Nimeona hii kitu jasho jembamba limetoka ghafla, I was there; wakati huo nasoma Jitegemee A- level, that day nimepata ruhusa nikawa naenda Kimara kutembelea ndugu.
Nimepanda hiace nikakaa siti ya nyuma kabisa, tuko pale mataa tunasubiri gari za kutoka Mwenge zilikuwa zina cross kuelekea mitaa ya Mabibo hostel ( hii njia nimeisahau jina) na mengine yana cross toka Sam Nujoma kuelekea Kimara.
Ghafla nikasikia sauti nikahisi tairi la gari limepasuka, nikaisikia tena, mara tena, na tena, nikajua hapa sio poa, kuna shida, natazama nje, naona kupitia dirishani barabara nyeupe hakuna mtembea kwa miguu hata mmoja, nikatoka kule nyuma nilipokuwepo nikaenda zile siti mbili pale mbele nyuma ya siti ya dereva, sio kukaa kujibanza pale chini abiria wanapoweka miguu..
Wale jamaa waliokuwa nimekaa nao, na siti iliyofuata nao wote wakanifuata, tukajazana wote pale mbele wake kwa waume, nilifanya vile nikijua risasi inaweza kutoboa bati la gari nyuma ikanila mgongo ndio maana nikakimbilia mbele, tumekaa pale km dkk kumi ni majibizano tu ya risasi nje, wote kimya hakuna anayeongea na mwenzake wala nini.
Baada ya muda nikasikia ukimya umekuja, sasa nani aanze kunyanyua kichwa, nachungulia pembeni kumbe kondakta nae alikimbia akaacha mlango wa gari wazi hata sikujua, baadae ndio nasikia km sauti za wawili watatu wanaongea nje ndio tukapata nguvu tukaanza kujiinua pale chini, tukatoka nje eneo lote la ubungo anzia pale jengo la Tanesco, mataa, kote hapakuwepo na mtu hata mmoja barabarani nakumbuka ilikuwa kam saa sita mpk nane mchana hivi, palikuwa peupe..
Nimetoka pale naanza kuangalia baadhi ya magari nayaona yana matundu ya risasi, ndio nikajua huu mchezo uliokuwa unachezwa hapa haikuwa movie, na traffic mmoja ndio alisimamia ile show sijui alipata wapi silaha wakati ule, wale abiria wenzangu nao sijui walipotelea wapi.
Hakuna aliyeongea na mwenzake wala nini, kila mmoja alikula kona yake hakuna aliyekuwa na hamu ya barabara tena siku ile, baadae ndio nasikia ni majambazi waliiba NBC Ubungo branch walisababisha yote yale, na mmoja wao aligundulika alikuwa mwanajeshi Mgulani JKT baada ya kukamatwa ila sikumbuki km walifungwa au vipi..