Tukumbushane ukoloni uliowahi fanyiwa na wazee wako

Mzee wangu nakumbuka alikuwa anawahi kwenda shamba saa11 alfajili na kabla hajaondoka anatuamsha watoto wake , ilikuwa ikifika saa12asubuhi anarudi kuona nani hajaamka na alikuwa ana tabia ya kutumwagia maji pamoja na Yale magodoro tuliyolalia
Hiii ilikuwa tabia ya bibi angu anakuamsha saa kumi Na mbili asubuhi ata kama hauna kazi amka tu Sasa usipo amka anakumwagia maji ya kwenye mtungi yalivyo ya baridi ukichanganya na baridi la asubuhi[emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25] nampenda sana bibi angu alikuwa dicteta ila now naona faida yake (sorry sijalelewa Na mdingi)
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] du unachapwa kabla ya kosa ,sasa siku ukifanya kosa viboko vitapungua?
 
nimecheka sana asee
 
Wazee ni wote baba na mama sema wtu wanachanganya na nadhani pia wamekariri
Ooooh!! Kwa baba aisee tulikuwa na baba mpole, hakuwahi hata kunifinya na nilikuwa kipenzi chake ila kwa mama daaaah!!

Kuna siku nimetoka shule(nikiwa std2), njiani tukaamua tucheze 'marede', nikavua soksi zangu tukatengenezea mpira, nikarudi home kwa kuchelewa,mchafuuuu na soksi zimelegea, mama akajua tu kilichofanyika, tofauti na nilivyotegemea, hakuniuliza chochote.

Sasa kesho yake kulikuwa na maonyesho ya mazingaombwe shuleni, jinsi ya kuomba pesa nikashindwa maana nshalivuruga, kesho yake asubuhi wakati nataka kuondoka nikaona hela mezani, nikachukua iliyotosha kiingilio huyooo nikasepa.

Kurudi jioni, akatukalisha na kaka yangu kutuhoji aliyechukua hela yake, nikajifanya sijui, kaka akasema yeye hajachukua, sijui hata alihisi nini ila akajua tu ni mimi, akanitega nikajikuta nimejaa, weeeeeeh nilikula kichapo, akatuambia pesa yoyote ni yake, hivyo tukitaka tumuombe, ikawa hata nikiokota hela barabarani nampelekea.
 
Dota Heaven Sent hebu njoo useme kama tuliwahi kukufanyia ukoloni.
Haha ahsante kwa kuniita bi mkubwa, aiseeee nimecheka khaaa. Yule wa kugeuzwa stand ya tv, wa kuchapwa kila kikinunuliwa kitu kipya, wale waliojizimisha wakafungwa mashati nyuma ya baiskeli, na wa kuambiwa asimame kijogoo, mweee

Ngoja nikumbukie vizuri ukoloni wenu
 
Yaani nilikuwa mahali alafu nikawa nasoma hii thread, nimecheka mwenyewe kama chizi, kui mayai sijui yuko wapi!!
 


Tehe teh!, jamani pole sana dear, eti hata ukiokota hela unampelekea, adabu mkononi manake. [emoji28] [emoji23] [emoji23][emoji23]
 
Hakuna kutoka nje wala kukaa na masela yani siwrz sahau tuliruka toka gorofan kwenda kucheza alipo rud tulipata kipondo haitosh mding lazima acheck daftar wewe ni noma sana.
 
Yaani nilikuwa mahali alafu nikawa nasoma hii thread, nimecheka mwenyewe kama chizi, kui mayai sijui yuko wapi!!


Wewe nimecheka jamani, wazee wengine ni tatizo ha haha. kui cha njaa sijui atakuwa wapi


Hahaha!, asanteni kwa kunishtua haki nimecheka. Yule wa kuhamisha tv chumbani akimaliza kuangalia mbona shughuli na kujipa kazi ya ziada!,

Halafu wakati nasoma nikawa kama vile naona anavyosukuma tv yake kwenda na kurudi. [emoji28] [emoji28] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Tehe teh!, jamani pole sana dear, eti hata ukiokota hela unampelekea, adabu mkononi manake. [emoji28] [emoji23] [emoji23][emoji23]
Yaani acha kabisa, sasa si ushaambiwa hela zote ni zake na ukitaka uombe!
Baada ya hapo ilibidi aanzishe self reliance program, kila mmoja na bustani yake ya mboga na kuku. Yaani yule mama nikimkumbukaga najikuta nacheka tu na kumshukuru.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Kweli lazima hiyo picha ikujie sijui kwanini!!! Anawakomoa huku nae anajikomoa!!
 
alikuwa akichinjwa kuku baba anamla wote sisi tunakula miguu ,kichwa na damu basi na manyoya
 
Ha ha haa eti hata ukiokota hela unampelekea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…