Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

unaangalia stesheni kwa sasa / nina kingamuzi cha azam ni steshesheni gani naweza angalia days of our lives
Sina taarifa ndugu yangu. Check na watu wa Dstv labda wanaweza kuupa clue, siyo lazima uwe na Dstv isipokuwa inaweza kuwa king'amuzi ulichonacho kina one of the channels ya soap oprea hiyo. Niliwah kuipenda sana. Kuna nyingine inaitwa SECOND CHANCE, main character Salvador Solenza, hii nayo nadhani itakuwa bado inaendelea kuonyeshwa mpaka kipindi hiki in one of the channels of course!
 
Hiyo CTN tunaijua wahenga tu na kisha tuliokulia jiji la Makamba wa mkoani TV zilikuwa ndio zinanusa.Hata humu wa mkoa watakumbuka ITV tu na kidogo DTV.
CTN jengo la SUKITA kitambo kidogo,kwa akina Ephraim Kibonde?
Kibonde alikuwa anatangaza mpira na michezo taarifa ya habari
 
Dah! Nakumbuka kipindi hicho 95, 96, 97 niko primary tunafuga ng'ombe wa maziwa kila jioni natumwa kupeleka maziwa kota za Tiper kigamboni, home kwetu hakuna umeme tunatumia generator linawashwa saa mbili usiku hadi saa nne, so nikitoka mida ya saa moja kupeleka maziwa nilishachagua nyumba moja wenyewe hawana longo longo inakuwa ya mwisho nikifika nawakabidhi maziwa yao halafu nasimama hapo kucheck tv hapo ndio nilipoanza kuona isidingo, ikiiasha faster na baiskeli yangu nawahi home nakuta generator imewashwa nacheck news itv. Maisha ni safari.
Kitamboo mkuu historia tayari
 
Kuna vipindi kama Egoli, Hiki kipindi kilikuwa kinarushwa ITV, Ni kama isidingo ya sasa. Pia kuna Channel ilikuwa inaitwa ITV2 kwasasa nadhani ndio Channel 5, hii channel ilikuwa ni miziki tu tena ya Mbelembele.

Vipindi vya Maigizo kilikuwa kinajina sana kilikuwa Mambo hayo, waigizaji wake walikuwa wakina Bishanga, Aisha, Waridi na Rich mtambalike.

Enzi hizo channel bomba ilikuwa ITV kwa maigizo, hakuna bongo movie kabisa. Na mastar wa Movie bongo nzima hawakuzidi 15.

Mtaa mzima Tv ziko mbili, Vipindi vya michezo watoto mnajazana kwa jirani hadi kero kwa mwenye nyumba.

Ilivyo ingia miaka ya 2000, Ndio wasanii wengine wakaanza kuibuka kama wakina Muhogo, Mchungu, Cheni, Nyamayao, kibakuli, Bi hindu etc.

Sijui kwann ITV hawairudii hii michezo ya zamadi katika tasnia ya uigizaji, Ingetuburudisha sana sisi wahenga.
We kweli unakumbuka zamani aisee, hicho kipindi cha Egoli place of Gold nilikuwa nakipenda sanaa aisee
 
Root and Reggae, smooth vibe,kwanja time,Africa bambataa,hawavumi lakini wamo
 
Usisahau na wakati huo kutazama TV mostly ilikuwa kwa neighbours, na TV nyingi zilikuwa National zile fremu ya mbao....

Wale wenye fweza ndio walikuwa na TV zenye plastic casing...
 
Nakumbuka CTN ikifika mida fulani hv usiku walikuwa wanaonesha muv za kizungu.. dah haha nimeamka sana usiku kuchek muv na nilikuwa napenda sana vipengele vya mahaba aise ilikuwa poa sana..
Walikuwa wanaunga TNT, hapo lazima watu wapigane mikasi
 
Jumapili ilikua ni shivooo na akina bajeee (nguruwe)
Zile tamthilia za mida ya kubeti, akina Barbarita, Tony, Marcidita, Theresita......daaah watoto wa Kilatino wakali saana. Mambo ya Copa Cabana.
.......Acapulco Bay ! Daah walatino wazuri jamanii !
 
Mimi nakumbuka world cup94 Italy ITV walirusha matangazo ya mpira kiufasaa na kulikuwa na tangazo la salama condoms nlikuw nalipenda sana..
 
Back
Top Bottom