Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Lol, kwenye umati lazima utoke manundu hakuna namna.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ila raha ya kuanzisha mtiti uwe na nguvu.
Unamthaminisha kwanza mpinzani wako....afu unatambaa nae kiunaa.
Sio nguvu tu na tactics. Unaweza kuwa na nguvu ila ukila moja unapoteana...

Wewe siunaona kwenye WWE tu great kali alivyokuwa anamkalisha bigshow na limwili lake lote
 
Hahaaaaa umenikumbusha mwaka 2013 niko na Demu fulani hivii maeneo ya relini saa mbili unusu!
Niko namtomasa mtoto Zubedaa mara kaka yake akatingaa huyoo aisee nikapagawa, Jamaa akataka afosi anijue mm ni nani Demu akamkazia hataki animulike na tochi Huku na huku mara wakavaana wakaanza kutembezeana mkono wao kwa wao..
Muda wotee huo nimekaa sijui hata nifanyaje, nilishindwa kuamua wala kuingila huku moyoni najisemea ugonvi wa ndugu sipaswii kushirikii, dem naona anambinua kaka yake mara anabinuliwa na kakaka yake hadi akabaki taiti tupuuu..
Akili ikanijia nikatoka mbio nikaenda kuita watu wakaja kuamua, Alipotoka Akaja akanikumbatia akaniambia -Mond- wangu achana na hili lipuuzi Nakupenda sana huku ananinywesha juisi mbele za watu..
Toka siku hiyo nilijiona mm ni NYUMBU HASWAA huyu kama ningemuoa ningekua nimepata bodigadi wa maana..

Duuuh I miss you Zubee wangu bin cheupe
 
Sio nguvu tu na tactics. Unaweza kuwa na nguvu ila ukila moja unapoteana...

Wewe siunaona kwenye WWE tu great kali alivyokuwa anamkalisha bigshow na limwili lake lote
Au Daudi na Goliathi.

Nakumbuka nilikuwa Kariakoo mwaka mmoja, dunga dunga akataka kunigeuza kitoweo....mbona nilitaka kuondoka na dhakari zake.
Afu katikati ya soko
 

[emoji23][emoji23] wewe jamaa ulikuwa na bodyguard. Ila naye mafia anampiga hadi kaka.

Ila sio joanah kweli.......
 
Au Daudi na Goliathi.

Nakumbuka nilikuwa Kariakoo mwaka mmoja, dunga dunga akataka kunigeuza kitoweo....mbona nilitaka kuondoka na dhakari zake.
Afu katikati ya soko
Madame B inaonekana wewe mtataa balaaa aseeh. Ndiyo wale mkianzisha vagi hadi field force watue au mtaa unasimama kwa muda [emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23] wewe jamaa ulikuwa na bodyguard. Ila naye mafia anampiga hadi kaka.

Ila sio joanah kweli.......
Aaah J hawezi kusimamia hizii, daah na urembo wake sikuamini kama ndio kafanya vile..
 
Jirani,
[emoji3][emoji3]
Jirani, kwa hiyo ukamharibia binamu yako tongozo lake...

BTW, ungeliendeleza na huyo mkaka maana umati ulishajua unadate naye
huyo alijiharibua mwenyewe kwa kuandika jina mwishoni.
.............................................................................

Hii nyingine ndo ilifanya mpka leo kuwa makini na hasira zang.utoto raha sana.
Siku moja niko zangu mitaa ya kwa jirani ila ni karibu na home niko nausuka mpira wangu wa makaratasina na hii mifuko ya plastic,,jirani najua utakuwa unaijua hii mipira..nilipomaliza nikaanza kijipigisha danadana kumbe kuna mkaka alikuwa akiangalia kila kitu ninachokifanya (nilishawahigi kumtia kinazi (ndoo) ndg yake.kumbe aliniweka kiporo)

Sina hili wa lile jamaa akauchukua mpira wangu halafu akaniambia sikupi (jamaa alikuwa mkubwa kwangu nisingweza kumpiga) nilimuangalia kwa hasira nikajikuta nalia.ebwana nikajikuta natetemeka mwili mzima.kuangalia kushoto kuna tofali la udongo mbele yangu kuna jiwe.

Sikujua ni saa ngapi nililishika jiwe ila nilichokishuhudia ni yule kaka katupa mpira wangu chini analia na damu zikimtoka.ohoooo kuona hivyo mbio mpka kwa rafiki wa mama yangu wa kimasai nikampa mkanda mzima.akanambia kaa jion nitakupeleka nyumbn

Uko nyuma sasa mkaka wa watu kapelekwa hospital kashonwa nyuzi kama sio nane basi ni sita na ilibaki kidogo lile jiwe limlenge jichoni.

Jion nakuja kurudishwa kila kitu kimeshakaa sawa kule nilikoharibu kimbembe ni kwangu sasa..jmn baba aliniandalia mikwaju ya maana.mwisho wa siku maongezi yakafanyika hali ikwa shwar.

Tangu siku hiyo hadi leo marufuku hasira kuniongoza.

Na nashukuru huyo kaka mpka leo tumarafiki sana.
 
Madame B inaonekana wewe mtataa balaaa aseeh. Ndiyo wale mkianzisha vagi hadi field force watue au mtaa unasimama kwa muda [emoji23][emoji23]
Unajua kuna baadhi ya wanaume wanadhani wanawake wote ni maboya.
Mie sipendi dharau....
Yaani mie ukinichokoza jua nikitibiwa na kupona,
lazima nikutafute tuanze A.
Niliwahi pigwa stop Masai club, Waungwana bar na pale Igo Sinza....cheza vizuri, ukinibambia tu, kiboya nina wewe.
 
Aaah J hawezi kusimamia hizii, daah na urembo wake sikuamini kama ndio kafanya vile..
Teh
Wewe madame unaona show zake na uzuri wake. Vagi ni vagi Ngori ngori
 
Weweeee mbona hujanihadithia..
 
Hawanaga huruma[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee nakumbuka kipindi cha nyuma kidogo enzi hizo olevel nipo boarding sasa kuna jamaa alikua mwizi kishenz alikuwa katokea Tanga jina lake tukawa tunamwita "mtanga" sasa akawa anaiba nguo, mashuka, soksi,
Watu waka kaa kikao kumsaka mwizi siku ya siku ukaguzi ukaanza kwa wale wanao hisiwa daah kwenye dranka la mtanga tulikuta hadi sabuni, mashuka, nguo, soksi watu wakataka kumshushia kipigo dom leader akaamuru tumpe adhabu akavuliwa nguo, zote akabak
uchi kama alivozaliwa akapewa kipigo kwel mpaka akavimba uso baada ya hapo akatolewa nje daah ilikua aibu
Sasa kimbembe kavimba na anahitaji dawa alivimba usoni jichoni basi siku anaenda kuchukua dawa akamkuta
Matron, matron akamuuliza vip mbona umevimba mtanga akajibu "nimeng'atwa na nyuki" matroni watu walio kuwa karibu nae walicheka sana ila wizi aliacha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…