Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

CTN walijua kunikamata na Cartoon Network ya kipindi hiko.
Cartoon nyingi za kina Ed, Edd n Eddy, Power Puff Girls, Cow and Chicken, Dexters Labolatory, Winnie the Pooh, etc
Nilifurahia utoto wangu kiukweli.
Hata walipohamisha wakawa wanaonyesha Cartoon Network kupitia DTV pia nilihama nao.
Kwenye maigizo nakumbuka kulikuwa na maigizo ya Marehemu King Mzee Majuto akiwa na kina Marehemu pia Mwanachia na Kistuli.
Maigizo ya Marehemu Mzee Small, Kina Richie Richie pamoja na Jb na kina Cloud, Natasha..
Mambo yalikuwa moto sana kipindi hiko.
 
Nakumbuka wakati mzee anahamia Tabora mwaka 1999 Tv yetu ilikuwa inaonesha chenga tu hakukuwa na Itv kule sasa ikabidi tuwaulize wenyeji wa pale kuwa wanaangaliaga wapi Tausi? Kuna kijana mmoja akasema kesho twendeni niwapeleke,basi si akatupeleka Pale Game park kuangalia Tausi ndege na sio Tamthilia..!
 
Mkuu umenifurahisha sana sasa ilikuwa muda gani wakati anawapeleka huko
 
Nilikuwa naipenda muvi moja ilikuwa inaoneshwa sana ITV ilikuwa ina mtu mkuuubwa kimaumbile na wengine wadooogo walimkama huyo Mkubwa na kumfunga mahala kwenye toroli na baadae aliachiwa ni comedy ila siikumbuki inaitwaje muda kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000...

ID yako tu enzi hizo hilo jina la sabuni lilikuwa maarufu na umaarufu wake ulichaguzwa na tangazo la ITV la "Revola revolaaaaa revolaaaa...."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…