Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

unaangalia stesheni kwa sasa / nina kingamuzi cha azam ni steshesheni gani naweza angalia days of our lives
Sina taarifa ndugu yangu. Check na watu wa Dstv labda wanaweza kuupa clue, siyo lazima uwe na Dstv isipokuwa inaweza kuwa king'amuzi ulichonacho kina one of the channels ya soap oprea hiyo. Niliwah kuipenda sana. Kuna nyingine inaitwa SECOND CHANCE, main character Salvador Solenza, hii nayo nadhani itakuwa bado inaendelea kuonyeshwa mpaka kipindi hiki in one of the channels of course!
 
Hiyo CTN tunaijua wahenga tu na kisha tuliokulia jiji la Makamba wa mkoani TV zilikuwa ndio zinanusa.Hata humu wa mkoa watakumbuka ITV tu na kidogo DTV.
CTN jengo la SUKITA kitambo kidogo,kwa akina Ephraim Kibonde?
Kibonde alikuwa anatangaza mpira na michezo taarifa ya habari
 
Kitamboo mkuu historia tayari
 
We kweli unakumbuka zamani aisee, hicho kipindi cha Egoli place of Gold nilikuwa nakipenda sanaa aisee
 
Root and Reggae, smooth vibe,kwanja time,Africa bambataa,hawavumi lakini wamo
 
Usisahau na wakati huo kutazama TV mostly ilikuwa kwa neighbours, na TV nyingi zilikuwa National zile fremu ya mbao....

Wale wenye fweza ndio walikuwa na TV zenye plastic casing...
 
Nakumbuka CTN ikifika mida fulani hv usiku walikuwa wanaonesha muv za kizungu.. dah haha nimeamka sana usiku kuchek muv na nilikuwa napenda sana vipengele vya mahaba aise ilikuwa poa sana..
Walikuwa wanaunga TNT, hapo lazima watu wapigane mikasi
 
Jumapili ilikua ni shivooo na akina bajeee (nguruwe)
Zile tamthilia za mida ya kubeti, akina Barbarita, Tony, Marcidita, Theresita......daaah watoto wa Kilatino wakali saana. Mambo ya Copa Cabana.
.......Acapulco Bay ! Daah walatino wazuri jamanii !
 
Mimi nakumbuka world cup94 Italy ITV walirusha matangazo ya mpira kiufasaa na kulikuwa na tangazo la salama condoms nlikuw nalipenda sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…