa sita mpk nane mchana hivi, palikuwa peupe..

Nimetoka pale naanza kuangalia baadhi ya magari nayaona yana matundu ya risasi, ndio nikajua huu mchezo uliokuwa unachezwa hapa haikuwa movie, na traffic mmoja ndio alisimamia ile show sijui alipata wapi silaha wakati ule, wale abiria wenzangu nao sijui walipotelea wapi,

Hakuna aliyeongea na mwenzake wala nini, kila mmoja alikula kona yake hakuna aliyekuwa na hamu ya barabara tena siku ile, baadae ndio nasikia ni majambazi waliiba NBC Ubungo branch walisababisha yote yale, na mmoja wao aligundulika alikuwa mwanajeshi Mgulani JKT baada ya kukamatwa ila sikumbuki km walifungwa au vipi..
Hakuwa mwanajeshi na walimkamata mtu ambae anafanana sana huyo jambazi ambae tuna undugu nae. Amekaa ndani miaka kumi na tano mpka alipokuja kupatika huyu jambazi ambae alikua kikosi cha jeshi Zanzibar.
 
Hakuwa mwanajeshi na walimkamata mtu ambae anafanana sana huyo jambazi ambae tuna undugu nae. Amekaa ndani miaka kumi na tano mpka alipokuja kupatika huyu jambazi ambae alikua kikosi cha jeshi Zanzibar.
Haja sue kwa false imprisonment mkuu apige hela

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom