Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hivi mnakumbuka Time trax na Renegade??
Yap nazikumbuka sanaa
tapatalk_1481629253935.jpeg
tapatalk_1481628918593.jpeg
 
Vipindi vya music nilikuwa navutiwa navyo. Enzi za Cool James, Kwanza Unit, Diplomats. Nje walikuwepo The New Radicals, Everton Blender, Los Del Rio na C+C Music Factory, "one hit wonders" kama Mr. Vain, Boom shack a lack, Tom's diner, Scatman na nyingine nyingi tu . Kipindi kile nilikuwa na ndoto ya kuja kuwa msanii pia.
Tanzania ilionyesha kuwa inakwenda na mda pia. Atleast ngoma za Sikinde na za aina hiyo tuliwaachia wazee, wajomba na shangazi zetu. Rap, RnB na reggae dancehall ziliwavutiwa vijana na watoto sana.
 
Lorenzo Lamas a.k.a Rino Renz na mpikipiki wake ilikuwaga ni Bonge moja la series
 
NWO, mieleka akina macho men, hulk hogan, undertaker, lex Luger, Kevin nash
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
 
Back
Top Bottom